Na Rehema Maigala
BAADHI ya wakazi wa Kunduchi Mtongani Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam waliobomolewa nyumba zao na Jeshi la Polisi wamemaliza hasira zao kwa kuvunja Ofisi ya
Serikali ya Mitaa na kuwapiga baadhi ya watendaji wa ofisi hiyo.
Wananchi hao walifikia hatua hiyo kwa madai kuwa mwenyekiti wa mtaa wa Kunduchi ndiye chanzo cha nyumba zao kubomolewa.
Uvunjaji wa ofisi hiyo ulianza jana saa 8 mchana, huku wakazi hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali pamoja na vifaa vya kubomolea.
Baadhi ya mabango hayo yalisomeka "Mwenyekiti ndio chanzo cha kubomolewa hatutakuacha mpaka kieleweke".
Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Kata ya Kunduchi Mtongani, Bi. Janeth Lite alisema baadhi ya wakazi hao walivamia ofisi hiyo na kuchana nyaraka mbalimbali za ofisi.
"Wamevamia katika ofisi za serikali ya Mtaa na ile Mtendaji na kuchana nyaraka mbalimbali pamoja na kuwapiga vibao baadhi ya watendaji," alisema diwani huyo.
Alisema kitendo hicho kimesababisha hasara kubwa pamoja na upotevu wa baadhi ya nyaraka muhimu za serikali.
"Tunasubiri ni hatua gani itachukuliwa kutoka kwa polisi ili kufahamu ni akina nani waliohusika na kitendo hicho, baada ya uvunjaji walikimbia," alisema.
Wakati huo huo. Mwandishi wetu David John anaripoti kuwa Mbunge wa Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposya amewahakikishia wananchi wa jimbo hilo kuwa atatekeleza ahadi zote alizoweka wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa kuwa ni deni kwake.
Amesema anatambua analo deni kubwa la kulipa fadhila ya watu wa jimbo hilo kwa kumwamini na kumpa dhamana ya kuongoza jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutekeleza kila alichoahidi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jana, alisema anajukumu kubwa la kuhakikisha anafanya aliyoahidi kwa wapiga kura wake baada ya kuingia madarakani.
Tatizo la gazeti hili halina mhariri, wote wamekalia ufisadi wa habari za kupenda mishiko; Waliounjiwa maana yake nini?
ReplyDeleteBado miezi mwili litakufa hili, hata kiswahili hamjui.