11 June 2012
Catherine ndiye Redd's Miss Changombe
Na Victor Mkumbo
MNYANGE Catherine Masumbigana, juzi ameibuka mshindi wa Redd's Miss Chang'ombe 2012 katika mashindano yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Quality Centre, Dar es Salaam.
Catherine aliweza kuibuka mshindi baada ya kuwashinda wenzake 14 waliokuwa wanawania kinyang'anyiro hicho kwa kujibu maswali vizuri kuliko wenzake.
Katika mashindano hayo ya Redd's Miss Chang'ombe, warembo walioingia katika hatua ya tano bora ndiyo watawakilisha Kitongoji hicho katika mashindano ya Redd's Miss Temeke, ambayo yatafanyika hivi karibuni.
Wanyange ambao waliingia katika hatua ya tano bora ni Catherine, Zulfa Bundala, Jesca Haule, Mariam Ntakisigwa na Flora Kazungu.
Katika mashindano hayo kulikuwa na burudani ya aina yake kutoka kwa bendi ya muziki wa dansi ya Mapacha Watatu pamoja msanii Naseeb Abdul' 'Diamond'.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Jesca Haule, wa tatu Zulfa Bundala, wa nne alikuwa Mariam Ntakisigwa na wa tano ni Flora Kazungu.
Mgeni Rasmi katika mashindano hayo alikuwa Naibu Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla ambaye alisema wadau wa mashindano ya urembo hawana budi kujitokea kwa wingi ili kuweza kuyaboresha zaidi.
Alisema kama mashindano hayo yatatumiwa vizuri, Tanzania itapata warembo bora ambao wataiwakilissha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.
"Wadau na wadhamini hawana budi kuyaboresha zaidi mashindano ya urembo na kubuni mavazi ambayo yatailetea sifa Tanzania katika nyanja mbalimbali," alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment