13 July 2011

Maradona apata ajali, alazwa

Buenos Aires, Argentina

MCHEZAJI nyota wa zamani wa Argentina, Diego Maradona amepata majereha madogo baada ya kupata ajali nje ya mji wa Buenos Aires.Kwa mujibu wa
Daily Mail, Maradona mwenye umri wa miaka 50 na patina wake Veronica Ojeda, walipelekwa hospitali baada ya kupata ajali wakati gari lao lilipogonga basi, kabla ya mechi ya michuano ya Copa America kati ya Argentina dhidi ya Costa Rica.

Maradona inasemekana ameumia goti na Ojeda paja, lakini Oscar Sico, Mkurugenzi wa Hospitali ya de Ezeiza, anaiamnihawajaumia sana.

Aliiambia Radio 10: 'Wako katika hali nzuri.'

Sico aliongeza na kukaliliwa na kituo cha televisheni cha C5N: "Walikwenda kwenye (hospitali) yao, lakini hawana matatizo. Wote wanaweza kwenda nyumbani."

Chanzo cha ajali kinachunguzwa.

Maradona alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, wakati ilipotwaa ubingwa wa Dunia 1986 na aliinoa timu ya taifa ya Argentina kwa miaka miwili hadi 2010.

No comments:

Post a Comment