Na Timothy Itembe, Rorya
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani hapa Tarime kimeibuka kidedea katika Uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata tau kati ya nne zilizofanya uchaguzi huo
juzi Octoba 02.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Rorya Bw.Cousmas Ngangaji, mgombea wa CCM Kata ya Nyahongo Bw. Mussa Hezeroni, aliibuka mshindi kwa kupata kura 1343 huku wa NCCR Mageuzi Bw. Elyasi Masiku akifuata kwa kura 1137.
Alisema mgombea wa CHADEMA Bw. Edward Sokoine, alipata kura 968 na kwamba jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 3529 kati ya wapiga 9069 waliojiandikisha.
Katika Kata ya Nyamtinga alisema mgombea wa CCM Bw.Rubago Oguku, aliibuka mshindi kwa kura 1, 328 akifuatiwa na wa CHADEMA Bw.Jombo Agati aliyepata kura 890.
Kwa upande wa Kata ya Mkoma mgombea wa CHADEMA Bw.Kitori Razaro, aliwashinda wapinzani wenzake kwa kupata kura 1,716 huku Bw. Joashi Waryoba CCM akifuta kwa kura 1559.
Alisema mgombea wa NCCR Mageuzi Bw.Abiasaph Ryoba alipata kura 234.
Kwa upande wa Wilaya ya Tarime Kata ya Susuni mgombea wa CCM Bw. Bonifasi Marwa, alibuka mshindi kwa kura 1,255 kati ya 2,218 zilizopigwa akifuatiwa na wa CHADEMA Bw. Abiuld Lukasi pamoja na CUF Bw. Emanuel Sabure.
Msimamizi wa uchaguzi katika kata hiyo Bw. Fidels Lumato, alisema hali ya uchaguzi ilienda vizuri na hakuna malalamiko yoyote.
No comments:
Post a Comment