03 August 2011

City yajipanga kutuma ofa kumnasa Nasri

LONDON, Uingereza

MANCHESTER City iko tayari kutuma ofa ya pauni milioni 22, kwa ajili ya kunasa saini ya kiungo, Samir Nasri.


Chanzo kilichopo City kilisema kuwa, wamejipanga kutoa ofa ya mwisho, ambapo wanaitaka Arsenal kuichukua au kuiacha, kwa ajili ya nyota huyo wa kifaransa.

SunSport limesema kuwa, Kocha wa Gunners, Arsene Wenger na bodi yake wanataka kumwachia kiungo huyo ambaye inaonekana hayuko tayari kuendelea na timu hiyo.

Maofisa wa City wametiwa moyo kuweza kumsaini na kwamba, Arsenal mwishoni wanataka kuweka sawa mambo na wanataka kuachana na nyota huyo.

Kulikuwa na mawazo kuwa, uhamisho unaweza kuharakishwa wikiendi ijayo, kitu ambacho kinaweza kufanya Nasri kushindwa kucheza  katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester United, ambayo pia ilikuwa ikimtaka mchezaji huyo mwenye miaka 24.

Arsenal ina uamuzi wa kukubali fedha kwa ajili ya mchezaji huyo au kukubali achezee msimu huu na kuondoka bure baada ya mkataba wa kumalizika mwakani.

Nasri alisisitiza kuwa, Oktoba angesaini mkataba mwingine kama kungekuwa na mazungumzo mapya ya kusaini mkataba wa kubakia Emirates.

Kwa sasa mchezaji huyo anaonekana anataka kuondoka, kwa kuwa City inaweza kumwongeza mshahara hadi pauni 125,000 kwa wiki, kiasi ambacho kinazidi kiwango alichopangiwa na Arsenal na United kwa pauni 10,000.

No comments:

Post a Comment