18 July 2012
Mbunge ataka Dkt. Nchimbi afungwe jela *Adai akitoka gerezani, atakuwa balozi mzuri *Vullu: Aibu ofisi ya RPC Pwani kukosa choo
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Ludewa, mkoani Njombe, Bw. Deo Filikunjombe (CCM), amesema Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi na Naibu wake, Bw. Pereira Silima, wanapaswa kufungwa jela mwaka mmoja na baada ya kumaliza kifungo hicho, watakuwa mabalozi wazuri kueleza hali halizi iliyopo katika magereza nchini.
Bw. Filikunjombe aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Mambo wa Ndani Nchi na kusisitiza kuwa, haungi mkono bajeti hiyo kutokana na hali mbaya iliyopo katika magereza mbalimbali nchini likiwemo Gereza la Ludewa.
Alisema anaomba Mungu Dkt. Nchimbi na Bw. Silima wafungwe walau mwaka mmoja gerezani ili waweze kujifunza na kujionea namna wafungwa wanavyodhalilika wanapokuwa magerezani.
“Mheshimiwa Spika, naomba Mungu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Dkt. Nchimbi) na Naibu wake (Bw. Silima), wafungwe gerezani japo mwaka mmoja tu, ili waone hali ya magereza ilivyo tena aje kufungiwa Gereza la Ludewa,” alisema Bw. Filikunjombe.
Aligusia suala la vitendea kazi na kusisitiza kuwa, hali ya vifaa ndani ya jeshi hilo si nzuri kwani hawana vifaa vya kutosha na polisi hawawezi kuendelea kulinda nchi kwa kutumia virungu.
Mbunge wa Mwibara, mkoani Mara, Bw. Kangi Lugola (CCM), alisema hadi sasa silaha kubwa tegemezi ambayo inatumiwa na polisi ni filimbi hivyo bajeti hiyo ndio itaamua uhalifu uendelee au umalikize kupitia.
Alisema wahalifu kwa sasa wanafuatia bajeti hiyo ili kujua polisi wametenga kiasi gani cha bajeti kukabili nao na kuongeza kuwa, hatuwezi kukomesha vitendo hivyo kwa filimbi na vurungu.
“Hatuwezi kuondoa uhalifu kwa kupanua magereza, kuwekwe bajeti madhubuti ya kupambana na uhalifu ambapo majiji makubwa yafungwe kamera maalumu ili kubaini mitandao ya wahalifu.
“Ndani ya Jeshi la Polisi kuna mtandao mkubwa wa uhalifu na ushahidi pamoja na kumtaja mtu mmoja (jina tunalo), kuwa anamtandao wa uhalifu,” alisema.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Bi. Zainab Vullu (CCM), alisema ni aibu hadi leo Ofisi ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Tanga kukosa choo hivyo kutaka hatua za haraka zichukuliwe kurebisha kasoro hiyo.
Alisema mazingira ya askari mkoani humo sio mazuri hivyo wakati umefika kwa Wizara hiyo kufanya ukarabati wa makazi na Vituo vya Polisi ili askari waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KINACHOKUTOFAUTISHA NA WABUNGE WENZAKO NI UELEWA MDOGO WA MFUMO WA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI MARA NYINGI KUNA KITU KINAITWA "COLLECTIVE CABNET RESPONSIBILITY"WABUNGE WA KAMBI FULANI KUWA NAMSIMAMO MMOJA KUTETEA BAJET YAO WANACHOFANYA NI KUIBORESHA HIYO NDIO"PARTY CAUCAS" UNAPOONA MBUNGE ANASAIDIA UPINZANI KUKOSOA BAJET YAO AMBAYO ANGEPASWA AITETEE NA KUIBORESHA NDIO UNAPOTAMBUA WALA HAJUI ATENDALO SIJUI ANAFIKIRI CHAMA KISINGEMPITISHA ANGEKUWA MBUNGE NIMEONA WENGI WAKIANGUKA AWAMU YA PILI UKIPENDA USHAURI USIPOTAKA SI LAZIMA
ReplyDelete