26 January 2012

KATIBU MKUU TUCTA AWATAKA MADAKTARI KUTOKURUDI NYUMA KWA MADAI YAO.


Na Rehema Maigala

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Nicholaus Mgaya  amewataka madaktari wasirudi nyuma katika maslahi ya kuomba haki yao mpaka pale kitakapoeleweka.



Akizungumza na madaktari katika ukumbi wa DonBosco jijini Dar es Salaam, jana Mgaya alisema kama madakatari wameamua kufanya mgomo wa kudai haki zao za msingi ni vizuri washirikiane kwa pamoja ili kupata matunda yaliyo bora.

"Hakuna maslahi yanayopatikana katika sahani ni lazima mpiganie kwa umoja wenu na muwahakikishe akuna hata mmoja kati yenu anayeenda kinyume na nyinyi"alisema Mgaya.

Aliongeza kuwa  Kamati mlizoziunda akikisheni mnaziamini zisije baadae zikanunuliwa na serikali mkakosa pakulilia.

Alisema kuwa yupo tayari kufanya kazi na madaktari ila anachokiomba shughuli hizo zote ziendeshwe kwa kufuata sheria jinsi inavyosema ili tuzae matunda mazuri.

Hata hivyo Mgaya alisema kuwa halikuwa hana taarifa na mgomo wa madaktari ila amehujua kupitia katika magazeti.

"Nilikuwa sielewi chochote kinachoendelea katika Hospitali  ya Taifa ya Muhimbili lakini nilivyosoma katika magazeti ndio nikajua na leo na nimeelezwa yote yanayowasibu"alisema Mgaya.

Vilevile alisema kuwa anajua kuwa Tanzania hakuna haki ya wafanyakazi wapo baadhi ya watu ndio wanaopewa haki kama vile wabunge lakini si mfanyakazi.

Hata hivyo Mgaya aliwambia madakatari kuwa watakapokuwa katika majadiliano na Serikali kuhusu haki zao wafikirie suala la kuludi kazini .

Madaktari waliposikia kauli hiyo waliipinga kwa kupiga makelele katika ukumbi huo.

Vilevile Ofisi ya Waziri Mkuu ilimtuma mwakilishi wake ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Kanda maalumu ya polisi Dar es Salaam ili aje achukue hoja za msingi ili zipelekwe katika ofisi hiyo.

Hata hivyo madaktari hao walikataa na kudai kuwa hawataki mwakilishi yeyote mpaka waonane na Waziri Mkuu.


6 comments:

  1. Watanzania hasa sisi watu wa chini tulishafanywa ndala ambazo huonekana samani yake pale mtu anapohitaji kwenda kuoga ama chooni, tufikirie kazi ya mbunge ni nini na wapi kituo chake cha kazi, kama kituo chake cha kazi ni dodoma kwa nini adai night out allowance kwa ajili ya kwenda kituoni kwake? je vipi kuhusu watumishi wengine ambao nao vituo vya kazi vipo kama vya wabunge? nao wadai posho za aina hiyo? vipi kuhusu walimu, madaktari, maaskari na watumishi wengine wa umma?

    ReplyDelete
  2. Ifike mahali serikali isilaumu tu eti wapinzani wanachochea vurugu si kweli vurugu wanazisababisha wao wenyewe kwa sababu hawatendi haki, hawana utawala bora kama kila siku wanavyotudanganya eti utawala wa haki na sheria ndo wa hivyo?

    ReplyDelete
  3. Ila mwandishi na hiki kiswahili - balaa

    ReplyDelete
  4. kuna haja ya kuangalia mishahara yote , na iwekwe bayana , sio kuficha , kama vile mshahara wa rais na mawaziri kuificha ndio nini? kama ni wakweli kila mshahara wa kila fani uwekwe kwenye mjadala , na watu ambao wanatakiwa na kipato cha juu wawe wasomi , na watu wa chini kabisa kimshahara wawe wanasiasa na viongozi wa serikali kwani wao wana uchungu sana na nchi kwa hio waanze wao kujitolea kwa kukubali mishahara duni

    ReplyDelete
  5. KATIBU MKUU TUCTA ASIWE KAMA VUVUZELA WA SERIKALI. AVAE BUTI AUNGANE NA HAWA MADAKTARI.

    AWAUNNGANISHE WAFANYAKAZI WOTE. KAMA ILIVYO VIUNGO VYA MWILI, JICHO LIKIUMWA NA MWILI WOTE UNA HUSIKA.

    KUNA HAJA YA VYAMA VINGINE VYA WAFANYAKAZI WAWAUNGE MKONO HAWA MADAKTARI. NAO WANA SHIDA HATA KUZIDI MADAKTARI. WA KUWASHAURI NI HUYO KATIBU WA TUCTA. ASIWE MTU WA KWENDA KULA UGALI IKULU.

    HIVI HUYU KATIBU HAONI KUWA WAFANYAKAZI WENGINE KAMA WAALIMU, MANESI, WAFANYAKAZI SERIKALI KUU NA ZA MITAA, NA WA MAKAMPUNI BINAFSI NAO WANA TAABIKA KUHUSIANA NA MISHAHARA AMBAYO HAILINGANI NA MFUMUKO WA BEI?

    KAIBU NA UONGOZI WAKE FANYENI HIMA KUTUTETEA AU SISI WANACHAMA TUTALIA NA NYIE. NYIE SIO CHAMA CHA SIASA. TETEENI MASLAHI YETU. KAMA HAMUWEZI CHAPENI LAPA MWONDOKE.

    ReplyDelete
  6. Mimi niwatahadhalishe serikali yetu kwamba, migomo ndo tu imepangwa leo madaktari na kesho itakuwa kwa wakulima, wachimbaji na wavuvi wakidai kufutwa na kuondolewa kwa uwekezaji usio na faida kwa umma.

    ReplyDelete