Na Andrew Ignas
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni kaimu Ukuu wa wilaya ya Temeke BW. Jordan Lugimbani amewataka viongozi wa serikali kuhakikisha wana simamia na kulinda rasilimali mbali mbali ili ziweze kuwanufaisha vizazi vijazo.
Zaidi ya miradi kumi (10) maendeleo ambayo imeghalimu bil 2.2 imezinduliwa rasmi jana na kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru Bi Mtumwa Rashidi Khalfan.
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Temeke jana wakati wa sherehe za kupokea mwenge wa uhuru ambao kitaifa utaazimishwa Dec 1 Mkuu huyo amesema viongozi wa serikali wanawajibu wa kuhakikisha Miradi aliyoanzishwa anatunza ili ije kunuisha vizazi vijavyo.
"Temeke inajukumu la kusimamia na kutunza miradi hii ya maendeleo ambayo imeanzishwa na taasisi pamoja na serikali ili ije kuwanufaisha vizazi vijavyo "alisema Lugimbani.
Alisema kuwa ili Taifa liweze kukua haraka kimaendeleo ni lazima kusaminiwa kwanza kwa rasilimali zilizopo.
Hata hivyo Bw. Lugimbani amewataka vijana kupitia kauli mbiu ya mbio hizo ya Tanzania Tumethubutu,Tunaweza na Tunasongambele iwe changamoto ya kupambana dhidi ya vita ya ukimwi,Madawa ya kulevya na umaskini.
'Changamoto kubwa bado inawakumba vijana juu ya maambukizi ya ukimwi,Madawa ya kulevya na Umaskini hivyo ni jukumu letu wote kuhakikisha tunaikabili hali hiyo.
Aidha kwa upande mwingine Mkuu wa wilaya hiyo ametoa rai kwa maafisa wa elimu wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam juu ili kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa huu Bw. Said Meck sadiki juu ya nyongeza ya vyumba vya madarasa ili waweze kwa kipindi kijacho ongezeko la kufaulu la asilimia 100 wapate nafasi.
No comments:
Post a Comment