19 August 2011

Serikali yashtuka kutoka usingizini

*Maige amsimamisha mkurugenzi wanyamapori
*Msekwa ajibu tuhuma za ufisadi Ngorongoro
*Mgawo wa umeme walalamikiwa upya bungeni

Na Waandishi Wetu

SAKATA la kutorosha wanyamapori kwenda nje ya nchi limeishtua serikali kutoka usingizini baada ya Mkurugenzi wa
Idara ya Wanyamapori Bw. Obeid Mbwangwa na watendaji wengine wawili kusimamishwa kazi na serikali ili kupisha uchunguzi.

Bw. Mbwangwa amekumbwa na hali hiyo zikiwa ni siku chache baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, na siku moja baada ya wabunge kutaka hatua zichukuliwe haraka kwa wahusika, akiwamo mkurugenzi huyo na wanyama walioibwa warejeshwe ama wakiwa hai au wamekufa.

Kutokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mkurugenzi wa awali, Bw. Erasmus Tarimo Februari 8, mwaka huu na kumpatia likizo ya kusubiria kustaafu ambapo kwa mujibu wa sheria Julai 7, mwaka huu ndipo Bw. Mbwangwa alishika wadhifa huo kutoka nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa wizara hiyo.

Tamko la kusimamishwa kazi kwa Bw. Mbwangwa na wenzake wawili ambao hawakutajwa majina ili kupisha uchunguzi, lilitolewa jana bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige wakati akifanya majumuisho ya makadirio na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011 na 2012.

"Mheshimiwa Spika kutokana na malalamiko mengi ambayo waheshimiwa wamelizungumzia ni suala la kutoroshwa kwa wanyamapori, ninashukuru sana na maoni ya kamati juu ya suala hili ni nimeyazingatia," alisema Bw. Maige

"Hivyo basi kuanzia leo Agosti 18, 2011 Mkurugenzi wa Maliasili na Utalii, Obeid Mbwangwa na wenzake wawili ambao kutokana na uchunguzi wa jambo hili sitawataja hapa, nimewasimamisha kazi rasmi, ili kupisha uchunguzi wa utoroshaji wa wanyamapori hao," aliongeza.

Kilio cha wabunge

Wabunge jana waliendelea kuchangoa bajeti hiyo, wakiitaka serikali kuwarudisha wanyama 116 waliotoroshwa, wawe hai au mizoga kwa kuwa na kama itashindwa kufanya hivyo itakuwa imeonesha udhaifu mkubwa.

Walisema kwa kitendo hicho, serikali imeingia doa ambalo ni tishio kwa usalama wa taifa kwa kuruhusu ndege ya kijeshi ya Qatar kuingia nchini na kuruhusiwa kukaa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa  kuwapakia wanyama hao na kuwasafirisha.

Mbunge wa Simanjiro, Bw. Christopher Ole Sendeka (CCM) alisema utoroshwaji wa wanyama hao ulifanyika kwa sababu viongozi wengi wamezoea njia za kufanya mambo kwa mkato.

Mbunge huyo alisema nyara za taifa zinaporwa kwa kiasi cha kufedhehesha, hivyo leseni 180 za uuzaji wanyama nje zifutwe na zichomwe moto kuanzia jana.

“Mkurugenzi wa Wanyamapori Bw. Mbangwa hawezi kukanusha kuhusika katika utoroshwaji wa wanyama hai na ndege hai kwa kutumia ndege ya jeshi la Qatar kutoka Uwanja wa Ndege KIA, kuna matatizo katika idara hiyo likiwemo suala la ukabila, hivyo waziri ana kazi ngumu kuibadilisha idara hiyo,” alisema Bw. Sendeka.

Alisema kama Bw. Maige anataka kuwafahamu ama kupata ukweli kuhusu wanyama na ndege waliotoroshwa, aandike barua Geneva Uswisi na waliohusika wataumbuka na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Tupo tayari kuwapokea wanyamapori wetu wakiwa hai au mizoga, Mheshimiwa Spika bila kusita wanyama wote waliotoroshwa hapa nchini tunahitaji warejeshwe mara moja, hiki ni kibarua kizito kwa kuwa ilichangiwa na tabia mbaya serikalini, lakini lazima iwe hivyo,” alisema Bw. Sendeka.

“Ni mbaya sana kuona ndege ya jeshi la Qatar inaingia hapa nchini katika uwanja wa ndege wa KIA bila kibali na kufanya kazi yake kisha kuondoka na wanyamapori wetu wakati nchi zingine haiwezekani ndege ya kijeshi kutua na kufanya hivyo, hali ya usalama wa nchi iko hatarini,” alisema Bw. Sendeka.

Aidha mbunge wa Maswa Magharibi Bw. John Shibuda (CHADEMA) akichangia katika hotuba hiyo alisema utoroshaji wa wanyama hao ni doa kwa taifa hivyo haoni sababu ya kumsifia kiongozi yeyote kwa kuwa wanaipeleka nchi katika hali mbaya kiusalama.

“Kutoroshwa kwa wanyamapori hao kumeidhalilisha Idara ya Usalama wa Taifa, Polisi, na mamlaka nyingine za usalama na hawa wanaoitwa intelijensia taarifa zao zilikuwa wapi tangu wanyama hao walipokuwa wanakusanywa,” alisema Bw. Sibuda.

Aidha Mbunge wa Kilindi Bi. Beatrice Shelukindo (CCM) alisema matatizo yote ya kuuza wanyamapori yanatokana na viongozi wasio waadilifu.

“Mheshimiwa spika Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori hastahili kuwepo kwenye nafasi hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyetoa vibali 180 kwa wafanyabiashara kuuza wanyamapori nje ya nchi.

Serikali yasitisha vibali

Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda jana katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo aliwaeleza wabunge kuwa serikali imesitisha vibali vya usafirishaji na uuzaji wanyama nje ya nchi kwa kuwa biashara hiyo haina manufaa kwa taifa.

Bw. Pinda alisema biashara hiyo itatazamwa upya, na itakapoanza masharti yatabadilika ikiwa ni pamoja na kiwango cha tozo kwa kuwa wafanyabiashara wanapata faida kubwa kuliko serikali

Msekwa akanusha tuhuma dhidi yake

Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Pius Msekwa amepuuza vikali tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wabunge na kusema kuwa ni maneno ya 'kijinga na kipumbavu'.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Dodoma jana, Bw. Msekwa alisema kwamba yupo kwenye ziara ya kikazi na madai yanayotolewa juu yake kwamba anatumia vibaya nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi ya Ngorongoro kugawa maeneo kwa wafanyabiashara ni ya kipuuzi.

"Ndugu mwandishi nisikilize vizuri, madai hayo ni ya kipuuzi lakini nitaitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia ukweli wa jambo hilo," alisema Bw. Msekwa.

Umeme walalamikiwa upya

Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda ameitaka serikali itoe maelezo kuhusu kukosekana kwa umeme usiku na mchana katika maeneo mbalimbali kwa siku kadhaa licha ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kupitishwa wakati ikionesha matumaini makubwa.

Bi. Makinda alitoa agizo hilo jana bungeni mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Nyamagana, Bw. Ezekiah Wenje (CHADEMA) kuomba mwongozo wa spika, ili bunge lijadili jambo la dharura kwa kutumia kanuni ya 87(1).

Wakati anaomba mwongozo huo Bw. Wenje alilieleza Bunge kuwa, hakuna umeme Mwanza kwa siku nne sasa usiku na mchana, na pia tatizo hilo lipo kwenye maeneo mengi nchini ukiwemo mkoa wa Arusha, Kigoma na Dar es Salaam.

Imeandikwa na Godfrey Ismaely, Rachel Balama, Dar na Pendo Mtibuche, Dodoma



14 comments:

  1. Haiwezekan wanyama pori waibwe wazir husika,Polisi,Maafisa wanyama pori,Jeshi na Raisi wasijue.KUWASIMAMISHA KAZ MAAFISA WANYAMA PORI NI KIINI MACHO TU.

    ReplyDelete
  2. Kama kweli Wizara haikujua kutoroshwa kwa wanyama hao hadi pale iliposhtuliwa Wabunge, basi lazima kuna tatizo kubwa katika wizara husika na serikali kwa ujumla. Kama haikushiriki kitendo hicho, basi ilizembea. Iwe ilizembea au la, wizara nzima inapaswa kujiuzulu na siyo maofisa wachache tu wa wanyamapori. Kuwasimamisha maofisa hao ni kuwatoa kafara ili wengine wanaostahili kufukuzwa kazi wapone.

    ReplyDelete
  3. Nyie majira mbona hamjaandika habari ya Shibuda,kampeni zenu hazisaidii. Shibuda toka kwa wachaga hao watakuua. hivyo vyama vimezoea ndio MZEE.watakuchukia kwa ukweli wako daima.Tayari majibwa ya wachaga watajaza gazeti kwa kuwatetea mabwana zao. Shibuda toka hiyo chama hao wachaga ni mafia na usipokubali ya Mbowe,Ndesa,Mtei na promoter wao Slaa watakuua hao. Anzisheni chama huko usukumani siku moja wachaga watakuwa wabunge huko. hii midog imekodiwa,mtu mwenye msimamo kama wewe hukubaliki,hivi vyama vimezoea ndio mzee

    ReplyDelete
  4. KAMA HUYU SHIBUDA WAKO ANAMSIMAMO, KWANINI CCM ILIMTEMA KATIKA URA YA MAONI. ACHA UJI.NGA WAKO WEWE. WEWE NI MKE WA MAFISADI TUU, ENDELEA KUWAUZIA BUTI YAKO MAMA. CHADEMA NI CHAMA CHA UHAKIKA. NI MAANDAMANO MPAKA HILO JOKA LENYE MAGAMBA YA KENGE LING'OKE HUKO IKULU. IKULU SIO SEHEMU YA KUTEMBEZA UHU.NI WENU HAPO.

    ReplyDelete
  5. CHADEMA ni chanma cha wachaga na ndugu au ukoo watu kama wewe hauko katika makundi hayo lazima ung'olewe tu,fanyeni utafiti wa kina .Tundu Lisu ana watu wake, Ndesamburo anafamilia yake, Mbowe na familia yake , tumieni vichwa vyenu kufuatilia zuga ya chama hiki.

    ReplyDelete
  6. naweza kukubaliana na wachangiaji (CDM NI KLM TYPE)maana ngazi za maamuzi zote ni barabara moja na hata wanadai nyerere aliwabania sasa ni zamu yao.hata siwatambui kama wapinzani maana ni fujo tuuu.

    ReplyDelete
  7. KWANI KAMATI KUU CDM WAMESEMA NINI KUHUSU MH SHIBUDA.WENGI SASA TUNAAMINI CDM NI CHAMA MAKINI NA WENGI HAWAKUZOEA HILO HATA MHE SHIBUDA ANAELEWA HILO, CDM MSIBABAISHWE NA HAYA MAMBO YA UDIN,UCHAGA NK.NI CHUKI ZA WENYE HASIRA NA HOFU YA MAFANIKIO YENU.HIVI SASA MNAONGOZA SERIKALI BILA SERIKALI ILIYO MADARAKANI BILA KUJUA, KWA SABABU VILIO VYA WANANCHI KUPITIA WABUNGE WENU NA MAANDAMANO YENU SASA NDO DIRA YA CCM NA SERIKALI YAKE SI VIBAYA KWA SABABU WATU TUNATAKA MAENDELEO..WTZ TUWAUNGE MKONO CHADEMA

    ReplyDelete
  8. sielewi kama dege lajeshi kutoka nje laweza kutua Nchini lada isionne lazima wahusika walijua kinacho endelea,hii tabia ni ya kurithi.Hata wakati wa ujamaa Nchini Matajiri walikuwepo licha ya Azimio la Arusha kuwepo na Nyerere akiwepo.

    ReplyDelete
  9. inasikitisha sana kuona watu wakikijadili chama kwa mtazamo wa udini, ukabila au ukanda!!!! wat fool CCM is???? Tunachukuliwa wanyama kwa dege la kijeshi, eti Maige na serikali ya kaka yake Kikwete hawakujua????? fool!!!!! wametuona sisi wajinga ati. Hiyo ndege ilipitia chini ya ardhi au ile rada ya chenge imeshakufa kiasi cha kutoiona ikiingia.
    Ningekuwa mungu watu hawa ningewachoma hapahapa duniani. Ila kiacha cha CCM na wajinga wote nadani ya chama hicho ni 2015 tutawachapa au kama vipi tutaandamana mpaka Kikwete aikimbie ikulu. Wanatuchezea, hata mwinyi alikuwa anasafirisha wanyama vivyo hivyo data zipo. Mfalme wa Saudi akija zawadi zake pundamilia 50 hivi hii serikali ni ya wajinga kiasi gani??? kama mnawapenda sana hao waarabu wapeni wake zenu na sio maliasili zetu.

    CHADEMA HOYEEEEEEEE sio hicho chama cha magamba, huku kwetu ukikosea unaadhibiwa sawa na makosa yako sio huko CCM ambako unaangalia nani aadhibiwe na nani aachwe!!!!

    ReplyDelete
  10. NAONA WANANCHI WANAOCHANGIA KUHUSU VYAMA KWA KUWEKA UKABILA , UDINI N.K WAMEISHIWA SERA . TANZANIA HAKUNA CHAMA KAMA CHADEMA KWA UBORA . WANAOSIFIA CCM WANASUBIRI KUNYONYWA TU TAFAKARI KWANZA . YAELEKEA MWENDO HUU WA SERIKALI HAMJAONA NI WA KURUKA ? CCM NA SERIKALI YAKE SI CHOCHOTE . WASUBIRI KIFO MKONONI .

    ReplyDelete
  11. Hakuna nayehusisha chadema au ccm. tunasema hivi vyama vinataka mtu "WA NDIYO MZEE" sasa Shibuda siyo type hiyo.BRAVOOOOOOOOOOOOOOOOOO SHIBUDA keep it mwanaume ni msimamo usioyumba hata ulipokuwa ccm ulipotaka kugombea urais hao ndio mzee walikushangaa

    ReplyDelete
  12. Wewe Mdee umechokoza nyuki na iko siku watakuibukieni nyie wachaga,soma hii

    "MBUNGE wa Viti Maalumu, Regia Mtema (CHADEMA) amewaomba radhi wabunge na Watanzania kwa kauli yake aliyoitoa juzi ya kuwataka watu wasio na asili ya Morogoro waondoke kwenye mkoa huo na kuwaachia ardhi wenyeji.

    Regia aliomba msamaha huo jana bungeni baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo aliomba mwongozo wa Spika kupitia kanuni ya 68(7), ambapo alisema kauli hiyo aliitoa kwa bahati mbaya." HUYU NI MBUNGE WENU LAKINI BAADA YA KUMPA KIBANO HUKO ANAJIRUDI LAKINI UJUMBE UMEFIKA. MZEE WENU MTEI AMEHODHI EKA NGAPI MKOA WA MANYARA NA ARUSHA?

    ReplyDelete
  13. WATU WAJI.NGA UTAWAJUA TU! BADALA LA YAKUJADILI ILIKUWAJE NDEGE YA KIJESHI IKAINGIA NCHINI NA KUONDOKA NA NYARA ZA NCHI BILA HATUA ZA KIUSALAMA KUCHUKULIWA WATU WANAJADILI UDINI, UKABILA WA CHADEMA! UPU.UZI MTUPU! YAANI KILA CHAMA KIKIONEKANA NI TISHIO KINAFANYIWA PROPAGANDA ZA KIPU.UZI. HATA CUF WALIITWA WADINI/WAISLAMU MIAKA MICHACHE ILIYOPITA! LEO WAPO SERIKALINI! TAFAKARI

    ReplyDelete
  14. Yote tutajadili hata USA ilipitishwa madini ya uranium kwa magendo katka nchi yao kwa miaka kadhaa juu ya utaalamu mkubwa wa kila kitu walionao,leo hiyo kwa sababu tu imeenda kwa waarabu ndio mmefanya ishu kubwa,mapadri wenu wanaingiza makontena ya madawa ya kulevya hapa nchini hamuoni? tutajadili kila kitu hata hili la wachaga kuhodhi ardhi kubwa sehemu nyingine isiokuwa mkoani kwao kama vile fitina wanayoipeleka kwenye siasa pale wanapokosa ardhi sehemu nyingine,hivi Mkapa akimiliki ardhi eka 2000 kuna tatizo gani? hao kina Mtei,Ndesa,Mbowe wanamiliki ngapi,je sisi itakuwa sawa kuhoji Mbowe anamiliki vipi Bilicanas wakati ni mali ya uma? tuache fitina za kijinga nchi imejaa ardhi kibao haijaendelezwa na haina wenyewe nendeni huko na muache fitina zenu za kukosa ardhi pahala mnaanza kuchonganisha watu. Katu watanzania hawatamkabidhi Mchaga hapewi nchi hata siku moja,wametawala makabila mengine madogo tuko salama lakini mchaga kupata mwelekeo tu tayari nchi iko mashakani

    ReplyDelete