LONDON, Uingereza
CARLOS Tevez amesema kuwa, anataka kuondoa katika timu ya Manchester City kwa kuwa, hataki kutengana na familia yake ndogo.Nahodha wa Manchester City katika
kipindi hiki cha usajili, ameungana na Vanesa, ambaye ni mama wa watoto wake wawili
Katie (6) na Florencia mwenye umri wa miezi 18.
Mahusiano yao yaliingia dosasri kwa kuwa, hataki kuishi Manchester, ambapo alirejea Argentina akiwa ameondoka na watoto.
Licha ya kupatanishwa, Tevez amesema hakuna jinsi ya kumwambia mkewe waende kaskazini magharibi mwa Uingereza pamoja ,akiwa na familia.
Kutokana na hali hiyo, kwa sasa anataka kuiambia
City kwamba, anataka kuhama.
Juzi usiku, mchezaji huyo kutoka Argentina mwenye umri wa miaka 27, alitoa taarifa akieleza ni kwanini anataka kuondoka katika timu hiyo, baada ya kuichezea kwa miaka miwili.
Habari hizo zinaweza kufanya baadhi ya klabu kubwa za Ulaya kuanza kuvizia saini yake, ikiwemo Real Madrid, Inter Milan na Juventus.
Klabu ya Chelsea nayo imeweka rada yake kwa kuwa mkewe Tevez hapendi kuishi mji wa Manchester.
Tajiri wa Chelsea 'The Blues', ambaye ni milionea Roman Abramovich, anaweza kutoa ofa ya pauni milioni 50 iliyotakiwa kwa ajili ya nyota huyo.
Tevez alisema: "Ninasikitika kwamba, ninalazimimika kuifahamisha Manchester City nia yangu ya kutaka kuondoka. Ninataka kusema kwamba, ninaiheshimu sana klabu, mashabiki na mmililiki Sheikh Mansour, ambaye hana kitu kingine zaidi ya kuniheshimu.
"Ninatumaini kwamba, watu wataelewa hali ngumu niliyokuwa nayo katika miezi 12 iliyopita, kwa kuangalia familia yangu.
"Kuishi bila ya watoto katika mji wa Manchester imekuwa changamoto kwangu.
Amesema anajivunia kwa kipindi alichochezea Manchester City akiwa kama nahodha, kuiwezesha kutinga Ligi ya Mabingwa na kutwaa ubingwa wa Kombe la FA.
Vyanzo vilivyo karibu na Tevez vimesema kuwa, kuhama kwake hakuchangiwi na tamaa ya kutaka fedha.
Kuna habari kuwa, Inter Milan inamhitaji ambapo katika mkataba, inataka kumhusisha Samuel Eto'o kuhamia Eastlands.
Tevez hamna lolote, Columbia wanamchemsha yeye na Messi sasa hivi.
ReplyDelete