*Wafuasi wake 53 pia waliuawa
TRIPOLI, Libya
WAKATI Baraza la Mpito la Libya limekubali mwili wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi
uchunguzwe, miili mingine 53 ya wafuasi wake watiifu imepatikana karibu na hotelini katika mji alikozaliwa wa Sirte ikionekana imenyongwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la haki za binadamu la (Human Rights Watch), baadhi ya waliouawa walikuwa wamefungwa mikono na waliuawa wiki iliyopita.
Shirika hilo lilisema hayo yanasemekana ndiyo malalamiko ambayo yamejitokeza karibuni, tangu pande mbili za wafuasi hao wa Gaddafi na waasi wa NTC kupigana vita vilivyodumu kwa takribani miezi minane.
Utawala mpya wa Libya umekanusha kuhusika na mauaji hayo na kuwaomba Walibya kutokubali kulipiza vizasi, lakini umekubali kuunda tume kuchunguza mazingira ya kifo cha Gaddafi.
Kuhundulika kwa maiti hizo, kunakuja siku moja baada ya sherehe kubwa kufanyika nchi nzima juzi baada ya NTC kutangaza serikali mpya siku tatu baada ya kifo cha Kanali Gaddafi.
Baraza la Taifa la Mpito (NTC) limeshinikizwa kufanya uchunguzi juu ya namna ambavyo kifo hicho kilitokea baada ya kuonekana kwamba majeshi ya waasi yalimkamata Gaddafi akiwa hai na kumuua baadaye.
Mwili wake umehifadhiwa eneo la Misrata ambalo lipo wazi kwa ajili ya wananchi kumuona.
Wauawa wamefungwa mikono
Mihili hiyo 53 ilipatikana juzi ikiwa imetekelezwa katika Hoteli ya Mahari mjini Sirte, ambako ndipo mapigano makali yalitokea mwishoni mwa wiki mara baada ya NTC kupambana ili kuuteka mji.
“Hali hii inapaswa kuchukuliwa hatua haraka, mamlaka ya Libya inapaswa kufanyia uchunguzi haya yaliyotokea na waliohusika wachukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.
"Baadhi yao wamefungiwa mikono nyuma kabla ya kupigwa risasi," alisema Bw. Peter Bouckaert, Mkurugenzi wa Kitengo cha Maafa cha HRW kupitia taarifa yake.
"Ushahidi unaonesha kuwa baadhi ya waathirika walipigwa risasi wakati bado wakiwa wameshikiliwa kama wafungwa, wakati eneo hili la Sirte likiwa chini ya utawala wa waasi ambao ndiyo walichukua nafasi ya kuongoza NTC," alisema Bouckaert.
Kujenga upya Libya
Katika hotuba yake ya Jumapili katika mji wa Benghazi, kiongozi NTC Mustafa Abdul Jalil alitoa wito kwa Walibya kuweka kando vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya kujenga nchi mpya yao.
"Leo sisi ni mwili mmoja, taifa moja, sisi tumeungana sasa, kuliko tulivyokuwa siku za nyuma," alisema.
"Ninatoa wito kwa kila mmoja kutoa msamaha, kuvumiliana, na maridhiano ni lazima kuondokana na chuki na wivu. Hili ni jambo muhimu kwa mafanikio ya mapinduzi na mafanikio ya Libya baadaye." aliongeza.
Kifo chake kuchunguzwa
Baraza la mpito la Libya (NTC) limetoa amri ya kuchunguzwa tukio la kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo, Muammar Gaddaf baada ya kubanwa na vyombo mbalimbali vya kimataifa.
Tume ya uchunguizi inaundwa kuchunguza mauaji ya kiongozi huyo aliyekamatwa akiwa hai, na wapiganaji wa NTC nje kidogo ya mji wa Sirte alikozaliwa Alhamisi iliyopita, na kuuawa kwa risasi baadaye, akiwa njiani anapelekwa Misrata.
"Tumesikiliza mahitaji ya mataifa mbalimbali, tumeanza kuunda tume ya kuchunguza mazingira ya kifo cha Muammar Gaddafi baada ya kukamatwa," Bw. Mustafa Abdel Jalil, kiongozi wa NTC, alisema katika mkutano na wanahabari mjini Bengazi jana.
Serikali ya Mpito
Abdel Jalil pia alitangaza kuwa mchakato wa kuunda serikali ya mpito umekwishaanza na utakamilika ndani ya wiki mbili.
*Wafuasi wake 53 pia waliuawa
TRIPOLI, Libya
WAKATI Baraza la Mpito la Libya limekubali mwili wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi uchunguzwe, miili mingine 53 ya wafuasi wake watiifu imepatikana karibu na hotelini katika mji alikozaliwa wa Sirte ikionekana imenyongwa.

Alisema raia wote wa Libya walikuwa wanapata kiongozi hiyo ashtakiwe kwa makosa aliyowafanyia. Kwa mauaji, kutupa watu rumande, kutumia vibaya utajiri wa Libya... au kutumia utajiri huo kuwakandamiza watu wa Libya.
Hata hivyo, alisema Gaddafi anaweza kuwa aliuawa na wafuasi wake watiifu ili kuepuka kuunganishwa naye katika mashtaka. BBC/Aljazeera

Wamemuua kwa vile alitaka mafuta yake wapewe wa-africa pekee na siyo wazungu. Hakuwa na hatia hata kidogo. Kila mtu alikuwa akiishi kwa amani japokuwa kuna watu wake walikuwa waki-kiuka sheria mara chache. Kuna maana gani mtu umesha mshika mzima, badala ya kumfungulia kesi unamuua. Huo ni uonevu, basi hayo mafuta yataibiwa kila siku bila wao waarabu wa Libya kujua kwa vile wana nunuliwa na kuchonganishwa wao kwa wao. Inauma sana kumuua Ghadafi, inauma mno kusema kweli nime wachukia sana Wamarekani na washirika wao.
ReplyDeleteKwa nini viongozi waliopo kwenye mafuta tena waafrica tu ndio wanao fuatawa fuatwa kwenye nchi zao kwa uchokozi na kisha kuuawa? Mbona kwao ulaya hawaui mtu au sisi waafrica ni kama mbwa kwao hatuna thamani??? Waafrica, tuamke tunapoona mwenzetu anatendewa mabaya kama haya.
Viongozi wa ntc ni vibaraka wa nato. gharama za nato zitalipwa kwa kutumia mafuta ya libya.nato hawawezi kufanya kazi yote bure. lazimwa watalipwa na ntc
ReplyDelete