Queen lema, na Pamella Mollel, Arusha
UPANDE wa utetezi katika kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umewasilisha
pingamizi la kuitaka mahakama kufuta kesi hiyo kwa madai kuwa haoni utoshelezi wa kisheria ya mashitaka yanawakabili wateja wake.
Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo Bw. Methody kimomogoro na Bw.Albert Sando, waliwasilisha pingamizi hiyo mahakamani hapo jana mbele ya hakimu Daudi Magesa.
Baada ya pingamizi hiyo kuwailishwa Hakimu Magesa aliahirisha kesi hiyo hadi December 20 atapotoa maamuzi kuhusu pingamizi hilo.
Bw. Kimomogoro alidai mahakamani hapo kuwa mashitaka yanayowakabili watuhumiwa ambao ni wateja wake hayana msingi kisheria kwa madai kuwa toka hapo awali walitoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa masaa mengi zaidi kabla.
Wakili Kimomogoro aliendekea kudai mahakamani hapo kuwa kosa na shitaka la pili ambalo linawakabili wateja wake ambalo ni kufanya mkusanyiko ambalo ni la kukaidi amri halali ya polisi alidai kuwa nalo halina msingi kwa madai kuwa hati imeshindwa kutaja na kufafanua zaidi juu ya amri hiyo kutoka kwa jeshi la polisi.
Alidai kuwa makosa mengineyo nayo yanayowakabili wateja wake pia hayaioneshi na kufafanua zadi juu ya makosa ya nayowakabilikwa mujibu wa sheria jambo ambalo halina maslahi kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment