26 January 2012

BENKI YA KCB YATOA MISAADA KWA HOSPITALI YA BUGURUNI NA CCBRT.

Na Rehema Mohamed

BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa mbalimbali vya hospitali katika hospitali ya Buguruni na CCBRT vyenye zaidi ya thamani ya sh.milioni 22.3

Akikabidhi msaada huo Dar es Salaam jana katika hospitali ya Buguruni,Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Dokta Edmund Mndolwa alisema hospitali ya Bunguruni ilipata vifaa vyenye thamani ya sh.milioni 8.8 na CCBRT sh.milioni 13.5.

Dkt.Mndolwa alitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni vitanda vya kufanyia upasuaji,Mashine za digitali za kupimia presha na meza ya kufanyia upasuaji wa macho.

Dkt.Mndolwa alisema benki yake inazingatia wajibu wakusaidia jamii inayoizunguka katika sekta ya elimu,mazingira,maafa na afya ili kupunguza umasikini nchini.

Alisema kuwa hivi karibuni benki hiyo pia ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali katika hospitali ya Mwananyamala na Mkuranga wenye thamani ya zaidi ya  sh.milioni 39.

Naye Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bunguruni Dkt.Mwanahawa Lesso aliishukuru KCB Tanzania kwa msaada huo na kusema kuwa bado wanahitaji msaada zaidi kutokana na uhitaji kuwa mkubwa.

Dkt.Lesso alisema inahudumia zaidi ya wananchi 7653  ambapo kwa siku hupokea wagonjwa kati ya 400 hadi 500.

"Hospitali hii hujiendesha kwa kutegemea fedha za ruzuku kutoka serikalini ambazo hazitoshi kulingana na idadi kubwa ya wagonjwa tunaowapokea,hivyo tunashukuru tunapopata misaada kama hii kutoka kwa wafadhili kwani inazuia pale panapokuwa na mapungufu"alisema Dkt.Lesso.


No comments:

Post a Comment