12 June 2012
Wajasiriamali 11 wakabidhiwa vifaa
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Safari Lager imekabidhi vitendea kazi mbalimbali kwa wajasiriamali 11 walioshinda kupewa ruzuku za Safari Wezeshwa vyenye thamani ya sh. milioni 50.
Akizungumza katika sherehe za makabidhiano ya vifaa hivyo jijini Arusha jana katika viwanja vya Soweto Meneja wa Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema mashindano hayo ya Wezeshwa na Safari Lager nia yake kubwa ni kuwapatia ruzuku wajasiriamali wadogo na wakati kuendeleza biashara zao.
Shelukindo alisema jumla ya sh. milioni 50 zimetumika katika kununulia vifaa hivyo kwa Kanda ya Kaskazini, ambapo mwaka 2011 ruzuku ilikuwa ni milioni 200 kama vifaa vya vitendea kazi kwa wajasiriamali hao walioshinda katika mashindano hayo.
Alisema utaratibu huo huo ulianzia Mbeya na Arusha na wanatarajia wiki ijayo kuwa Mwanza na mwisho watamalizia Dar es Salaam.
Naye Mgeni rasmi katika sherehe hizo, Niarire Magunda ambaye ni Ofisa Biashara Manispaa ya Arusha, aliipongeza TBL kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kuanzisha programu hiyo yenye nia ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wakati.
Katika sherehe hizo wajasiriamali 11 kutoka Arusha, Moshi na Tanga walikabidhiwa vifaa mbalimbali vya vitendea kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment