CCM , CHADEMA mchuano mkali
•Awali CHADEMA walifurika mitaani kushangilia
•CCM yageuza kibao matokeo ya vijijini
•Utulivu watawala katika upigaji kura
Na Waandishi Wetu,Igunga
MATOKEO ya awali ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga yalianza kupatikana jana jioni na hadi tunakwenda mi tamboni Chama cha Demokrasia na Maendeleo k i l i k uwa
k i n a o n g o z a kikifuatiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku CUF ikijikongoja kwa mbali. Kutokana matokeo hayo ya awali yaliyoonesha kuwa Chadema kilikuwa kinaongoza katika vituo vingi vya mjini, mashabiki wa chama hicho waliingia mitaani mjini Igunga na kuanza kushangilia wakisema kutokana na mawasiliano waliyokuwa wanafanya katika maeneo mbalimbali walikuwa wameshinda.
Mji mzima ulijaa mashabiki wa Chadema huku vyama vingine vikiwa kimya, hali iliyowapa polisi wakati mgumu kuhakikisha ulinzi unakuwapo. Wakati tunakwenda mitamboni, baada ya kupata matokeo ya kata za vijijini ilionekana CCM kuigeuzia kibao CHADEMA kwa kupata kura nyingi na kuwepo uwezekano mkubwa CCM kuibuka na ushindi.
Matokeo ya baadhi ya vituo ambavyo matokeo yalikuwa yamepatikana ni 1. Mtendaji na. 1 ambapo CCM ilipata kura 63, Chadema 73 na
CUF 6.
Kituo cha Mtendaji na.2 CCM ilipata kura 65, Chadema 86, CUF 8 na DP kura moja; wakati kituo cha Ujenzi na. 1 CCM ilipata kura 80, Chadema 95, CUF 3, DP 2 na Sauti ya Umma (SAU) 1.
Katika kituo cha Ujenzi na. 2 Chadema ilipata 111, CCM 76
CUF 7, DP 1; Kituo cha Ujenzi na. 3 Chadema iliongoza kwa kura 104, CCM 70.
Kwenye Kituo cha Mpongolo Chadema ilipata kura 31, CCM 40 CUF 1; wakati kwenye kituo cha Elimu na. 1 Chadema 104, CCM 37, CUF 3 na Elimu na.2 Chadema ilizoa 95, CCM 48 na
CUF ikaambulia kura 2.
Matokeo hayo yalizidi kuonesha kuwa kwenye kituo cha Ntingu Chadema na CCM zilifungana kwa 63 zikafuatiwa na CUF iliyoambulia kura moja.
Katika Kituo cha Malindi na.1 Chadema ilipata kura 31, CCM 59, CUF 3; wakati kwenye Kituo cha Mwaloli Chadema ilipata 59, CCM 21 na CUF 7.
Kwenye Kituo cha Stoo ya Pamba na. 1 Chadema ilipata kura 79, CCM 84 na CUF 1; Stoo ya Pamba na. 2 Chadema iliongoza kwa kura 72, CCM 70 na CUF kura 2.
Kwenye Kata ya Ziba S/m na. 1 Chadema ilipata kura 57, CCM 59, CUF 6 wakati katika kituo cha Ziba S/m 2 Chadema ilipata kura 63, CCM 73, CUF 9; Kituo cha Chipukizi Chadema 71 na CCM 91.
Katika Kituo cha Ziba na. 6 Chadema ilipata kura 47, CCM 62 na CUF 7; Nyandekwe na. 1 Chadema ilipata 7 na CCM 19.
Mambo hayakuwa tofauti katika kituo cha Chidiso na. 1 ambapo Chadema ilipata 45, CCM 38 na CUF 6; wakati Kituo cha Chidiso na. 2 Chadema ilipata 49, CCM 46 na CUF 10.
Kituo cha Nyandekwe S/m na. 1 Chadema ilipata 104, CCM 70, CUF 7, DP 1, SAU 1; wakati kituo cha Katibu Tarafa (na. 5) CCM 87 Chadema 84, CUF 3 DP 1; Katibu Tarafa (na. 4) CCM 61 Chadema 88, CUF 6 na DP 1.
Katika Kituo cha Umoja CCM ilipata kura 3, Chadema 84 na
CUF 1; Ushirika CCM kura 26 na Chadema 86; Chipukizi na. 1 Chadema 91, CCM 71 na CUF 11.
Kwenye Kituo cha Chipikizi 2, Chadema ilizoa kura 108, CCM 77 na CUF 4; Geti maji na. 1 Chadema 111, CCM 84 na CUF 7; Geti Maji na. 2 Chadema 98, CCM 87 na CUF 7
Kituo cha Igunga S/m CCM 70, Chadema 99, CUF 3; Ofisi ya Kata CCM 65, Chadema 86, CUF 5; Sekondari Mwanzugi CCM 66, Chadema 54, na CUF 4.
Kituo cha Chajana na. 1 Chadema 66, CCM 32, CUF 1; Chajana na. 2 Chadema 43, CCM 27, CUF 1, Chausta 1;
Nyandekwa na. 4 Chadema 101, CCM 80, CUF 1;
Ikungisima S/m Chadema 120, CCM 128, CUF 6, Chausta 1 na
SAU 3.
Kura nyingine ni za Kituo cha Busomeke S/m na. 2 Chadema 77, CCM 60, CUF 2; Mwisi na. 1 Chadema 56, CCM 59 na CUF 2; Ndembezi na. 1 Chadema 63, CCM 63, Chausta 1; Igoweko na. 1 CCM 1, Chadema 74 na CUF 23.
Pia yalikuwapo matokeo ya vituo vya Masanga na. 1, CCM 56, Chadema 96 na CUF 1; Masanga na. 2 Chadema 73 na CCM 60;
Kinungu na. 1 Chadema 75 na CCM 51; Kinungu S/m na.2 Chadema 78 na CCM 53.
Matokeo mengine yalikuwa ya Kituo cha Simbo SM ambapo Chadema ilipata kura 87, CCM 29, CUF 11 na DP 1; wakati Kituo cha Bukoko Chadema ilipata 41, CCM 59 na CUF 1.
Kwa haya matokeo inaonyesha wazi kabisa Chadema ndio alistahili ushindi Igunga. CCM wamechakachua
ReplyDeleteCCM MMECHAKACHUA
ReplyDeleteNdugu zangu napenda kuwafahamisha kwamba njia ni nyeupe kwa CHADEMA miaka michache ijayo kutokana na idadi ya kura nyingi ilizopata Igunga, inaonyesha watu wanazidi kuvutiwa na sera nzuri za chama hiki, hivyo kuna matumaini makubwa mno labda pengine CHADEMA kizidi kujipanga zaidi hususani maeneo ya vijijini wapeleke elimu ya uraia kwa wapiga kura na tena wapange bajeti yakudumu na si ya muda mfupi maana kwa kufanya hivyo watu watawaelewa na kuwafahamu vizuri kama wanavyojipambanua ccm.Binafsi sishabikii ccm hata kidogo nikimuona mtu amevaa tisheti,kofia au khanga za ccm moyo unachukia mno huwa natamani kumvua mtu aliyevaa.
ReplyDeletejamani wizi wa ccm ni mpaka lini?dawa yao iko jikoni wasubiri 2015.
ReplyDelete