MLINZI John Terry juzi alimwomba kocha Fabio Capello amchague katika timu ya taifa licha ya madai kuwa alimfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi Anton Ferdinand.
Terry ameiambia FA kuwa hana hatia na anataka kuiongoza timu ya England, inayonolewa na Capello itatakayocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Hispania na Sweden katika Uwanja wa Wembley.
Beki huyo amekanusha madai kuwa alimtolea maneno makali na kufanya vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya Ferdinand wakati Chelsea ilipopigwa bao 1-0 dhidi ya QPR Oktoba 23, mwaka huu.
Jumanne, polisi walithibitisha kawu wanachunguza madai ya ubaguzi wa rangi.
Terry mwenye miaka 30, atahojiwa na polisi juu ya madai ya yeye kumtusi Ferdinand, huku ikidaiwa alionekana akibana pua mbele yake.
Uwezekano wa kuitwa katika kikosi hicho Jumapili ni nusu kwa nusu, Rio Ferdinand ambaye ni patina wa muda mrefu na Terry, katika timu ya taifa alivaa beji ambayo inaeleza kupiga vita ubaguzi wa rangi wakati United, ilipocheza dhidi ya Otelul Galati katika mechi ya Ligi ya Mabingwa na kushinda mabao 2-0 katika Uwanja wa Old Trafford.
Kitendo hicho kinaonekana kuwa anamuunga mkono ndugu yake Anton, kitu kinachoonesha kuwa wanaweza wasielewane kwenye kambi ya England kama watakwua pamoja.
No comments:
Post a Comment