15 November 2011

Tutabomoa nyumba zote maeneo yaliyovamiwa-CDA

Na Pendo Mtibuche, Dodoma

MAMLAKA ya Ustawishaji Makao Makuu Makao Makuu Dodoma (CDA) imesisitiza kuwa maeneo yote yameliyovamiwa na watu kinyume cha sheria hata kama ni kwa kushawishiwa na baadhi ya watu kuwadanganya kuwasaidia ni lazima yabomolewe.


kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mipango CDA Bw.John Mtema, na kutaja baadhi ya maeneo yaliyovamiwa kuwa ni Itega, Mbuyuni, Kwamwatano, Nkhungu, Bochela, Mbwanga, Mtube,Maili Mbili, Swaswa, Ipagala, Ilazo ,Ng’ong’ona, Ntyuka, Dodoma Makulu na Njedengwa.

Alisema kutokana na hali hiyo ya baadhi ya watu kuwadanganya wananchi wamekuwa wakipata wakati mgumu mno na kushindwa kuwadhibiti wananchi ambao wamekuwa wakivamia maeneo yaliyowazi kwani uvamizi huo huanza na nyumba moja na baadaye kuongezeka kwa kasi.

Alisema hali hiyo ilisababisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Reheme Nchimbi, kufanya ziara kutembelea maeneo hayo na kujionea uvamizi na kuzitaka mamlaka husika kueleza kuwa ni kwa nini hukaa kimya pale wanapoona uvamizi huo umefanyika hadi kufikia kuvunjia wananchi hao nyumba zao kwa kutumia jeshi la polisi.

Alisema ni lazima kamati za ulinzi na usalama zitumike katika kazi ya kuwahamisha wananchi katika maeneo yaliyovamiwa kwa kuwa kamati hizo zipo kuanzia ngazi ya Kata hadi Mkoa.

Alisema CDA pia inasikitishwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wa ngazi hizo kuwaacha wananchi kuvunja sheria kwa kuvamia maeneo ambayo hayaruhusiwi kujengwa nyumbaa za makazi au hata maeneo ya umma yaliyotengwa kwa kazi maalum.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Hazina ambaye pia eneo lake ilivamiwa Bw. Peter Ishebabi, alisema wao waliomba eneo hilo kujenga shule ya sekondari lakini walijibiwa na CDA kuwa eneo hilo ni kwa ajili ya Taasisi lakini baada ya muda walishanaga kuona wananchi wakivamia eneo hilo na kuanza kujenga.

Alidai wakati mwingine viongozi wa kata wakati mgumu kuwaondoa au kuwafukuza wananchi kuvamia maeneo kwa kuwa wanadai kupewa na mamlaka hiyo.

4 comments:

  1. cda iliavyanzishwa kulikua kunaishi fisi tu Dodoma? Ina maana Wagogo hawakuepo? Mimi naona walikuwepo. Walikuwa wanaishi angani au ardhini. CDA ni wazembe, mafisadi. Miaka zaidi ya 36 walifanya kazi ya miaka 5 tuu. Ivunjwe kazi ya kupanga mji wa Dodoma wapewe manispaa. Mbona manispaa na halmashauri nyingine zinafanya vizuri sana katika kupanga maeneo yao?

    ReplyDelete
  2. serikali inashiriki katika kudidimiza maendeleo ya nchi yake. watu wapo mbele kimaendeleo kuliko serikali. inashindwa kutekeleza majukumu yake ya upimaji viwanja hasa CDA badala yake inafikiria kubomoa nyumba za watu waliopata fedha lakini serikali ikashindwa kuwapatia viwanja. Inafikiria kuteketeza mamilioni ya wananchi wake yaaliyowekezwa, badala ya kuwasidia kuendeleza maendeleo yao kwa kisingizio cha kuvamia. Walioharibu wanaoharibu miji ni serikali. Ni mwananchi gani aliyepewa kiwanja akakataa badala yake anaenda kuvamia. Uvamizi mnausababisha ninyi wenyewe. Kama ni vita acha iwe vita ya serikali na wanachi wake. Huwezi kucheleesha maendeleo yangu, wakati huna kasi ya kukabiliana na changamoto za maendeleo.

    ReplyDelete
  3. mimi hawa CDA ninawashangaa. mimi ni mkazi wa Dodoma na pia ni mtuymishi wa serekali. ninachojiuliza ni kwamba kwanini awali ya yote CDA wasikiri UDHAIFU WAO wa kushindwa kuwapatia Raia viwanja? je mara ya mwisho waligawa viwanja ilikuwa lini? walipima kule ITEga na kuviuza kwa gharama zaidi ya milioni tano kimoja...hivi vilikwenda kwa waheshimiwa na matajiri wenye fedha.... hakuna shida, wakatangaza kuwa watu waje wajiandikishe kupata viwanja, watu kuanzia usiku wa manane wakalala kwenye foleni. matokeo yake walipoandikisha watu wasiozidi kumi wakatangaza vimekwisha na kuanza kutumia FFU kupiga mabomu raia na waliwaumiza wengi katika sakata hilo....

    kama CDA wana afisa mipango, kwanza ilibidi wajiulize

    i. je wamehahi kutangaza watu kujiandikisha kupata viwanja watu nwakakata kwenda?

    ii. je mara ya mwisho ni lini waliandikisha viwanja na ilichukua muda gani hadi walipowapatia?

    iii. je wanadhani kwa sababu yoyote watu wangevamia kama viwanja vingekuwa vinapatikana na si katika mazingira ya rushwa?

    iv. je wanalitambua ongezeko halisi la watu dodoma kwa vigezo vya kidemografia na hivyo kukabiliana na kasi ya mahitaji ya viwanja?

    v. je wanalitambua ongezeko la watu mjini dodoma kisera kutokana na ukweli kuwa sasa umekuwa rasmi mji wa vyuo?

    WAKIPATA MAJIBU YA MASWALI YOTE HAYO, WANGEKUWA WAUNGWANA NA KUKIRI UDHAIFU WAO, KISHA KUTAFUTA MUSTAKABALI NA WANANCHI KAMA WANAVYOFANYA MAENEO MENGINE....

    KAMA HAWALIONI HILO BASI NA SHIRIKA HILI LIVUNJWE!

    ReplyDelete
  4. wafanye hivyo tu lakini maamusi mengine yanadai eti ni sheria, lakini utamaduni wa maali na nguvu za Mungu vyapaswa kuangaliwa. Kuna maamuzi mengine yafananayo na kumuua mtoto kilema kwa ulemavu wake. Makazi yasipimwa yako sehemu nyingi tu duniani na hayatisha (labda kinadharia) kwa kuwa si kila kitu ni kibaya na kulaumiwa kwa kiasi wanachofikia cha CDA hata kukosa utu! Unabomoa nyumba ya mtu kwa kisingizio cha sheria? Ngojea uone kuwa Mungu si dhalimu kama wewe! wanaotoa maamuzi ya aina hii wasome historia ya waliowatangulia CDA!

    ReplyDelete