Na Anneth Kagenda
WATU zaidi ya 10 wanaofiwa kufa na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Njombe kwenda Dar es Salaam kupata ajali na kupinduka
katika eneo la Mwidu mpakani mwa Mji wa Morogoro na Pwani.
Ajali hiyo ilihusisha basi lenye namba T 559 ABK ambalo ni mali ya kampuni ya Glazzia.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, zilieleza kuwa juhudi za kuokoa watu walionusurika na kutoa miili ya marehemu walionaswa kwenye vyuma vya basi zilikuwa zikisuasua kutokana na uhaba wa vifaa.
"Sisi tumepita tumeshuhudia basi likiwa limepinduka, askari na trafiki wapo lakini hakuna kilichokuwa kikifanyika kutokana na uhaba wa vifaa," alisema mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.
Shuhuda mwingine wa tukio hilo alisema kuwa basi hilo lilikuwa limepinduka matairi yakiwa juu huku watu wakiwa wamebanwa kwenye vyuma bila msaada wowote.
Alisema kuwa pamoja na kwamba trafiki na polisi walimiminika katika eneo la tukio lakini hakukuwa na msaada wowote wa haraka uliotolewa.
Ajali zimekuwa zikiendelea kutokea katika maeneo mbalimbali na kuua watu wengi ikilinganishwa na ile iliyotokea hivi karibuni katika kisiwa cha Nungwi Zanzibar na kuua mamia ya raia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia ajali hizo na hbari zilizopatikana zilieleza alikuwa kwenye eneo la tukio huku ambako polisi walikuwa wakijaribu kuokoa majeruhi.
Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu,ajali haina mjanja na kila mtu anapenda kuishi;inawezekana kuna uzembe lakini haiwezekani kukawa na mukusudi ya kuandaa ajali
ReplyDeleteBadala ya kuchukua hatua bila shaka tutasikia Rais Kikwete ametuma rambirambi. What a president. Haya Mheshimiwa tunasubiri utume au tayari?
ReplyDelete