28 November 2011

JK ateta na CHADEMA Ikulu

Na Mwandishi Wetu
Rais Jakaya Kikwete (kulia), akiangalia ripoti ya mapendekezo ya katiba mpya iliyowasilishwa kwake na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe Ikulu, Dar es Salaam jana.

HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw. Freeman Mbowe, ameongoza ujumbe wa chama
chake iliyoteuliwa na Kamati kuu kuonana na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu kuwasilisha maoni yao kuhusu muswada wa sheria ya kuundwa kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.

Bw.Mbowe na ujumbe wake waliwasili Ikulu alasiri na kumkabidhi kwanza Rais Kikwete mapendekezo yao kisha kupiga picha na kuanza mkutano ambao hata hivyo wana habari hawakuruhusiwa kuhudhuria.

Hata hivyo habari kutoka katika kikao hicho zilieleza kuwa ilikuwa na mafanikio makubwa ya maelewano kati ya pande zote mbili.

Hata hivyo hadi tunakwenda mtamboni hakukuwa na taarifa rasmi ya kilichojiri katika kikao hicho.

Viongozi walioandamana na Bw. Mbowe kwenda Ikuli kama ni pamoja na Makamu wake Bara Bw. Said Arfi, Makamu wake Tanzania Visiwani Bw. Said Issa Mohamed, Mshauri wa masuala ya siasa wa CHADEMA Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Abdallah Safari, Mnadhimu wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni Bw. Tundu Lisu,ambaye pia ni Katibu wa Kamati hiyo pamoja na Mbunge wa Ubunge Bw. John Mnyika.

7 comments:

  1. Ndio maana watu wanampenda Rais Kikwete. Hafuati upepo, ni msikivu na ana umakini tofauti na hisia potofu za watu wengine. Hongera JK.

    ReplyDelete
  2. Maoni No. 2
    Kama Rais Kikwete atasikia la Mkuu yaani mawazo na matakwa ya Chadema na Watanzania wote,basi sote tukubali kuwa kumbe si 100% mtu mbaya, ila amezungukwa na wabaya wanaompotosha au ameweza kuona alama ya nyakati. Tusubiri tuone kama atanusuru machafuko au la.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na msemaji kwamba JK ni msikivu.Baadhi ya wanaomzunguka wanaweza kuwa tatizo. Nakupongeza sana Rais kwa hili.Wazo la akatiba mpya lilipondwa na wanaomsaidia lakini kwa usikivu wake kakubala kuwepo kwa katiba mpya. Ongera JK, ongera CHADEMA ndizo siasa tunataka.

    ReplyDelete
  4. Mwandishi wa makala hii ameiandika kiushabiki na wal si kiuandishi. Kichwa cha maneno kinasema JK ateta na CHADEMA, kisha anasema kikao kilikuwa na mafanikio. Wewe mwandishi huitakii mema Tanzania au pengine hujui kiswahili

    ReplyDelete
  5. kuna namna hawa chadema wanataka kuleta vurugu nchini kama watasikilizwa ,

    ReplyDelete
  6. na wale zanzibar mbona mmekaa kimya katiba mpya inataka kuundwa , mbona hamzungumzi masuala ya muungano , mafuta , na mengineyo mmekaa kimya au mshakula chochote ?

    ReplyDelete
  7. Baba Ridhiwani si msikivu na upepo wa uchama unampiga machoni, kwa mambo ambayo si lazima uwe na digrii ili ujue si sahihi yeye haoni aidha kwasababu hana uwezo huo au hauoni kwasababu ameamua asione kwa manufaa yake na mwanae.

    ReplyDelete