09 May 2012
Mbunge ashauri wananchi kujiunga VICOBA
Na Stella Aron
WANANCHI wameshauriwa kuachana na dhana ya woga kwa kuhofia kufilisiwa mali zao badala yake wajiunge kwenye Taasisi ya Kuweka na Kukopa (VICOBA) hali itayosaidia kuondokana umasikini .
Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Neema Mgaya kwenye uzinduzi wa kikundi cha Zomboko Vision, Mbagala kilicho chini ya taasisi ya Poverty Fighting Tanzania (PFT).
Alisema kumekuwa na dhana potofu kwa baadhi ya watu na kushindwa kufanya biashara mbalimbali kwa kuhofia mali zao kufiliwa pindi watakaposhindwa kurejesha mikopo.
"Ninawashauri kuachana na imani hiyo hivi sasa kila mmoja anahitaji kuwa na maendeleo na maendeleo yanatokana na upatikanaji wa mikopo hivyo VICOBA haina nia mbaya na wananchi, " alisema
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa PFT Bw. Issa Tunduguru alisema taasisi hiyo ina wanachama 2400 kutoka katika vikundi tofauti tofauti ambapo wanachama wake wamepata mafanikio kutokana na taasisi hiyo.
Alisema PFT ni taasisi inayomjali Mtanzania kwa ajili ya maendeleo hivyo imekuwa ikitoa mikopo bila ya ubaguzi ambapo hivi sasa wanatarajia kutoa sh. milioni 35 kwa kila kikundi ili kuwanufaisha wanachama.
Naye Mwenyekiti wa Zomboko Vision Bw.Eddy Kibona aliwashauri wanachama wa chama hicho kutumia fedha za mkopo kwa maendeleo na si katika kujinufaisha kwenye ulevi ama katika sterehe zingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment