05 July 2012

Pizo azindua 'Tatanisha'



Na Janath Abdulrahim

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya Deogratius Mlawa ambaye ni maarufu kwa jina la 'Pizo' ameanzisha kikundi cha kuibua vipaji mbalimbali ikiwemo muziki na uigizaji kitakachojulikana kama 'tatanisha'.


Akizungumza Dar es Salaam jana mwanamuziki huyo alisema kikundi hicho kina lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri pamoja na kutafuta vijana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania  ili kuwainua wale wenye vipaji ambao wanakosa sapoti kutoka kwa wadau.

Pizo alisema wameandaa mchakato wa kulitambulisha kundi hilo nchi nzima ambapo wanatarajia kuanza mchakato huo kesho Mjini Morogoro katika vijiji vya Ifakara, Mahenge, Kilombelo na Maleen.

Alisema pia kundi hilo watalitambulisha katika mikoa ya kanda ya ziwa na baadae nchi nzima ambapo pia wanategemea kutangaza vipaji vitakavyopatikana kupitia mchakato huo.

Alisema mara baada ya kupatikana kwa vijana hao watapiga kambi ya miezi sita  mjini Dodoma kwa ajili ya kuviinua vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment