15 September 2011

Padri naye ajitosa kampeni za Igunga

Na Moses Mabula, Igunga

KANISA Katoliki wilayani Igunga limewataka wagombea ubunge pamoja na vyama vyao, kuhakikisha kwamba ahadi wanazozitoa kwa wananchi wakati huu wa
kampeni zitatekelezeka.

Wito huo ulitolewa jana mjni Igunga Paroko wa kanisa Katoliki Wilaya ya Igunga Padri Joseph Maziku alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni zinazoendelea kuwania ubunge jimbo hilo.

Alisema kuwa mara nyingi kumekuwa na ahadi hewa kwa wananchi kutoka vyama vya siasa na hasa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni kwa kujinadi lakini mara nyingi zimekuwa hazitekelezeki kabisa.

“CCM sasa wazinduke, na wasome alama za nyakati wananchi wengi hivi sasa hawadanganyiki kwa maneno mazuri bila kuona vitendo, mimi huo ndio ushauri wangu wa bure,” alisisitiza Padri Mziku.

Padri Maziku aliwakata wananchi wa Jimbo la Igunga kupima sera kwa kila chama ili wanaone ni chama gani kinaweza kuwaletea ukombozi ambao umekuwepo kwa muda mrefu, hususani kero mbalimbali zikiwemo ukosefu wa pembejeo kwa jili ya kilmo cha zao la pamba.

Kiongozi huyo wa kiroho alisema moja ya matatizo ambayo yamekuwa yakiwakabili wa wananchi wa Igunga ni daraja la Mto wa Mbutu ambalo limekuwa kero kubwa na ya muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na kusababisha wakazi wa maeneyo hayo kuwa 'kisiwani' wakati wa masika.

Kuhusu siku ya kupiga kura Padri huyo aliwaomba waumuni wa kanisa hilo kujitokeza kwa wingi kupiga kuga kura ili waweze kuchagua kiongozi mzuri wanayemuhitaji wao bila kupewa shinikizo kutoka kwa mtu yoyote.

6 comments:

  1. Sawa baba wa Kiriho, umeichapa CCM kiaina!

    ReplyDelete
  2. Tulisema hawa wana chama mkabisha sasa linaanza kujitokeza hadharani.

    huwezi kuficha unacho amini/penda kwani kitajulikana ktk matendo yako

    ReplyDelete
  3. Paroko Joseph Maziku mbona una vunja sheria na utaratibu wa kanisa lako? Mapadre hamruhusiwi kupiga kura za maoni, wala kuonyesha upande unaoupendelea wala kuuchukia. Hilo daima huwa ni siri ya mtu. Imekuwaje sasa ukaanza kutamka majina waziwazi? Unapoteza umakini wa kanisa lako. Kama una uhakika na namna ya kuongea chagua kukaa kimya "in order to be at a safer position". Baba pengo waangalie pia na hawa wasije wakatuingiza katika malumbano yasiyo na maana.Tunajua kuwa "a human person is a political animal" LAKINI usipitilize na kujisahau.

    ReplyDelete
  4. Nyie waandishi tafakarini kabla ya kuandika. Mnataka kuchonganisha watu na vyama. Paroko alitoa maoni yake na huo wala sio msimamo wa Kanisa Katoriki. Huyu ni mtu aliyeongea kama mtu. Tunasikitika kuwaambia wananchi wa Igunga kuwa Paroko amejikanyaga kidogo. Tumhurumie.

    ReplyDelete
  5. KANISA Katoliki wilayani Igunga limesema kuwa 'mara nyingi kumekuwa na ahadi hewa kwa wananchi kutoka vyama vya siasa na hasa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni kwa kujinadi lakini mara nyingi zimekuwa hazitekelezeki kabisa'.

    Duh! Sasa mlikua mnabisha kitu gani? Jambo lipo wazi kabisa kua chadema ni chama cha kanisa katoliki. hapa paroko wayani igunga anawaelekeza waumini wa kanisa hilo kujitokeza kwa wingi kupiga kuga kura ili waweze kuchagua kiongozi mzuri. Hapo kanisa linakwenda nje ya malengo yake.

    ReplyDelete
  6. Oya ucpotezee sms kwa CCM na padri amawataka CCM wajirekebishe, wachague maneno ya kuongea ili wasiharibikiwe, yawezekana na yeye pia ni mwenzao, m cjui,

    hatahivyo, hajataja chama kingine ili akipe ushaur kama alivyofanya kwa CCM, so cjui mmemweka padri kuwa ni mwanachama wa chama gani hicho?

    Even though, ni m2 mwenye maslahi binafsi, anayefuata mkumbo, mwenye akili mgando au anayetumia akili za m2 mwingine ndiye aweza kuwa MSHABIKI AU MKEREKETWA AU AKASHAWISHI WATU WAICHAGUE CCM kwa hali halisi ya maisha ya watanzania wa sasa, NASEMA UONGO??????????????

    ReplyDelete