19 March 2012

Twiga Cement kuzalisha zaidi 2012


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Lesoinne Pascal (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni wa mwaka 2011, Bw. Joseph Mabula, wakati wa hafla ya katoa tuzo kwa wafanyakazi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani na Shughuli za Biashara (TUICO) kiwandani hapo, Bw. Myatiro Rusian. (Na Mpigapicha Wetu)

Na Mwandish Wetu
KAMPUNI ya kuzalisha saruji ya Twiga Cement imesema mejipanga kuvuka wastani wa kiwango chake cha kuzalisha saruji kwa mwaka 2012.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa wafanyakazi bora wa mwaka 2011 na siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Twiga Cement, Bi. Jayne Nyimbo alisema wanatarajia kuvuka kiwango hicho mara baada ya kuvuka kiwango cha uzalishaji kila siku.

Alisema sasa kiwanda chao kimeweza kuzalisha takribani tani 5,000 za saruji kwa siku kiasi ambacho kama changamoto zozote hazitatokea, uzalishaji wa saruji utaweza kuvuka kiwango cha uwezo wa kiwanda hicho cha kuzalisha tani milioni 1.4 kwa mwaka. "Kama hadi sasa tuwemeza kuzalisha tani 5,000 basi kutokana na mikakati mbalimbali tuliyojiwekea hatuna shaka tutaweza kuzalisha saruji hata zaidi ya kiwango chetu kama hatutapata changamoto kubwa ikiwa ni upatikanaji wa umeme," alisema. A k i z u n g umz i a s a b a b u y a kuwazawadia wafanyakazi bora wa mwaka jana, Mama Nyimbo alisema hiyo imetokana na ufanisi walioonyesha katika utendaji wao wa kazi wa kila siku akisema hiyo pamoja na kuwapa motisha ya kufanyakazi zaidi lakini pia itatoa changamoto kwa wafanyakazi wengine kuongeza bidii ili nbao kuweza kupata zawadi mwakani.

Mkurugenzi huyo alisema kwa mwaka huu wameweza kutoa zawadi kwa wafanyakazi bora 13 wakiwapa fedha taslimu kila mmoja kiasi cha sh. 350,000/- vyeti za zawadi nyingine. Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPCC, Lesoinne Pascal aliwashukuru wafanyakazi wote wa kampuni hiyo akisema mafanikio ya kiwanda hicho kwa mwa 2011 yametokana na mchango wa kila mmoja kiwandani hapo.

No comments:

Post a Comment