03 July 2012

Watakiwa kusaidia watoto yatima


Na Omary Mngindo, Pwani

WAKAZI wa Kijiji cha Tukamisasa Kata ya Ubena wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani wameombwa kujitokeza kwa hali na mali katika kusaidia watoto waishio
kwenye mazingira hatarishi.


Rai hiyo ilitolewa na mlezi wa Shule ya Msingi Tukamisasa Bw.
Abdallah Nauyai hivi karibuni mjini hapa.

Alisema, hatua hiyo itawezesha watoto hao kuweza kupata huduma muhimu ikiwemo elimu, afya na nyinginezo.

"Katika kijiji chetu kuna watoto waishio katika mazingira hatarishi
wapatao 49 ambao wanahitaji huduma muhimu kama elimu, afya na nyingine
nyingi hivyo ufike wakati tujitoe kwa hali na mali katika kutimiza
hayo,” alisema Mlezi huyo.

Bw. Lutengwe aliwataka wazazi na walezi wa watoto kuwapatia muda wa masomo warejeapo nyumbani na sio kuwatumikisha bila kuwapatia muda wa kujisomea.

Aidha Bw. Lutengwe amewaasa wazazi na walezi wenye tabia ya kuwaficha
watoto wenye ulemavu majumbani ambapo alisema ni kosa kubwa na pindi
watapobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Tutoe taarifa kwa siri kuwabaini wenye tabia hiyo ya kuwaficha watoto
wao wenye ulemevu majumbani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,”
alisema Bw. Lutengwe.

Akifunga sherehe hizo, Mwenyekiti wa kijiji cha Tukamisasa Bw. Shaaban
aliwashukuru wakazi wote aliojitokeza katika sherehe hizo na kujitolea
fedha zao na kufanikisha kupatikana zaidi ya sh. Laki 2 papo hapo
ambazo zitatumika kwa kufungua akanti ya MVCT na shughuli nyingine

No comments:

Post a Comment