01 June 2012
Kakanko watakiwa kujikwamua na umaskini kupitia kilimo
Na Patrick Mabula, Kigoma
WANANCHI wa Wilaya mpya ya Kakanko mkoani Kigoma wametakiwa kutumia fursa za mipango ya Serikali katika kilimo ili kujikwamua na umaskini na kujiletea maendeleo.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Bw. Christopher Chiza ambaye pia ni Mbunge wa Buyungu Wilaya ya Kakonko aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutobweteka na badala yake kuzitumia fursa za mipango ya Serikali katika kilimo.
Akihutubia wananchi wa wilaya hiyo hivi karibuni Bw. Chiza alitoa onyo kwa watumishi watakaopangwa kufanya kazi wilayani humo kuhakikisha wanawatumikia wananchi katika mipango kupitia fursa za Serikali.
Alisema, Wilaya ya Kakonko ina fursa mbalimbali katika kilimo, hivyo asingependa kuona mtumishi wa umma akifanya kazi kinyume na maelekezo na watu kubweteka badala ya kuchangamkia fursa hizo ili kujikwamua na umaskini,
kujiongezea kipato na kupata maendeleo.
"Ndugu zangu viongozi na wananchi wa Kakonko, nafurahi sana kuona mmeacha itikadi za kisiasa na kujikita katika masuala ya maendeleo, nami naitaka Serikali kuhakikisha inateua watumishi waaminifu na siyo walarushwa," alisema Waziri Chiza.
Katika kuwasaidia wananchi wa Kakonko kujikwamua na umasikini, alisema amekuwa akisisitizia kilimo cha mazao mbadala ya chakula na biashara ikiwemo mpunga, kahawa, alizeti na ufuta.
Kwa upande wake Ofisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya ya Kibondo Bw. Omar Bori, alisema Kakonko ina fursa nyingi hasa katika kilimo kwa sababu mazao mengi ya chakula na biashara hustawi vizuri na kuwaomba wananchi kuzitumia fursa hizo.
**********
3third
Washauriwa kuwajengea
uwezo watoto yatima
Richard Konga na Queen Lema, Arusha
JAMII zimeshauriwa kuachana na uchangiaji wa shughuli za hanasa badala yake ijikite zaidi kuyajali makundi yasiyojiweza hususan watoto yatima na wenye maambukizi ya Ukimwi wanaolelewa bila msaada wa uhakika kwenye vituo vya watoto yatima.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano cha jijini Arusha Bw. Godilizeni Temba wakati kikundi hicho kilipotembelea na kutoa msaada wa vyakula na vinywaji wenye thamani ya shilingi milioni moja kwa vituo viwili vya kulelea watoto yatima mjini hapa.
Vituo hivyo ni pamoja na Sant Lusia kilichopo Moshono kinacholea watoto wenye maambukizi ya ukimwi pekee na Kituo cha Sant Joseph kilichopo Kata ya Mlangarini wilayani Arumeru.
Bw. Temba aliwaomba Watanzania kujijengea utaratibu wa kujisaidia wenyewe na kuachana na dhana iliyojijenga ya kutegemea wafadhili pekee kutoka nje ya nchi ambao wengi wao wamekuwa wababaishaji huku wakiweka masharti magumu na misaada yao.
Aidha, alisema jamii ina kila sababu ya kuguswa na tabu wanayoipata watoto yatima kwani mbali na kukabiliwa na changamoto nyingi kimaisha wamekosa msaada muhimu ya kijikimu hususan elimu bora itakayowasaidia kuondokana na utegemezi hapo baadaye.
Pia alitoa rai kwa kila Mtanzania kwamba jukumu la kuyasaidia makundi hayo ni wajibu wa kila mtu iwapo ataguswa na kujitolewa hata kwa kuchangia mtoto mmoja kila mwaka ikiwepo kumsombesha na kuachana na uchangiaji mkubwa wa hanasa ambao umekuwa ukipoteza fedha nyingi kwa muda mfupi.
"Suala la kuwasaidia watoto ni jukumu la kila mtu ni vizuri basi kwa kila Mtanzania, iwapo ataguswa kwa namna yake na kutoa mchango kwani wengi wetu tumekuwa tukijitoa sana kuchangia harusi za kifahari, bila kujali kuwa michango yetu pia inahitajika kwa makundi mengine muhimu," alisema
Naye Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima cha St.Lucia Bi. Winfrida Mrema alisema kuwa kituo chake kinalea watoto wenye umri wa miaka mwili hadi 10 wenye maambukizi ya VVU na kimekuwa kikikabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa lishe bora kwa watoto hao.
Aidha, kwa upande wa mmiliki wa Kituo cha St.Joseph Sister Crispin Mnate alisema kuwa kituo hicho kina jumla ya watoto yatima 46 na wamekuwa wakilelewa katika mazingira magumu kutokana na kukosa ufadhili wa kudumu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HIVI BADO ELIMU YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA IKO TANZANIA ? KAMA HAIPO NA HAWAKUFUNDISHWA SHULENI KWA VITENDO WAKIWA URAIANI NDIO WAFUNDISHWE KWA NADHARIA TUSIJIDANGANYE MTAALA ULIOPO SHULENI NI KUWAANDAA VIJANA KWA "WHITE COLLAR JOBS" KWANI NANI ASIYEONA VIJANA WAKIMALIZA MAFUNZO MAKELELE NI AJIRA VYAMA VYA SIASA KUAHIDI AJIRA HATA KWA WATU AMBAO KWENYE SOKO LA AJIRA HAWAAJIRIKI KAMA WATANZANIA ASILIMIA 3O HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA HAWA HATA KWA KILMO CHA KISASA HAWAFAI LABDA KUPIGA DEBE STEND ZA MABASI
ReplyDelete