19 September 2011

CHADEMA yajivunia kumkamata DC Igunga

*Yadai kikao alichokuwa akiendesha cha uhalifu
*Yajipanga kuwapigania waliokamatwa hadi wachiwe
*Mgombea CUF alaani DC Kimario kupingwa hadharani


Na Benjamin Masese, Igunga

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kilikuwa sahihi  kumkamata na
kumdhibiti Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Bi. Fatuma Kimario, kutokana na kuingilia mkutano wake kinyume cha sheria ili kulinda amani kwa kuwa kikao alichokuwa akiendesha kilikuwa cha uhalifu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa CHADEMAhama, Bw.Tundu Lissu, alisema uamuzi huo unatokana na maadili ya uchaguzi ambayo  yanazuia viongozi wa serikali kujihusisha na kampeni wakitumia rasilimali za serikali kwa manufaa ya chama tawala.

Alisema Bi. Kimario  hana mamlaka yoyote ya kisheria ya kupokea barua za maombi ya watu kwa ajili ya kusimamia uchaguzi kazi ambayo alikuwa akifanya.

“Chadema ilikuwa halali kumdhibiti Bi.  Kimario kwa sababu kama angeendelea kufanya kikao pale angeweza kuhatarisha amani na utulivu…nawaambia kwamba maadili ya uchaguzi yanawazuia viongozi wa serikali, mawaziri, ma-RC na ma-DC kufanya shughuli zozote za serikali zinazoendana na serikali…tunasikitika kuona jeshi letu limewakamata viongozi wetu," alisema Bw. Lissu na kuongeza;

"Waliotumia mamlaka yao kisheria kama raia kukamata wahalifu pale wanapokutwa wakifanya uhalifu, lakini hakuna polisi karibu, sasa inaonekana polisi wamejigeuza kuwa mkono wa mabavu wa CCM , baadala ya kuwa walinzi wa sheria za Tanzania,”alisema Bw.Lissu

Alisema mkuu huyo wa wilaya aliburuzwa  kwa sababu aligoma kutii amri halali ya kujisalimisha, ndipo wananchi na viongozi wakatumia mamlaka ya uraia kumdhibiti kwa sababu alikuwa anajadili suala la uchaguzi.

Alisema wabunge waliokamatwa  Bw. Sylvester Kasulumbayi (Maswa Mashariki) na Bi. Suzan Kiwango (Viti Maalum), hawana kosa lolote  la kujibu mahakamani kutokana na mambo hayo kutokea kila chaguzi zinapofanyika.

 “Kama kawaida polisi wanajificha ya taarifa za kiintelejensia  kujaribu kuhalalisha kitendo hiki,kila mwenye macho na kila mwenye kuona ni kutaka kuona viongozi wetu hawapati msaada wa wakili pamoja na wadhamini ambao wangeupata kirahisi katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga,

Alisema kama wabunge hao leo hawatapewa dhamana ambayo ni haki yao ya msingi, jeshi la polisi limtafutie chumba cha kumhifadhi ili aunganishwe na watuhumiwa wengine.

Alisema jeshi la polisi linatengeneza mashujaa wa ukombozi wa pili wa Tanzania, kama ambavyo jeshi la polisi la kikoloni lilivyotengeneza mashujaa wa ukombozi wa Tanganyika kwa  kuwakamata na kuwafungulia mashitaka ya kutunga viongozi wa  TANU, kama vile marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

“Kama mtakumbuka baada ya msukosuko wote, hao ndiyo waliokuja kuwa viongozi waandamizi wa  Tanganyika huru na ndivyo  tunavyoona mambo ya leo ya CCM ya kuwakamata na kuwashitaki wanaharakati wa CHADEMA.

Alisema kukamatwa kwa viongozi hao hakutaathiri mwenendo wa kampeni ya nafasi ya CHADEMA kuibuka na ushindi.

Katika hatua nyingine wabunge hao,Bw. Kasulumbayi,Bi. Kiwanga pamoja na kada wa chama hicho, Bw. Anuary Kashaga wanatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mkoa wa Tabora kujibu mashitaka yanayowakabili.


Wakati huo huo mgombea ubunge kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Igunga, Bw. Leopold Mahona, amelaani kitendo cha viongozi na wafuasi wa  CHADEMA kumtwanga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi.Fatuma Kimario.

Akihotubia  mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Ziba jana, Bw. Mahona alisema kitendo hicho kimemdhalilisha kiongozi huyo wa serikali kutokana na kupigwa hadharani.

"Kitendo cha kumpiga DC ni utovu wa nidhamu, ni kiongozi wetu wa serikali... yule ni sawa na mama yangu, kwanini umpige wakati sheria zipo,nalaani kitendo cha kumpiga DC" alisema, Bw. Mahona.

Alisema kuna watu wamedhamiria kuleta fujo katika jimbo la Igunga hao ni wageni kwa sababu mila na desturi za wenyeji wa jimbo hilo hawana
tabia ya kupigana kwa ajili ya siasa.

Bw. Mahona alisema matukio ya kumwagiwa tindikali kwa kijana anayedaiwa ni mfuasi wa CCM na kitendo cha kukatwa mapanga kwa mkazi mwingine wa jimbo hilo hayakuwepo kabla ya kampeni.

Aliwataka wananchi wasikipigie kura chama ambacho kitawaletea madhara badala yake wachague mgombea wa CUF ambaye ana sera za amani na utulivu kwa
Watanzania.

 

25 comments:

  1. Tundu Lissu ni mtu kunaekuamini na kukutegemea umebobea ktk sheria,lakini kwa kauli zako hapa kidogo nina wasiwasi unapotoka!!kuwa Mkuu wa wilaya alikataa kutii amri halali ya kujisalimisha ina maana wafuasi wa chadema wana mamlaka ya kumpa Amri HALALI ya kujisalimisha Mkuu wa Wilaya?Fanyeni kampeni kwa amani na kiungwana sidhani hizi fujo na chuki mnazozipandikiza zitaleta manufaa kwenu na kwa wana IGUNGA taratibu zipo mngeweza kuzifata lakini hapa mnaonyesha kujichukulia sheria mikononi mwenu sio sahihi.

    ReplyDelete
  2. Msiwe mnawaona viongozi wenu kama miungu watu kiasi kwamba hata wakitenda kosa hawastahili kuchukuliwa hatua. Nafikiri vile vile nafikiri wananchi wengi hamjui maana ya polisi jamii ndio maana mnapoambiwa mkuu wa wilaya alikataa kutii amri halali hamuelewi.

    ReplyDelete
  3. Tumepatwa na Mstuko mkubwa sisi watu na wenyeji wa Igunga. Kwakweli hawa Chadema Toka wamefika Igunga ni vurugu tupu. Isitoshe wote hawa wanaofanya vurugu hizi ni Wageni kwakuwa Sisi wenyewe tunafahamiana na isitoshe hwa Chadema kwa hapa Igunga kiukweli ni wachache kupita maelezo na kwa utamaduni wetu Chadema Igunga ni watulivu kupita maelezo kwakuwa wengi wao tupo nao siku zote na hawana matatizo.Sasa hawa wageni wamekuwa kama wenyeji na wanatuletea Utamaduni Tusiokuwa nao wanatushangaza sana. na kwanini wawe wao tu? Wanapandikizwa chuki na Viongozi wao ambao wanaonekana wanasiasa za Chuki na Jazba. Tukio hili la kudhalilishwa Mkuu wetu wa Wilaya kwa hili Chadema lazima wakubali wamepotoka na kamakweli Katibu Mkuu aliwatuma Vijana wake wakiwamo hao wabunge basi ipo namna. Tutaomba Igunga isafishwe kwa kumchukulia hatua pia huyu Katibu Mkuu. Tunachohitaji ni Amani na Utulivu tuliokuwa nao Upendo na Udugu tuliokuwa tukiishi bila tofauti za Kisiasa, Leo ukweli Baada ya Uchaguzi kuna Tofauti na Watakao umia na kupata Madhara ni hao wachache wa Chadema. Tunaomba na Tunamuomba Mungu lisitokee tena kubwa zaidi la hili na Uchaguzi Uishe kwa Amani.

    ReplyDelete
  4. Watanzania wa leo wameamka jamani. Kama Mkuu wa Wilaya alikuwa anaongoza kikao haramu na pale mahali hakuna Polisi ni sawa kabisa wananchi wana uhuru wa kumkamata ili liwe fundisho kwa viongozi wengine. Siku zote tunaambiwa kuwa kiongozi wa serikali, polisi, hawaruhusiwi kujihusisha na ushabiki wa vyama vya siasa. Sasa huyu mama kihere here gani kilimpata kufanya kikao sehemu hiyo hiyo ambayo CHADEMA walikuwa na mkutano wao halali wa kampeni? Huyu mama ni mlinda usalama au mvunjifu wa amani? Kama sheria haziruhusu kwa nini alifanya hivyo. Hawa viongozi waliopewa dhamana jamani wasichokoze wananchi kwa sababu huu ni uchokozi wa wazi kabisa. Kwa sababu ni mwanamke ndio avunje sheria kwa kujitetea kuwa amedhalilishwa kijinsi? Wanawake wamedai haki sawa kwa hiyo wajaribu kujiheshimu ili nao waheshimiwe.

    ReplyDelete
  5. Hivi mwizi akikuvamia kwako, ukamwambie ajisalimishe akakataa utafanya nyinyi? Common sense inaniambia nitatumia nguvu kumdhibiti.

    Huyo DC alikuwa mwizi aliyevamia mkutano wa CHADEMA, na baada ya kukataa amri ya kujisalimisha ilibidi nguvu ya umma itumike kumdhibiti.

    Mbona siku aliyokamatwa yeye mwenyewe alikiri kwamba amefanya makosa? Hii ya kubadilisha maelezo mbona imekuja baadaye (Hopeful baada ya kuwa trained)

    Kitu kimoja ambacho inabidi waTZ tutambue hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria.

    Afterall hawa DCs na RCs ni mzigo kwa walipa kodi dawa yake ni katiba mpya.

    ReplyDelete
  6. Mwizi wa kuvamia mkutano!! Wapi na wapi yeye alikuwa yuko ndani na ktk kikao na watendaji wake,Chadema wakamvamia baada ya kupata uvumi kuwa ana ajenda ya kuwahujumu hakuwepo ktk mkutano wa chadema na pia umbali wa alipokuwa ktk kikao na mkutano wa chadema ni mita 400 huu ni utovu wa adabu maana usipo muheshimu mlezi wa mwenzio basi ujuwe iko siku na wako atavunjiwa heshima,isije ikawa mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu tuwe wastaarabu na wavumilivu na watulivu tusiwe na papara.Msihukumu bila kujuwa uhalisia wa habari.Fatilieni vizuri sio kuwa kavamia au alikuwa ktk mkutano wa CDM.
    Sio kupenda ni kupotosha chongo ukaita kengeza

    ReplyDelete
  7. wanaigunga wakati wa kuwa na akili ni sasa pimeni muone wenyewe kipi ni pumba na lipi ni mchele chagueni mtu sahihi kwa maendeleo yenu! lakini tambueni kuwa kabla ya maendeleo amani na usalama kwanza hutangulia!wanyamwezi na wasukuma ni watu wastaarabu sana kwa hiyo chungeni sana hila za wasiowatakia mema bali maslahi yao binafsi!

    ReplyDelete
  8. ccm ni chama dola lakini siku ipo tu.

    ReplyDelete
  9. viongozi c miungu mtu akome kata mwizi meeeeeeeeeeeen

    ReplyDelete
  10. Eti kadhalilishwa kwa kuwekwa tumbo wazi? Huyu shangingi kajidhalilisha mwenyewe kwa kujifanya mungujike. Akumbuke katika mashitaka feki aliyoyafungua hakuna atakaye nyongwa!Ole wenu ccm muwafunge hao wabunge wa CHADEMA miaka mingi kuliko yule mwizi wa B.o.T

    ReplyDelete
  11. Mh.Fatuma Dc wa Igunga ww ni Mchokozi kilichokufanya uende kwenye Mkutano wa Chadema ni kitu gani?Ninaomba uwe mstaarabu na muungwana.

    ReplyDelete
  12. ccm arrogance at the highest!

    ReplyDelete
  13. Hawa Ma DC sio ndiyo "chakula" cha akina Mwigulu Nchemba and Co.

    Wewe Fatuma and Co. mlisha jidhalilisha wenyewe tangia zamani msisingizie CDM!

    ReplyDelete
  14. Siku si nyingi zinakuja CCM itakuwa katika historia ya chama kilichowahi kutawala.Vijana ndio nguvu ya umma popote duniani,siku watakapochoka zaidi na mbinu halali zikashindikana basi kifuatacho mbinu haramu zitatumika.Ni rahisi kuona nachochea fujo lakini ukweli ndio uliopo;amani bila utawala wa sheria ni fujo!

    ReplyDelete
  15. Hamna akili kabisa , yani mnazidi kun.gangania DC alivamia mkutano wa CHADEMA , mmeshapewa ufafanuzi hamsikii hamuelewi . huu ni upofu wa kipuuzi na ambao hauwezi kuwasaidia wanachadema. mara kadhaa mmeelezwa Chandimu walipaswa kufanya mkutano wao saa 4-6. badala yake wakafanya saa tisa . pia DC alikuwa anafanya mkutano wake ndani na haukuwa mkutanom wa hadhara lakinibado mnadai ulikuwa mkutano wa hadhara .

    Tatizo mnadhani watu hawaelewi kama ninyi , hakika Igunga itakula kwqenu hamtapata kitu .

    ReplyDelete
  16. Wanachadema ni wapishi na hawataki kuelewa hata kama ukweli wanauona. Wao kazi yao ni kupinga, LAKINI kwa hili mmejipalia mkaa. Hapa Igunga tumeamua hatuwapi kura zetu. Nyie mnaoshabikia CHADEMA kwa njia ya magazeti anzeni kufikiria ya kuandika baada ya uchaguzi kwani meshashindwa. CHADEMA ana fujo, ana jazba, uchu wa madaraka, HAWANA HOJA. Nendeni huko Arusha na sio Igunga. Huu utamaduni wa fujo kwetu hatuna. CHADEMA IGUNGA KWA HERI.

    ReplyDelete
  17. Mchezo huo ni mchafu, sheria ziko wazi, vipi DC unasubiri kampeni zianze ndiyo wewe uanze kazi tena kwenye eneo la kampeni, jamani hebu muache haya mambo mnatuharibia nchi

    ReplyDelete
  18. dc ni raia kama raia wengine. kama sheria inasema asifanye hiki basi asifanye la sivyo kupigwa atapigwa tu. mbona sisi wananchi tunakamtwa na kupigwa na polisi bila makosa hatusemi na wao wanaangalia tu? wacha nao waonje joto ya jiwe ili wajifunze. hata kikwete akienda tofauti piga sanaaaaaaa. tunahitaji viongozi wastaarabu bwana.

    ReplyDelete
  19. eng. Mwakapango, E.P.ASeptember 20, 2011 at 9:33 AM

    Nafikiri Polisi huwa wanapopopata matukio ya namna hii wanachukua hatua bila kupima madhara ya yatakayotokea ikiwa ni pamoja na hatua za kimahakama zitakazo chukuliwa. hatufuruhii sana hatua zilizochukuliwa na CHADEMA lakini lazima ifikie mahali watu waheshimu taratibu na sheria tulizojiwekea ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali kutojiingiza kwenye kampeni kwa kutunia rasilimali za serikali ikiwemo magari ya serikali. nimekuwa nikijiuliza kiongozi wa serikali ni nani na wa chama ni yupi hasa inapofikia uteuzi. viongozi tunajua ni binaadam wa kawaida hivyo hauwezi kuondoa mapenzi na ushabiki kwa chama anachokipenda. lakini ukishateuliwa serikalini shiriki katika vikao vya kimkakati tu. Rais aliyekuteua amepewa mamlaka na wananchi ambao ni watanzania wote hebu jaribu kupiga mahesabu ni wanachama wangapi wa CCM na ni watu wangapi waliomchagua Rais? Unapofanya shughuli za chama ukiwa kiongozi wa serikali huoni kuwa unawakwaza wanachi wengine walioshiriki kuichagua serikali iliyopo madarakani? mimi nampenda Dr. Jakaya Mlisho Kikwete anajua ku practice politics viongozi wengine wamwige waziri mkuu upo? POLISI leo nchi iko mikononi wa CCM siku CHADEMA ikishika nchi mtakimbilia wapi? hatutaki ya ujerumani yatokee tuje tuwashuhudie wakina said mwena, Advocate, Baro waje wafikishwe mahakamani wakiwa vikongwe kama ilivyotokea kwa walioshiriki kambi ya mateso Sorbibor. Hatutaki kuja kushuhudia makaburi ya wakuu hawa wa polisi yakiwekewa alama za ajabu ajabu.
    sote tu watanzania tufikiri tunako kwenda tunataka maendeleo tu ukiangalia input ya wabunge hivi unaweza kusema nani CCM, CUF na CHADEMA? Tuache ushabiki wa kisiasa tujenge nchi hii nchi ni yetu sote sio ya ya kina January, wasira na nchemba na mkuchika pekee yao!

    ReplyDelete
  20. HIVI NYIE WANACDM MNATOA MAONI POTOFU MMETUULIZA SISI WANA IGUNGA TULIOKUWEPO HAPA NA KUONA JINSI MAMBO YALIVYOKUWA? AU MRADI TU MUWAKOROGE WATU WAWE KAMA MNAVYOTAKA? HUYO DC ALIKUWA KTK KIKAO NA WATENDAJI WAKE NDANI SIO KTK UWANJA WA MKUTANO PILI NI UMBALI WA MITA 400 TOKA WALIPOTAKIWA CDM WAFANYE MKUTANO WAO TENA KIKAO CHA DC KILIKUWA MCHANA SAA 8 HAO CDM WALITAKIWA WAFANYE MKUTANO WAO SAA 4-6 HV HAPA NANI MKOSA? NINI KOSA LA DC NYIE NI WATOVU WA ADABU HAMNA SERA,SERA ZENU NI FUJO ILI MUPATE SABABU MKISHINDWA MAANA HAPA TISHIO KIDOOOGO NI CUF LAKINI CDM NI WASINDIKIZAJI!! ACHENI KUWAPOTOSHA WATU LAKINI SI AJABU KIPOFU AKIMUONGOZA KIPOFU MWENZIE TEGEMEO NININI?

    ReplyDelete
  21. KAULI ZA HUYO DC KWENYE VYOMBO VYA HABARIBAADA YA KUKUTWA NA WANANCHI NA ZILE ALIZOTOA ALOPOKUWA CHINI YA ULINZI HALALI WA WANANCHI ZINATOFAUTIANA, ANABABAISHA NA ANAONEKANA SI MKWELI, NA NI MNAFIKI SANA. AMEKUTWA KATIKA MAZINGIRA YA UTATA NA ALIBABAIKA NA KUTOJIAMINI KAMA MKUU WA WILAYA ALIONEKANA TU ALIKUWA ANAFANYA KITU HARAMU KINYME NA UTARATIBU. HATA KAMA POLISI NA VYOMBO VYA SHERIA VITAMLINDA KAMA ILIVYOKAWAIDA YA SERIKALI YA CCM, KWETU SISI WANACHI TULIO WENGI TUNAONA CHADEMA WANAHAKI NA HAWAKUPASWA KUSHTAKIWA KABISA. TUPO NYUMA YA CHADEMA NA WANANCHI WEWNGI TUNAWAUNGA MKOO. PIGANIENI HAKI SIKU MMOJA TUUTAFANIKIWA KUUONDOA UKOLONO HUU WA WATU WEUSI WANAFKI NA WABAYA HATA KULIKO UKOLONI WA WAZUNGU. NI HERI TUNGEENDELEA KUTAWALIWA NA WAZUNGU KULIKO WAAFRIKA WENZETU WALIOTUGEUKA BAADA YA KIFO VHA BABA WA TAIFA. KAMA ANGEFUFUKA SASA HIVI HAKIKA ANGEJIOMDOA CCM NA KUREJESHA KADI KAMA ALIVYOWAHI KUJARIBU KUFANYA HAPO AWALI. CCH NI WAKOLONI WABAYA NA WANYONYAJI WALIOKUBUHU NDIYO MAANA WANAKUMBATIA MASISADI NA HWATAKI KUWASHITAKI, MWALIMU HAKUKUMBATIA MAFISADI KAM ROSTAM AZIZI, LOWASA, KAGODA N.K. ASINGEKAA NAO HATA MEZA MOJA. WATANZANIA MUAMKE, MTALALA NA KUDANGANYWA HATA LINI. WAKUU WA WILAYA WAMEAMBIWA CCM IKIPOTEZA MAJIMBO YA UCHAGUZI NA WAO HAWANA KAZI. HIVYO WANAFANYA MBINU CHAFU NA VIKAO BATILI ILI KUINUFAISHA CCM- CHAMA AMBACHO SASA KIMEOOZA TANGU MWALIMU ATUTOKE. HAKIFAI.

    ReplyDelete
  22. Tundu Lissu wewe ni mwanasheria uliobebea. Tunakutegemea sana. Ila hapa Igunga ndugu yangu unaongea kisiasa. Kifupi UMECHEMSHA

    ReplyDelete
  23. ni bahati nzuri alivaa hijabu na wakaona waivue hiyo, asingekuwa na hijabu wangemvua nguo gani? ustaarabu wa ki- tanzania umepotelea wapi? hii ndio sayanso na teknolojia? tundulisu, ulizaliwa kwenye tumbo la mwanamke kama tulivyozaliwa wengine? ingekuwa na lipi la kusema kama mama yako alikuzaa angevuliwa nguo, hifadhi ya mwili wake hadharani? naanza kuhisi inawezekana viongozi wengi wa CHADEMA si wa- tanzania na kama ni wa- tanzania basi ni wahuni msiofaa kupewa madaraka

    ReplyDelete
  24. Sio chadema wala ccm ninasikitishwa na kitendo cha kuzalilishwa mama mtu mzima bila kujali cheo chake hivi watanzania tunaelekea wapi? kwa kifupi katibu wa chadema haukutumia busara kuwaagiza vijana wako kufanya uupuzi kama huo tena na wabunge wakiwa kati ya hao wapuuzi, kwel nchi hii inaelekea pabaya, mi naamini ka kutumia sera zenu mngefika mbali, lakini kwa stahili hiyo hata mimi nimekuwa na mashak na nyie, tunduliso mwana sheria kuaminika leo nimegundua kuwa wewe ni mpuuzi kwa kushindwa kufuta sheria unayoitambua na kufanya sisa ya ushabiki, maoni kwa chadema bado mnanafasi kama mtabadilika lasivyo mtakuwa mnapoteza ubora wenu kila kukicha kutokana na skendo MUNGU ibalikia Tanzania zenu

    ReplyDelete
  25. Mwl. Kalolo, C. E. Mwendisule!September 23, 2011 at 11:01 AM

    watu bado hawajajua dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi, ndio maana wamekomalia kuwalaumu chadema kuwa walipotoka. lakini huyu mama kama alikuwa akifanya uhalifu na askari hawakuwepo eneo la tukio nani alipaswa kudhibiti uhalifu huo? tanzania ni nchi inayoongozwa na utawala wa sheria, hakuna mtu aliye juu ya sheria. hata rais hayuko juu ya sheria, itakuwa huyo mkuu wa wilaya?
    watu wameshasahau fujo zilizofanywa na CUF pale Igunga walipokuwa wakizuia msafara wa chadema na waandishi wa habari wenye mrengo wa CCM hawakuikomalia kwa kuwa tu CUF ni CCM B. leo la mkuu wa wilaya kwa kuwa linaonekana kuinufaisha CCM imekuwa mjadala kila kukicha
    naomba tubadilike na tuilewe vema dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi

    ReplyDelete