21 September 2011

SHIMMUTA yaipongeza Taifa Queens

Na Mwali Ibrahim

SHIRIKISHO la Michezo la Mashirika ya Umma na Kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), limeipongeza timu ya taifa ya netiboli 'Taifa Queens' kwa
kutwaa medali ya fedha katika mashindano ya Afrika yaliyomalizika Maputo nchini Msumbiji wiki iliyopita.

Kwa medali hiyo, Taifa Queens ilishika nafasi ya pili na kuiwezesha Tanzania kushika nafasi ya 15, katika michuano hiyo.

Katika michuano hiyo Tanzania pia iliwakilishwa na timu za judo, ngumi za ridhaa, kuogelea, soka la wanawake na michezo ya walemavu (PARALALIMPI), ambazo hata hivyo hazikufua dafu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Katibu Mkuu wa SHIMMUTA Award Safari, alisema wanaipongeza timu hiyo kwa kuiwakilisha vyema nchi katika mashindano hayo makubwa.

Alisema licha ya kuiwakilisha nchi, pia wachezaji wa timu hiyo wanastahili pongezi kutokana na ari, nidhamu ya hali ya juu waliyoionesha tangu walipokuwa kambini kwao kabla ya kwenda hadi katika mashindano hayo.

"Walistaihili pia kupata ushindi wa kwanza na kutwaa medali ya dhahabu, lakini inawezekana kuna mahali kiufundi walikosea ila nina imani wamepaona na watapafanyia kazi, hatuwezi kuficha hisia zetu za kutoa pongezi kwao," alisema Award.

Alisema wanawapongeza uongozi wa vyama cha Netiboli Tanzania Bara(CHANETA) na cha Zanzibr (CHANEZA) kwa kushirikiana na mafanikio makubwa barani Afrika.

No comments:

Post a Comment