12 June 2012

Mashabiki wa Chelsea kujipongeza



Na Elizabeth Mayemba

TAWI la Chelsea nchini, limeandaa sherehe za kuipongeza timu ya Chelsea ambayo imenyakua ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya na Kombe la FA.

Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Chelsea Tawi la Dar es Salaam, Cliford Ndimbo alisema sherehe hizo zimepangwa kufanyika Msasani Beach, Dar es Salaam Juni 24, mwaka huu.

"Tumeamua kuanzisha tawi letu la Chelsea hapa nchini, hivyo tumeona ni vyema tuipongeze timu yetu kwa vikombe hivyo ambavyo wamevipata, tunaamini sherehe zetu zitafana sana," alisema Ndimbo.

Alisema pia katika kunogesha sherehe hizo wamewaalika na wapenzi wa Manchester United na wale wa Arsenal, ambapo kutakuwa na mechi kati ya wapenzi wa Chelsea ambao watacheza na timu zote mbili na zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi.

Ndimbo alisema wapo katika harakati za kusajili rasmi tawi lao, ili lijulikane kote duniani na wanaamini watapata wanachama wa kutosha katika kuliendeleza tawi lao.

Alisema kiingilio katika sherehe hizo ni sh. 10,000 kwa kila mtu, pia watoto nao watapata fursa ya kuhudhuria ambapo mwisho wao itakuwa ni saa 12 jioni.

No comments:

Post a Comment