*Mama naye afariki Dunia
Na Mwandishi Wetu
SIKU moja baada ya Famili ya Bw. John Mashauri, wa Kijiji cha Mwabaluhi, wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, kupoteza
watoto wawili Aisha John (2) na Shida Jonh(10) kwa kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu Mama wa familia hiyo Bi. Monika Mashauri (25) naye amefariki dunia.
Mama huyo alifariki dunia jana saa 12 asubuhi wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo alikolazwa juzi baada ya kula chakula hicho na familia yake hivyo kuongeza simanzi isiyo na kifani katika familia na kijiji hicho kwa ujumla.
Vifo hivyo vimesababisha Diwani wa Kata hiyo,Bw. Paulo Lubongeja, kububujikwa na machozi na kujitolea kugharimia mazishi ya watoto hao na baadaye kupata taarifa za kifo cha mama watoto hao.
Wanafamilia hao walikula chakula hicho usiku wa kuamkia Novemba 23, mwaka huu saa mbili usiku siku iliyofuata walianza kujihisi kuugua matumbo lakini walivumilia hadi siku ya ijumaa saa 5 usiku wa kuamkia juzi walianza kujisikia vibaya na kudai chakula walichokula hakikuwa kizuri.
Ofisa mtendaji wa kata hiyo,Bw. Jastine Masasi, alisema siku hiyo walikula ugali na samaki na baadaye waliugua ghafla hivyo kupelekwa katika hospitali ya wilaya kwa ajili ya matibabu lakini baada ya kufika mtoto mmoja alifariki dunia kabla ya kupata matibabu.
Waliolazwa ni, Robert John (6) na, Richard John (3) na Maico John (4)aliruhusiwa baada ya kupata nafuu.
Mtendaji huyo alifafanua kuwa baada ya kula chakula hicho na kuhisi kuugua matumbo walianza kutapika na kuharisha hadi walipofikishwa hospiatalini kupata matibabu.
"Ni manjonzi kweli, tumechanganyikiwa watu kupuputika hivi, jana
tulizika na idadi ya watu ilikuwa kubwa na kila mmoja alijiuliza kuhusu msiba huo na chakula walichokula," alieleza Bw.Masasi.
Awali akizungumza na waandishi wa habari akiwa wodini kabla ya kufariki dunia Bi. Mshauri alisema "Mchana nilipika ugali na samaki tukawa tumekula na usiku nilipika pia tulienda kulala na ilipofika saa 5 usiku nilianza kujihisi chakula hakikiwa kizuri na siku iliyofuata watoto wangu wote walianza kuharisha na kutapika na ndipo tulikuja hospitalini hapa kuangalia vipimo," alisema Bi. Monika
Mganga Mkuu Wilaya Dkt. Boniventure Ndaki, alisema chakula walichokula haki jachulikana kama ilikuwa na na kudai kuwa uchunguzi wa kubaini sumu hiyo unaendelea ambapo vipimo vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali mkoa wa Mwanza kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Bw. Liberatus Barrow, alipotafutwa kwa njia ya simu kuzugumzia tukio hilo simu yake iliita na baadaye kukatwa bila kupokelewa.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Sengerema (OCD), Bw. Pundensiana Protas, alipopigiwa simu yake ya mkononi alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema "Nenda hosptalini utapata maelezo yote' na alipoulizwa chanzo cha tukio hilialikata simu.
No comments:
Post a Comment