03 July 2012
Hotuba ya Rais Kikwete yawakuna Wanashinyanga
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
BAADHI ya wakazi mjini Shinyanga wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kutokana na hotuba aliyoitoa kwa wananchi juzi na kuelezea msimamo wa serikali juu sakata la mgomo wa madaktari nchini.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti jana mjini hapa, wakazi
hao walisema msimamo uliotangazwa na Rais Kikwete juu ya mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa nchini unastahili kuungwa mkono kwa vile madaktari hao wamekiuka kiapo chao cha kazi.
Wakazi hao walisema, baadhi ya madai ya madaktari yana ukweli wa
kiasi fulani lakini hawakupaswa hasira zao kuzihamishia kwa mtu ambaye hakuwa na ugomvi nao (mwananchi) ambao hawana uwezo wa aina yoyote ya kutekeleza kile kinachodaiwa na madaktari hao.
Bw. Khalid Mlangira mkazi wa Mtaa wa Buzuka Manispaa ya Shinyanga alisema msimamo uliotangazwa na Rais Kikwete ulipaswa kutangazwa mapema na serikali kabla mambo hayajaharibika na kusababisha wananchi wengi wasio na hatia kupoteza maisha baada ya kushindwa kupata matibabu.
Bw. Mlangira aliunga mkono kauli ya Rais Kikwete kwamba, madaktari ndiyo wenye maamuzi ya kufanya kazi kwa mshahara ambao mwajiri amepanga na kwamba kama waliona hautoshi walipaswa kuacha kazi badala ya kugoma na kusababisha madhara kwa watu wengine wasiohusika.
“Mimi napongeza msimamo wa Rais Kikwete, ni kweli madaktari wetu hawakuwa na haja ya kulumbana na mwajiri wao (serikali) kama waliona mshahara wanaolipwa hautoshi wangeacha kazi na kwenda kutafuta maeneo mengine, maana wanapogoma anayeumia si serikali bali ni wananchi wasio na hatia,”
“Nafikiri kwa maelezo ya jana (juzi) ya Rais wetu, ni wazi madaktari wetu watarejea kazini na kuachana na mambo ya mgomo maana vinginevyo wananchi tutaendelea kuteketea, wale wanaoona mishahara haitoshi, ni vyema waache kazi badala ya kugoma na kuzuia serikali kuajiri watumishi wengine,” alisema Bw. Mlangira.
Kwa upande wake Bw. Jonathan Gambile alisema baadhi ya madaktari
wametumia kigezo cha kwamba mgomo wao unatokana na serikali kushindwa kuwapatia vitendea kazi vya kutosha ambapo ukweli wanacholalamikia ni maslahi duni.
Alisema, suala la kudai kwamba wanagoma kutokana na ukosefu wa vitendea kazi na madawa hospitalini siyo kweli maana waliopaswa kugoma kwa hilo ni wananchi wenyewe wanaofika katika hospitali hizo kupatiwa matibabu na siyo madaktari kama walivyofanya maana kugoma wakati kuna wagonjwa wanakufa kwa kukosa huduma ni kuvunja viapo vyao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kila Mtanzania mwenye akili timamu hataungana na madaktari kwenye mgomo wao maana kuwaunga mkono ni sawasawa na kunywa sumu ili ufe. wananchi ndio waliowasomesha hawa madaktari sasa mzozo wao na serikali na kuwatumikia wamafia na wanasiasa nchini ndio zawadi yake kuwaadhibu wananchi wasio na hatia. ni kwa nini msikatae kuwatibu viongozi serikalini mnakataa kuwatibu wananchi walalahoi ambao hawana pesa za kwenda hospital za private? NENO JUMUIA YA MADAKTARI,MAHAKIMU,WACHAGA,WAHAYA,UAMSHO NI HATARI KWA NCHI HII TUNATAKA JUMUIA YA WATANZANIA TU. NDIO MAANA WAKATI WA NYERERE HAKUKUBALIANA NA UPUUZI HUU. RAIS TUNAKUOMBA UPIGE MARUFUKU MADAKTARI WALIOAJIRIWA SERIKALINI KUFANYA PART TIME HOSPITAL BINAFSI,HUENDA ZINAWATIA KIBURI,WANAIBA DAWA NA WANATUMIA VITENDEA KAZI ZA HOSPITAL ZA SERIKALI KUNUFAISHA MATUMBO YAO HALAFU SHUKRANI ZAO NI KUWAKOMOA SERIKALI NA WANANCHI. WANANCHI MSIDANGANYIKE ATI WANATAKA HUDUMA BORA ZA AFYA. NI MTANZANIA YUPI MWENYE MATATIZO AMBAYE HAJADAIWA PESA NA DAKTARI ILI AMTIBU? HIYO NI GERESHA TU WNATUMIA HIYO LUGHA YA KUWAPENDA WANANCHI ILI WAUNGWE MKONO. LAKINI JIULIZE WEWE MWANANCHI ANAYEKUPENDA YUKO TAYARI KUKUACHA UFE HADI MADAI YAO YA PESA NONO YATEKELEZWE> MADAKTARI ONDOKENI HUKO MAHOSPITALINI,KAENDELEENI NA MGOMO MAJUMBANI MWENU AU KWA WAFADHILI WENU WA MGOMO HUU. UBEPARI NI UNYAMA.IWE KWA WANASIASA,VIONGOZI AU MADAKTARI.
ReplyDeleteKwa kweli ni upumbavu kushauri kuwa kama madaktari wanaona kuwa mshahara hautoshi waache kazi na kwenda wanakoona kuna mshahara unaowatosha. Huu ni unyanyasaji wa kitaaluma, na mategemeo ya mtu katika kujitolea katika huduma anayojisikia au kuitwa. Huduma ya afya ni nyeti kama ilivyo huduma ya uongozi wa jamii kama bunge na serikali. Mbona rais, mawaziri na wabunge wanalipwa vizuri, iweje madaktari wanaoponyesha na kuokoa maisha ya watu? Busara inatakiwa katika kuamua swala la madaktari siyo kusema kuwa kama hawataki kufanya kazi waache kazi na kutafuta wanakoona kuna mshahara mzuri. Mbona wewe rais huaachii ngazi pamoja na kushutumiwa kwa makosa mengi yanayokukabili?
ReplyDeleteMAONI NA MTU NA RASILIMALIMTU YANATOFAUTIANA WATU NI WENGI ILA RASILIMALIWATU NI WACHACHE MFANO WAMTU AKIAMBIWA UKIMWI UNAUA ATAJIBU UKIMWI NI SAWA NA UGONJWA MWINGINE ILA RASILIMALIMTU ATAPOKEA USHAURI SISHANGAI KUAMBIWA ZAIDI YA WATANZANIA ASILIMIA 30 NI MAZUZU HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA INAPOFIKIA ZAIDI YA MILIONI40 YA WATANZANIA WANYONGE MASIKINI WAUME KWA WAKE [MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WADOGO ]WANAKUFA ILI MADAKTARI WALIPWE MSHAHARA WA KUANZIA MILIONI SABA KWANI WAKILIPWA NDIO WATAKUPA RUSHWA YA TIBA YA BURE TANZANIA HATUENDELEI TATIZO SIO RASILIMALI MBONA CONGO NI NYINGI KULIKO TANZANIA LAKINI CONGO IKO MWISHO KIUCHUMI DUNIANI TATIZO KUBWA TANZANIA INA WATU WENGI ILA RASILIMALIWATU SIFURI AU KWA MANENO MENGINE IMEJAZA MAZUZU HAWAAJIRIKI HATA MWEKEZAJI AKIJA LABDA WAUZWE UTUMWANI SOMENI JIFUNZENI KUTOKA JAPAN,SWITZERLAND,BELGIUM NA CHINA MUTABAKIA KUBWABWAJA TUACHE SIASA ZA MAJITAKA KWENYE MAISHA YA WATU HATA KAMA NYINYI NI FREEMASON MUSITOE KAFARA WATANZANIA MULAANIWE MUTOKOMEE KWENYE USO WA DUNIA KILA MTU ASIPOANDIKA AU ASIPOZUNGUMZA NI VIGUMU KUMJUA KICHAA MAONI YALIOTANGULIA NI YA KICHAA
ReplyDeleteINASIKITISHA KIONGOZI WA MADAKTARI KUWA MWANASIASA INAMAANA WAGONJWA WOTE BILA KUWA MWANACHAMA WA CHADEMA UTAKOSA HUDUMA ZA TIBA INAKUAJE KUTEKWA KWA DRULIMBOKA KUNAFANANISHWA NA YALIYOWAPATA WABUNGE HIGHNESS KIWIA WA ILEMELA NA SALVATORY MACHEMI WA UKEREWE WANATAKA KUTUAMBIA CHADEMA NDIO WANAOHAMASISHA MADAKTARI WAGOME KUMBE NYIE CHADEMA NI MAGAIDI WAUAJI MAFREEMASON WANAHAMU YA KUNYWA DAMU ZA WATU WALAANIWE KUMTAJA MUNGU BUNGENI NI UNAFIKI HATA LUSIFA ANAMTATAJA MUNGU HAISHANGAZI MATENDO TU YANADHIHISHA
ReplyDelete