23 July 2012

Bao la Boban lamkuna Milovan



Na Speciroza Joseph

BAO la kiungo wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' aliloisawazishia timu yake juzi limemkosha kocha wa timu hiyo, Milovan Cirkovic na kuliita goli bora na kulifananisha na magoli ya wachezaji wa Ulaya.


Milovan alifurahishwa na goli hilo lililofungwa katika dakika ya 66 ya mchezo kati ya AS Vita ya Congo DRC na Simba, Boban alifunga kwa shuti kali akimalizia mpira uliopigwa na mchezaji, Musa Mude na kuifanya Simba kumaliza mchezo huo kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumzia goli hilo kocha Milovan, alisema ni moja kati ya magoli mazuri anayofunga mchezaji huyo na kulilinganisha kama wanayofunga wachezaji wa bara la Ulaya 'Euro Goal'.

"Ni goli zuri sana, hutokea mara chache hasa kwa wachezaji wa nchi za Ulaya, lakini mchezaji wangu kaweza kufunga amenifurahisha," alisema Milovan.

Hili ni goli la kwanza kwa Boban kufunga katika mashindano hayo na goli muhimu kwa timu yake, ambayo bila bao hilo ingepoteza mchezo huo.

No comments:

Post a Comment