Na Agnes Mwaijega
WIZARA ya Kilimo, Chakula na Ushirika, imesema ili kukabiliana na uhaba wa sukari nchini, Serikali imesitisha leseni ya kuuza sukari nje ya nchi.Vilevile imeanua
kuagiza tani 120,000 za sukari kutoka nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa sukari.
Kiasi hicho kinajumuisha tani 20,000 ambazo tayari zilikuwa kwenye mchakato wa kuingizwa nchini kutoka nchi za SADC katika kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kiasi kingine cha tani 100,000 ambacho kitaingizwa kutoka vyanzo mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw.Mohamed Muya alisema upatikanaji wa sukari nchini umekuwa sio wa kuridhisha kutokana na sukari kuvushwa na kuuzwa kwa magendo Kenya na Uganda na kusababisha upungufu wa sukari kwenye soko la ndani.
"Serikali imeamua kuchukua hatua hii ambazo ni za dharura ili kuhakikisha nchi inakuwa na sukari ya kutosha," alisema.
Pia alisema leseni za kuingiza sukari hiyo, zitatolewa kwa wafanyabiashara wengi kupitia taratibu na kanuni za sukari ili kuhakikisha sukari itakayoingizwa nchini inawafikia walengwa.
Hata hivyo alisisitiza kuwa hakuna mfanyabiashara yeyote atakayepewa leseni ya kuingiza sukari zaidi ya tani 5,000.
Alisisitiza kuwa, utaratibu wa kuagiza sukari utawashirikisha maafisa tawala wa mikoa ya pembezoni mwa nchi ikiwamo Mtwara,Ruvuma,Mbeya na Rukwa ili kuhakikisha sukari inapatikana katika maeneo hayo.
"Katika hatua hii ya kukabiliana na upungungufu wa sukari serikali itahakikisha inatuatilia kwa karibu wale wote watakaopewa jukumu la kuagiza sukari kuhakikikisha wanafanya hivyo na kuisambaza nchi nzima," alisema.
Hata hivyo alisema katika hatua za kati za kukabiliana na tatizo la uhaba wa sukari nchini serikali imeunda kikosi kazi cha wataalamu watakaofanya utafiti wa taratibu za soko la sukari na ukokotoaji wa bei ya sukari ili kuishauri serikali juu ya hatua stahiki za kuchuka ili kuikabili changamoto iliyopo.
"Tathimini za upatikanaji wa sukari pamoja na bei yake nchini imebainisha kwamba bei ya sukari imepanda kutoka bei elekezi ya sh.1,700 iliyokubaliwa na wadau katika kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu Machi mwaka huu," alisema.
Kwa hatua za muda mrefu Bw.Muya alisema serikali inaendelea na utekelezaji wa mikakati ya kuongeza uzalishaji wa sukari kwa kiasi kisichopungua tani 550,000.
Mfumuko wa bei ni ishara kwamba viongozi wameshindwa kudhibiti nchi. Mh. Mkapa aliwahi kusema kwamba kama kiongozi "ukishindwa kudhibiti soko ni udhaifu." Mh. Mkapa alijitahidi sana kuzuia mfumuko wa bei.
ReplyDeletemaoni yako si kweli; naomba ujue mkapa ndiye anayewatesa watanzania na sukari kwa sababu viwanda vyote ana hisa, na kiwanda mtibwa na kagera ni chake ila Nassoro amewekwa kama kibarua wa kuwanyanyasa na kuwadhulumu watu.
ReplyDeletena kwa sasa ndio wanaosababisha shida ya sukari, wanafanya mchezo, sukari inahamishwa leo kwenda kagera, kesho inakwenda mtibwa, kesho kutwa pale huku wakiipeleka nje.
msiwe mbumbu, nenda mkindo kwenye hekalu la mkapa
AMA KWELI KUKOSA AKILI NI PIGO KWA MWANAADAMU,HAWA WACHAGA NDIO WASAFIRISHAJI WAKUBWA WA SUKARI KWA MAGENDO,WANASUMBUA WATU KWA WIZI,MAGENDO NA SASA SIASA. OLE WENU WATANZANIA MTAKOMA NA HAWA NI BALAA MNO HAWA TOKA ENZI NA ENZI
ReplyDeleteKama huna maoni ya maana hakuna haja ya kuandika ujinga.Hivi viwanda vyote vya sukari vinamilikiwa na wachaga?Kama serikali inajua ya kuwa sukari inauzwa Kenya na Uganda kwanini isiweke ulinzi wa kutosha mipakani.Tulikuwa na matatizo na Tanzanite ikaja issue ya magogo na sasa ni sukari na kesho utasikia kitu kingine.Hii nchi yetu ni kama haina viongozi maana naona wamelala usingizi na wanachojua wao ni kuingia mikataba mibovu na kula posho tu.
ReplyDelete