09 May 2012
Uchumi wahusishwa na ukatili wa kijinsia
Na Daud Magesa, Mwanza
IMEELEZWA kwamba ukatili wa kijinsia kwa watoto ni tatizo kubwa katika jamii linalosababishwa na sababu za kiuchumi na kijamii kutokana na ukosefu wa elimu na uelewa mdogo kuhusu haki za watoto.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijiji Mwanza na Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa mpango wa maboresho ya sekta ya sheria katika Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Wanyenda Philip.
Alisema kuwa, kutolewa kwa elimu hiyo kwa askari polisi ni mwanzo wa kulionyesha tatizo ikizingatiwa kwamba askari hao wanayo nafasi kubwa katika jamii.
Mshauri huyo alisema, tatizo la ukatili wa kijinsia liko katika sura mbalimbali kijamii na kiuchumi hivyo ni vyema jamii ikapewa elimu ya kushughulikia masuala hayo ili kubaini chanzo cha tatizo kuanzia ngazi ya kifamilia na namna ya kulitatua.
“Kutoa elimu ni mwanzo wa kulionyesha tatizo kwa upana wake, elimu hii ianziee ngazi ya familia ili watoto wajuee haki zao. Elimu hii iende katika ngazi mbalimbali kama jeshi la polisi ambao wakipata uelewa na elimu hii watasaidia kupunguza tatizo, kwa kusaidiana na sekta zingine kama magereza, chama cha wanasheria, mahakama, Ofisi ya Mwaanasheria wa serikali ,”alisema Wanyenda
Awali kabla ya kufungwa kwa mafunzo hayo ya siku tano kwa askari 37 wa jeshi hilo mkoani Mwanza Mkuu wa Kitengo cha Jinsia na Watoto, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa polisi Bi. Zuhura Munisi alisema makosa ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ni tatizo kubwa linalohitaji msukumo wa hali ya juu kulitatua kwa kuishirikisha jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment