16 May 2012

Wauguzi Ilala kuanzisha SACCOS


Na Heri Shaaban

WAUGUZI wa Manispaa ya Ilala wameanzisha Chama cha Kuweka na Kukopa SACCOS yenye wanachama 76 kwa ajili ya kuweka amana zao.

Akizungumza na Majira hivi karibuni Ofisa Muuguzi wa Afya ya Jamii Bi.Beauty Obadia aliwataka wauguzi waliopo ndani ya manispaa hiyo kujiunga katika chama hicho waweze kuweka hisa zao.


Bi.Obadia alisema kuwa chama chao kina wanachama  hai 76 na kiwango cha hisa zilizokusanywa zaidi ya milioni 6.

"Fedha hizi tumekusanya kwa kiwango cha hisa 20 kila mwana chama  aliyejiunga katika chama hichi ,"alisema Bi.Obadia.


Aliwaomba watumishi wa manispaa hiyo wajiunge katika benki hiyo ili waweze  kujiendeleza kwa  kuweka na kuchukua mikopo kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Alisema kuwa toka benki hiyo ianzishwe wauguzi wa Ilala imewakomboa kwa kuwainua kiuchumi kutokana na kuchukua mikopo bila riba



No comments:

Post a Comment