23 July 2012
Simba yalizimishwa sare na Vita *Sasa kuivaa Azam robo fainali *Yanga uso kwa uso na Mafunzo
Na Speciroza Joseph
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya michuano ya Kombe la Kagame iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Simba imekuwa ya tatu katika kundi lao, hivyo itakuna na Azam FC ambayo imekuwa ya pili katika kundi B linaloongozwa na Mafunzo ambayo nayo itakutana na Yanga katika mechi ya robo fainali.
Vita ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 35 kwa mkwaju wa penalti uliokwamishwa wavuni na Etekiema Teddy.
Simba ndiyo ilianza kubisha hodi langoni mwa Vita ambapo dakika ya pili Abdallah Juma, akiwa amebaki na lango la Vita alishindwa kutumbukiza mpira kimiani baada ya shuti lake kupaa juu ya lango.
Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi, Antony Ogwayo wa Kenya baada ya beki Juma Nyoso kuunawa mpira akiwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwa Simba.
Awali Vita ilifanya shambulizi la kushtukiza dakika ya 18 ambapo, Ebunga Simbi aliachia kombora lililodakwa na kipa Juma Kaseja.
Dakika ya 22 na 32 ilikosa mabao baada ya Shomari Kapombe mashuti yake kutoka nje ya lango la Vita.
Magola Mapanda wa Vita aliwatoka mabeki wa Simba dakika ya 29, lakini shuti lake likatoka nje ya lango.
Abdallah Juma wa Simba dakika ya 27, alilazimika kutoka nje baada ya kubanwa na msuli na nafasi yake kuchuliwa na Kigi Makasy.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kumtoa kiungo, Kanu Mbiyavanga, Mude wakaingia Haruna Moshi 'Boban' na Salum Kinje.
Vita nayo iliwatoa Teddy, Lema Mabidi na Basilua Makolo na nafasi zao zikachukuliwa na Ngoyi Emomo, Niembe Mkanu na Tshimanga Mutamba.
Mabadiliko hayo yaliisaidia zaidi Simba, ambayo dakika ya 66 Boban aliipatia timu yake bao la kusawazisha baada ya kuunganisha krosi ya Musa Mude.
Dakika ya 90, Simba ilipata penalti iliyotolewa na mwamuzi, Ogwayo baada ya mchezaji mmoja wa Vita kuunawa eneo la hatari lakini, mwakwaju wa Felix Sunzu uliokolewa na kipa Lukong Nelson.
Katika mechi iliyopigwa saa 8 mchana katika uwanja huo Azam FC na Tusker zilitoka suluhu na hivyo kuifanya Azam kupenya robo fainali ambayo itakutana na Simba katika mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment