16 December 2011

Makandarasi 5 wapatikana ujenzi Daraja la Kigamboni

Na Nyakasagani Masenza

KAMPUNI tano za Ujenzi zimeingia kwenye mchakato wa ushindani kuwania zabuni ya ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam, baada ya kuthibitishwa kuwa na
vigezo vilivyotakiwa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa zabuni ya ujenzi wa daraja hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Ludovick Mrosso, makampuni hayo yameingia kwenye droo ya mwisho itakayotoa mshindi hivi karibuni.

Alisema bodi ya zabuni ilifikia hatu ya kuteau makampuni hayo baada ya kupitia vigezo vyote vya kitaalamu vilivyotakiwa na waombaji.

Alisema awali kampuni saba za ujenzi zilijitokeza kuomba zabuni hiyo ya kujenga daraja la Kigamboni na kwamba baada ya kutakiwa kuthibitisha uwezo wao kifedha mbili zilijitoa na tano kuthibitisha kuwa na vigezo vilivyotakiwa.

Bw. Mrosso alitaja kampuni hizo kuwa ni Long Jian Road and Bridge Limited ya kichina, Schuan Road and Bridge Group Lilimited pamoja  na China Communication Constructon Limited.

Kampuni nyingine ni China Railway Construction Engineer Group na China Major Bridge Engineer Limited na Chong Qung.

Meneja Miradi wa NSSF, Bw. John Msemo, alisema baada ya kampuni hizo kuthibitisha kuwa na uwezo wa akiba ya fedha za kuanza ujenzi, Kamati itakutana na kupitisha jina la kampuni itakayoanza ujenzi wa daraja hilo.

"Ni matarajio yetu kuwa makandarasi watakaoshinda zabuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni watafanyakazi hiyo kwa ufanisi na wakati uliopangwa, haraka iwezekanavyo," alisisitiza Bw.Msemo.

4 comments:

  1. Why all five (5) are Chinese companies?

    ReplyDelete
  2. Something wrong in this tendering process. It seems equal opportunity for would be qualified contractors is lacking and safety issues and quality are deliberately ignored to satisfy political influence and cheap services.

    ReplyDelete
  3. Hapa napata shida kwani makampuni yote ni ya kichina. Hivi kweli hakuna kaqmpuni lolote toka nchi nyingine lililojitokeza au tatizo ni bei za hadaa zinazotolewa na hawa jamaa kisha usimamizi unakuwa mgumu sana kwani wengi wao hawajui kitu.

    ReplyDelete
  4. Makampuni manne kati ya haya matano ni "state-owned" companies. Kwa hiyo yana uwezo wa kupata pesa kutoka serikalini kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa daraja hilo pasipo kutegemea pesa ya serikali ya Tanzania.

    Kwamba makampuni yote ni ya kichina, si jambo geni kwa kuwa inajulikana inapokuja katika kandarasi za ujenzi kwa pesa zitokanazo na serikali makampuni ya ulaya hawawezi kushindana na makampuni ya china hasa katika gharama na uwezo pia.

    ReplyDelete