12 June 2012
Uchaguzi Yanga SC waiva
Na Elizabeth Mayemba
KAMATI ya Uchaguzi ya Yanga, jana ilitangaza majina ya wagombea wa uchaguzi mdogo wa klabu hiyo ya kujaza nafasi za waliojiuzulu baada ya kupitia vyeti vyao, hivyo yatabandikwa ubaoni keshokutwa ili kutoa nafasi kwa wale wenye pingamizi.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Julai 15, mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu wa kamati hiyo, Francis Kaswahili alisema kati ya majina 29 ya walioomba kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, Abdallah Sharia ambaye ni mkazi wa Zanzibar vyeti vyake hakuwasilisha hivyo ametakiwa kufanya hivyo kabla ya usaili, baada ya mwenyewe kuiomba kamati.
Kaswahili alisema mgombea Mohammed Mbaraka, yeye ameondolewa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa hana sifa.
Kwa upande wa wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti wote wanne wamepita, ambao ni Yusuf Manji, John Jambele, Edgar Chibura na Sarah Ramadhan kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti waliopita ni Ayoub Nyenzi, Clement Sanga, Yono Kevela na Ally Mayai.
Wajumbe waliopita ni Lameck Nyambaya, Ramadhani Kampira, Mohamed Mbaraka 'Binkleb', Ramadhan Said, Edgar Fongo, Ahmed Gao, Beda Tindwa, Jumanne Mwamenywa na George Manyama.
Wengine ni Gadeuncius Ishengoma, Haron Nyanda, Omary Ndula, Shaban Katwila, Justine Baruti, Jamal Kisongo, Peter Haule na Stanley Kevela 'Yono'ambaye pia anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Kaswahili alisema pingamizi kwa walioomba kugombea uongozi litaanza kutolewa Juni 14 hadi 18, mwaka huu na baada ya hapo Kamati za Yanga na TFF zitakaa kupitia pingamizi hizo.
"Tunatoa hadhari kwa wale wote ambao wataleta pingamizi zao wawe na ushahidi wa kutosha, kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao," alisema Kaswahili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment