11 August 2011

Wauzaji mafuta wasalimu amri

Wasambaza lita milioni tano jana
Wananchi walazimisha vituo kuuza

Na Wandishi Wetu

Mafuta yaliyosambazwa zilizosambazwa

Petroli 1,821,600.00   
Dizeli 3,309,500.00   
Mafuta ya taa 270,500.00   
Jumla 5,401,600.0





Awali, gazeti hili lilishuhudia msongamano mkubwa wa gari, pikipiki, bajaj na idadi kubwa ya watu wenye vidumu kwenye vituo vya mafuta vilivyokuwa vikitoa huduma na kusababisha baadhi ya barabara kufunga na kulazimika Askari wa Usalama Barabarani kuingilia kati.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya vijana hasa walianzisha biashara ya kununua mafuta kwenye vidumu vya lita tano kwa bei elekezi ya EWURA na kuwauzia kwa bei ya kuruka wenye magari, pikipiki na bajaj waliokuwa wameishiwa na vyombo vyao kuzimika barabarani.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na majira kuhusu sakata hilo walisema kuwa limeathiri uchumi wa nchi pamoja na uzalishaji viwandani na hata katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano, kwa kuwa mafuta hayo ndio yanayochangia kuzalisha umeme sehemu za kazi, hasa kipindi hiki chenye mgawo wa nishati hiyo.

Dereva teksi mkazi wa Mwenge, Bw. Jeremiah Joseph alisema kuwa serikali imekosa nguvu ya kufanya maamuzi na imeshindwa kuongoza badala yake wafanyabiashara ndio wenye nguvu ya kuamua.

Hata hivyo, asiliamia kubwa ya waliozungumza juu ya suala la mafuta waliita serikali kama imeshindwa kuchukua maamuzi magumu wa kutatua tatizo hilo kuweka wazi, huku wakitishia kuingia barabarani kwa maandamano ikiwa tatizo hilo litaenedele kwa wiki hii yote.

Katika kituo cha Oilcom, Tabata Relini kundi la watu lilivamia kituo hicho wakiwa na vidumu na kulazimisha watumishi hao kuwauzia mafuta, walipoelezwa kuwa hawakuwa nayo walilazimisha matanki yafunguliwe wathibitishe.

Watu wlaioshuhudia tukio hilo, walisema baada ya kufungua matanki hayo, ilibainika kuwa petroli ilikuwa imekwisha na dezeli ilikuwa nado ipo ndipo ilipowalazimu polisi waliofika hapo kusimamia kuuzwa kwa mafuta yaliyokuwapo, huku umati huo ukitamba baada ya hapo wangekwenda katika vituo vingine vya karibu kuhakikisha mafuta yaliyopo yanauzwa.

Kuchelewa kutoa kauli

Mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Bw. Mizengi Pinda alizungumzia sababu za serikali kushindwa kutoa kauli mapema hadi ilipobanwa na wabunge:

“Kila mtu alikuwa anatafsri hoja hii vibaya, lakini sheria inaeleza wazi kwamba mara baada ya kuidhinishwa kwa chombo huru ambacho kinasimamia shughuli hizo yaani, EWURA wao ndiyo wenye mamlaka ya kutoa maamuzi ya mwisho kama wanaona mtoa huduma anakaidi agizo.

"Na kama watatoa ‘compliance order’ (Amri ya kutaka watoe huduma) ndani ya masaa 24 wahusika ambao ni vituo vya mafuta wakishindwa kutoa maelezo, adhabu kubwa ni kufutiwa leseni tu, wala hapa hapahitajiki maelezo kutoka kwa waziri mkuu kwa sababu sheria zipo wazi,” alifafanua Bw. Pinda.






No comments:

Post a Comment