30 November 2011

JK asaini Muswada Katiba Mpya

*Asema nafasi ya kuuboresha bado ipo wazi
*Wanaharakati wapinga, waishukia CHADEMA


Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, jana amesaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya 2011, uliopitishwa na Bunge mjini
Dodoma, Novemba 18 mwaka huu.

Hatua ya Rais Kikwete kusaini muswada huo, inakamilisha safari ndefu ya mchakato wa kutungwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba hivyo kusubiri kuanza kutumia.

Kusainiwa kwa muswada huo kunafungua awamu ya pili ya mchakato wa kuandikwa Katiba Mpya kwa kuundwa Tume ya Kukusanya maoni ambayo pia itamshirikisha Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilisema kusainiwa kwa muswada huo ili uwe sheria ni hatua kubwa na muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya.

Awali katika salamu zake kwa wananchi Desemba 31 mwaka jana, Rais Kikwete aliwaahidi Watanzania kuwa atawapatia Katiba Mpya kabla ya kumaliza muda wake wa utawala mwaka 2015.

Taarifa ya Ikuku iliongeza kuwa, pamoja na kusainiwa kwa muswada huo kuwa sheria bado, serikali itaendelea kusikiliza maoni, mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

“Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yeyote mwenye maoni au mawazo ya namna ya kuboresha sheria hii, ajisikie huru kutoa maoni yake na serikali itasilikiza na kuchukua hatua zinazostahili,” ilisema taarifa hiyo.

Katika mazungumzo kati yake na Kamati Maalumu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), juzi Rais Kikwete alikihakikishia chama hicho kuwa serikali itaendelea kupokea maoni mbalimbali ya wadau ili kuboresha sheria hiyo kwa maslahi ya Taifa.

Jukwaa la Katiba lazidi kupinga

Wakati huo huo, Rehema Maigala anaripoti kuwa, Jukwaa la Katiba Tanzania limemsihi Rais Jakaya Kikwete, asisaini muswada huo.

Jukwaa hilo limedai kuwa, makubaliano yaliyofikiwa na CHADEMA pamoja na Rais Kikwete kuhusu muswada huo, yameongeza hamasa ya jukwaa hilo kufanya maandamano.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa jukwaa hilo Bw. Deus Kibamba, alisema maandamano yapo pale pale kwa madai kuwa hivi sasa hoja za msingi za kufanya maandamano zimeongezeka.

“Tunaona wazi kuwa kuwa wanasiasa wanataka kuwaandikia Watanzania katiba mpya kitu ambacho hakiwezekani, hii ni mojawapo ya hoja za msingi kushinikiza maandamano.

“Wananchi hatutaki katiba yetu iandikwe na wanasiasa kwa sababu tunaona mazungumzo ya Rais na CHADEMA, yanataka kufika mwafaka wa wao kuandika Katiba ya Tanzania bila kushirikisha wananchi,” alisema Bw. Kibamba.

6 comments:

  1. Watanznia kuweni macho na Hili Jukwaa la Katiba haliwatakii mema watanzania. Ukweli huyu Kibamba pamoja na wenzake wanatumiwa ili kuleta hali tete katika kuelekea Mchakato wa kupata Katiba Mpya. Ukweli hao wanaowasemea siyo watanzania wote. Hizo ni Ngo zisizokuwa na wanachama wapo kwa ajili ya matumbo yao. Nikikundi kidogo sana na wala Msiwafumbie macho wawekeni sehemu tukimaliza kutengeneza katiba yetu waende kwa baba zao wakaseme vizuri. Nampongeza Kikwete Rais kwa kuwa makini na kuelewa matakwa ya watanzania. Tudumishe Amani na Utulivu wetu katika kupata Katiba Mpya. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  2. Sitoshangaa kama nikisikia hao wanajiita jukwaa la katiba ni mamluki wanaotumiwa kutaka kutuvurugia amani yetu.Viongozi wa serikali NA wa Chadema wamelitolea maelezo mazuri kabisa jambo hili.Sasa hao akina Kibamba wanachotaka ni nini hasa?TUNAZIDI KUMUOMBA MUNGU AIBARIKI NCHI YETU NA ATUEPUSHE NA MABALAA YA AKINA KIBAMBA

    ReplyDelete
  3. kwanza mbona hamtuambii sisi wananchi huu muswada unasema nini kwa uwazi? mnasainishana vitu mnavyovijua wenyewe. Kumwingiza Rais Sheni kwenye hio tume ni danganya zanzibar , mwingizeni mtu kama Mbunge Jussa asiegopa chochote na yuko mbali na kubebwa kwa rushwa na vyeo.Kila nchi iwe na katiba yake kwanza zanzibar na Tanganyika ,halafu ndio iundwe katiba ya muungano , msibabaishe watu.

    ReplyDelete
  4. KIBAMBA NENDA NA WEWE IKULU KAONANE NA KIKWETE, KWANI SHIDA NI NINI! TUNACHOTAKA NI KATIBA MPYA KWA AMANI.nJIA YA MWONGO NI FUPI TU, KAMA KWELI RAIS SI MKWELI TUTAJUA TU NA NDIPO TUANDAMANE FULL KULALA BARABARANI MPAKA KIELEWEKE.

    ReplyDelete
  5. Chadema wanamshutumu JK kwa kupenyeza issues zingine za katiba kinyemela. Sasa mbona walisaini, au hawakusoma vizuri walichosaini?

    ReplyDelete
  6. acheni uloda katiba inataka kutufanya kama kenya chadema mtulie bwana bado vijana wadogo wengine tunataka life zaidi nchi ikigombana si itakuwa kama rwada.

    ReplyDelete