Na Amina Athumani
KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC), imesema aihusiki na kuvurugika kwa kozi ya kimataifa ya ngumi za ridhaa iliyoahirishwa.TOC imesema
wanaohusika ni Shirikisho la Kimataifa la Ngumi (AIBA), pamoja na mkufunzi wao kutoka Algeria, Azzedin Aggoune.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi alisema anashangaa kuona washiriki wa kozi hiyo wakiitupia lawama TOC kwamba wanahusika kuvurugika kwa mafunzo hayo, jambo ambalo limewasikitisha.
Alisema chanzo cha kuvurugika kwa kozi hiyo, kimetokana na mkufunzi aliyependekezwa na AIBA kuendesha kozi hiyo kutotokea na kuiahirisha hiyo zaidi ya mara moja.
Bayi alisema BFT walitakiwa kuandaa mafunzo hayo tangu mwaka 2010, lakini kutokana na shirikisho hilo kufungiwa na AIBA kutokana na tuhumza za dawa za kulenya, lililowakumba viongozi na mabondia wa taifa hayakuweza kufanyika.
Alisema baada ya BFT kurudishiwa uanachama wake AIBA Februari 28 mwaka 2010 katika mkutano wa AIBA, TOC na BFT walipanga mafunzo hayo yafanyike Januari mwaka huu, lakini hayakufanyika baada ya kushindwa kumpata mkufunzi.
Katika hatua nyingine BFT inatarajia kuwachukulia hatua washiriki wa kozi hiyo, walioonesha utovu wa nidhamu baada kushindwa kufanyika.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema hawataweza kuendelea nao kwa kuwa wanaweza kuonesha utovu wa nidhamu sehemu nyingine na kulitia aibu taifa.
No comments:
Post a Comment