09 May 2012

Ushahidi kesi ya Prof. Mahalu wafungwa


Na Agnes Mwaijega

USHAHIDI wa kesi ya kuhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya euro 2.065.827.60 inayokabili aliyekuwa balozi wa Tanzania  Profesa Costa Mahalu na mwenzake Bi.Grace Martin, aliyekuwa Ofisa Utawala wakati huo umefungwa jana.


Hatua hiyo ilifikiwa Dar es Salaam jana baada ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bw.Elvin Mugeta, baada ya kusikiliza ushahidi wa mshtakiwa wa pili, Bi. Martin.

Akitoa ushahidi mahakamani hapo, Bi.Martin alisema tuhuma sita ambazo zinamkabili yeye na Profesa Mahalu hakuna hata moja yenye ukweli.

Alisema kutokana na tuhuma hizo nzito zinazowakabili kutokuwa na ukweli, anaiomba mahakama hiyo kutupilia mbali tuhuma hizo.

Aliogeza kuwa Profesa Mahalu hajaisababishia hasara Serikali kutokana na manunuzi ya jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia na kusisitiza kuwa yeye hajawahi kushirikiana na balozi huyo kufanya njama za wizi.

"Hakuna kosa hata moja ambalo profesa Mahalu alitenda kati ya mashtaka yote yanayomkabili, hajawahi kufanya udanganyifu wa aina yoyote kupitia mikataba ya manunuzi ya jengo hilo," alisema.

Baada ya kumaliza kusikiliza ushahidi wa Bi.Martin, hakimu Bw.Mugeta alisema kesi hiyo itatajwa tena Mei 16, mwaka huu baada ya pande zote kumaliza kufanya majumuhisho.



No comments:

Post a Comment