13 June 2012
Giza latanda ujio wa Maximo
Na Victor Mkumbo
ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Marcio Maximo, ameshindwa kuja nchini kama ilivyopangwa kutokana na kumalizia majukumu yake ya kuifundisha Democrata F.C ya Mjini Rio de Jeneiro, Brazil.
Kocha huyo alitarajiwa kutua nchini jana mchana kwa ajili ya kuja kusaini mkataba na mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa timu ya Yanga, Luois Sendeu alisema kocha huyo ameshindwa kuja kama walivyopanga baada ya kutokea dharula na sasa atatua nchini mwishoni mwa wiki hii.
Alisema sababu kubwa iliyomfanya kocha huyo kushindwa kuwasili jana, ni kutokana na timu anayoifundisha kwa sasa ya Democrata F.C kukabiliwa na mchezo mgumu Jumamosi.
"Maximo tayari amekwishatumiwa tiketi ya safari ya kuja hapa nchini, ameshindwa kuwasili leo (jana) kutokana na Klabu yake anayofundisha kukabiliwa na mchezo mgumu,"
Sendeu alisema kuwa Marcio mara baada ya kuwasili nchini atafanya mazungumzo na Uongozi wa Klabu ya Yanga ikiwemo kusaini Mkataba na Klabu ya Yanga kabla ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho.
Wakati gazeti hili, likienda mitamboni lilipata taarifa kwamba timu hiyo haipo tayari kumuacha kirahisi kocha huyo, hivyo hawezi kuja nchini mpaka baadhi ya vitu waviweke sawa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HIVI WAANDISHI WA HABARI NI LINI WATAKUWA WAKIZINGATIA MAADILI YA UANDISHI ZAIDI KULIKO KUZINGATIA BIASHARA KAMA MAXIMO ALIPENDA KURUDI TANZANIA ILIKUAJE RAIS KIKWETE ALIPOKUWA HUKO ASITOE KAULI HIYO NA WALIZUNGUMZA NAYE
ReplyDeleteGazeti hili lilipata taarifa toka wapi..? mbona siwaelewi.... kuweni makini na kazi yenu bana na c kucheza na vichwa vyetu tu...
ReplyDelete