06 July 2012

FM Academia kupamba Redd's Miss Morogoro



Na Ramadhan Libenanga , Morogoro .

MASHABIKI wa muziki wa dansi mkoani hapa, wanataarajia kupata burudani ya nguvu kutoka bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' ambao wanatarajia kufanya vitu vya katika mashindano ya Redd's Miss Morogoro yatakayofanyika Julai 13 mwaka huu.


Akizungumza mjini hapa jana Mratibu wa mashindano hayo, Frank Kikambako alisema FM Academia wameahidi kutoa burudani ya nguvu katika mashindano hayo wakati wanyange 15 watakapokuwa wanawania taji la Redd's Miss Morogoro 2012.

Alisema wengine msanii mwingine atakayesindikiza mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia ya Redd's ni Rich  Mavoko.

Kikambako aliwataja washiriki watakaopanda jukwaani siku hiyo kuwa ni Zulfa Vuai, Betrice Joseph, Salvina Kibona na Nancy Reuben.

Wengine ni Mwanahamis Mussa, Sabrina Joseph, Aisha Kuandika, Easter Fred, Joyce Buruhi, Prisca Mengi, Modesta Uwero, Nafia Waziri na Betrice Filbert.

"Tunategemea mashindano ya Miss Morogoro mwaka huu yatatoa warembo watakaouwakilisha vyema mkoa na hata katika fainali za Miss Tanzania 2012," alisema.


No comments:

Post a Comment