18 July 2011

Wapangaji wasiolipa kodi NHC Arusha kuondolewa

Na Queen Lema, Arusha

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), mkoani Arusha, limeanza mpango mkakati wa kuwatoa wapangaji sugu wasiolipa kodi katika nyumba za shirika ili kuepuka
hasara wanayoipata.

Meneja wa shirika hilo mkoani hapa, Bw. Jamess Kisarika, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema baadhi ya wateja si waadilifu hivyo kusababisha shirika hilo kupata hasara ambayo inakwamisha malengo waliyonayo.

Aliongeza kuwa, hivi sasa kuna baadhi ya wapangaji ambao hawalipi kodi kwa wakati hivyo kusabbisha shirika hilo kushindwa kutekeleza malengo waliyonayo.

“Hawa wapangaji wanasababisha shirika letu lipate hasara ila hapa mkoani, tumejipanga kuhakikisha mpango huu unakuwa endelevu ili kuepuka hasara za mara kwa mara.

“Dhamira yetu ni kufanya uhakiki nyumba hadi nyumba ili kuwabaini wapangaji wasio waadilifu ambao wanakiuka masharti mbalimbali pamoja na kupangisha nyumba tulizowapa kwa watu wengine,” alisema.

Alisema operesheni hiyo itaanza hivi karibuni na itakuwa na manufaa makubwa kwa maendeleo ya shirika hasa kwa kuwabaini wapangaji ambao hawajaingia nao mikataba.

“Wapo baadhi wa wapangaji ambao wanaishi katika nyumba za shirika kwa kujinufaisha wenyewe na kupata fedha nyingi kuliko sisi hivyo tunachofanya ni kuwatafuta hawa wamiliki wa mali za umma,” alisema Bw. Kisarika.

Alisema shirika hilo lina mpango wa kuuboresha mji huo kwa kujenga nyumba za kisasa katika maeneo ya Levolosi na Ngarenaro mjini.

2 comments:

  1. Napenda kazi hiyo ianze haraka. Tupo tunaohitaji nyumba hizo na tupo tayari kulipa kila kodi bila usumbufu. Watolewe hao wamezoea vya bure, na wanarudisha nyuma maendeleo ya shirika na nchi kwa ujumla

    ReplyDelete
  2. bullshit, mtu huhitaji kutangaza kwenye magazeti ishu hii, ni kama vile kumpiga mwananchi changa la macho...sio kila mtu ni mjinga hapa, hii inaonyesha jinsi shirika lilivyochafuka rushwa, huwezi kutanganza eti kuna watu wanakaa bure halafu watu wanaohusika wanakaa tuu wanangalia..."tiihi ihiiii eti mpangaji amekataa kulipa..." one need to come up with better explanation as to what is going on if not corruption!!!!!!!!!

    ReplyDelete