Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Bw. Mizengo Pinda, amesema suala la uwekezaji nchini haliwalengi watu wa nje tu, bali hata wa ndani wanaweza kuwekeza hata kwa kiwango
kidogo.
Bw. Pinda aliyasema hayo Dar es Salaam juzi wakati akizungumza na wakazi wa mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Mkoa tarajiwa wa Katavi katika chakula cha jioni ambacho aliwaandalia kwenye makazi yake yaliyopo Oysterbay.
Zaidi ya wakazi 100 kutoka mikoa hiyo walialikwa kushiriki Tamasha la Utamaduni la mikoa ya Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tamasha hilo lilifanyika Novemba 25-27 mwaka huu, katika Kijiji cha Makumbusho.
Alisema yeye alipochukua mkopo waliopatiwa wabunge sh. milioni 90, hakuona haja ya kununua gari bali aliamua kuwekeza katika
ujenzi wa nyumba ya kulala wageni kijijini kwao, Kibaoni, wilayani Mpanda.
“Nilichukua mkopo mwingine benki ya NMB nikaamua kujenga ya vyumba 24 pale kijijini kwetu, sikutaka kuchukua mafundi wazuri kutoka Kariakoo, Dar es Salaam, niliamua kutumia mafundi wa kijijini ili wapate fedha za kununua bati na kuezeka nyumba zao jambo ambalo limewezekana.
“Ujenzi wa vyumba 24 karibu unakamilika, kiasi kingine cha fedha nililima shamba la mahindi nikafanikiwa kuvuna magunia 380,” alisema Bw. Pinda na kuongeza kuwa, aliamua kuuza magunia 300 na kupata sh. milioni 11 ambazo aliziwekeza tena katika mradi wa ufugaji nyuki kijijini kwao na Dodoma.
“Nina mizinga 250 kule Dodoma na Kibaoni mizinga 600, kila mzinga unauzwa sh. 50,000, kila mmoja una uwezo wa kutoa lita 10 za asali, bei ya asali hapa mjini ni sh. 10,000,” alisema.
Aliongeza kuwa, suala la uwekezaji haliepukiki na kumtaja Mbunge wa Mpanda Mjini, Bw. Said Arfi kuwa ni miongoni mwa wawekezaji wadogo kwani ana ekari 200 za mahindi na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Kanali mstaafu, Antonio Mzurikwao, mwenye ekari 100 za mahindi.
Alisema Taifa bado linakabiliwa na changamoto ya kupunguza umaskini kwa kuhahakikisha kuna uzalishaji wa chakula cha kutosha ili watu washibe lakini uzalishaji huo unapaswa kuwa na tija ili wakulima wapate mazao mengi na kujiongezea kipato.
Mwisho.
4444444
4TH:
Waliokwama Mto wa Mbu wandelea na safari
Na Said Njuki, Monduli
BAADHI ya abiria walioshindwa kuendelea na safari baada ya mafuriko kukata mawasiliano ya barabara katika Mji Mdogo wa Mtu wa Mbu, Wilaya Monduli, mkoani Arusha, hatimaye wamefanikiwa kuendelea na safari baada ya eneo hilo kufanyiwa ukarabati.
Mbali ya abiria hao, baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambao walikimbia nyumba zao, jana walianza kurejea katika makazi yao na kuiomba Serikali iwape misaada mbalimbali.
Akizungumza na Majira jana, Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Magesa Mulongo, alisema hali ni shwari katika eneo hilo kwani idadi kubwa ya wakazi wa mji huo, wamerudi katika nyumba zao na wasafiri waliokwama, waliendelea na safari zao.
Alisema tathimini ya hasara iliyotokana na mvua hizo, inafanywa na kamati maalumu ya maafa ambapo timu ya madaktari imepiga kambi eneo hilo ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko.
“Maendeleo ni mazuri, barabara ilianza kutumika tangu jana (juzi) jioni, maji yamepungua katika makazi ya watu ambao wengi wao wamerejea katika nyumba zao,” alisema.
Alitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo, kuhama mara moja kwani taarifa ya utabiri wa hali ya hewa inasema mvua hizo zitaendelea hadi mwezi ujao.
Alzitaja kampuni zilizotoa msaada kwa waathirika kuwa ni Monaban Trading & Farmers Ltd, ambayo ilitoa tani tano za unga wa sembe ambapo mfanyabiashara Bw. Kareem Dalia na wenzake, wametoa tani mbili za mchele, tani moja sukari, kilo 300 za maharage, katoni 10 za mafuta ya kupikia, katoni 10 za sabubi na katoni 10 za tambi wakati Serikali mimetoa tani tano za unga wa sembe na Benki ya NMB ikiahidi sh. milioni 10.
No comments:
Post a Comment