Na Waandishi Wetu, Dar, Morogoro
WATU watano wamekufa kwa kuungua moto baada ya basi la Hood T.762 AVL lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Arusha kuungua katika Hifadhi ya Mikumi mkoani
Morogoro.
Katika ajali hiyo abiria 40 walijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Morogoro kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Bw. Joseph Lugilla alisema ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na lori la mafuta ya kula lilolokuwa likitoka Morogoro kwenda Iringa.
Akifafanua zaidi, alisema chanzo cha tukio hilo ni menejimenti ya mbunga ya wanyama Mikumi kuendesha shughuli ya usafi wa mazingira ya wanyama pembezoni mwa mbunga hiyo kwa kuchoma moto nyasi
iliyosababisha moshi mwingi uliosababisha madereva kushindwa kuona kilichokuwa mbele yao.
Bw. Lugila alitaja majeruhi wa tukio hilo ni Benito Suga (34), mkazi wa Arusha; Peter Benilo (35), Kondakta wa basi hilo, mkazi wa Kibaha; Leila Mgina(23); Amran Salehe (32) mkazi wa Iringa, Jemes Shitindi (36) mkazi wa Mbonzi na Mirika Maneno (7) mkazi wa Same.
Wengine ni Charles Yesaya (21) mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni Mwanajeshi mwenye namba JWTZ-MT 0860; Jorada Mwasifike (46) mkazi wa Mbeya; Beatrice Mafuti (50); mkazi wa Ifunda; Joyce
Kamkanila (11) mkazi wa Kihonda, Morogoro; Asha Maneno (34) mkazi wa Same; Godson Sokreti (27) mkazi wa Arusha na mwalimu wa Sekondari ya Mrama, pamoja na Rose Zambi (43) mkazi wa Mbeya.
Alitaja wengine ni Zenolina Marick(23) mkazi wa Arusha, Maria John (36) mkazi wa Iringa, Naropili Siroia (29) wa Arusha, Bahati Chonya (35), mwanasheria wa Manispaa ya Moshi, Salehe Tembo (42) mkazi wa Dar es Salaam ambaye alikuwa dereva wa basi la Hood, Mbeleselo Joseph (33) daktari wa Hospitali ya Rufaa KCMC Moshi, Pius Mupitia (23) wakala wa Vodacom, Nestor Ngao (24) mkazi wa Mbeya ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Dakawa.
Pia walikuwamo Evans Mwasifiga (55), mwalimu wa Sangu Sekondari; Godlivin Fred (23), mwanafunzi wa chuo cha Ruha; Monica Toloiya (59) mkazi wa Loliondo, Arusha; Richard Lubulu (52)
mfanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa; Janny Stesioza (26) mfanyabiashara wa Moshi njia panda Himo, Teodori Raphael (20) mwanafunzi aliyehitimu Seminari ya Same; Janny Fred (24), mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa; na Erica Malimbwi(19) mwanafunzi wa sekondari ya JJ Muungano.
Majeruhi wangine waliotambulika ni pamoja na Cheso Lubulu (50) wa Mkinga, Anastazia Kisera (48) na Kisa Mwakilubwa (40) wa Tukuyu, Mbeya.
Awali, taarifa zilizolifikia Majira zilidai kuwa magari hayo yaligongana uso kwa uso kutokana na moto uliokuwa umechomwa katika mbuga hiyo, hivyo kusababisha moshi kutanda barabarani.
Baada ya kugongana, basi hilo liliangukia sehemu ambayo moto ulikuwa ukiwaka hivyo likalipuka, hivyo mpaka jana usiku watu wengi walidaiwa kufa, huku wakipatikana majeruhi 46, waliopelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu.
Sasa inakuwaje tunaishi kama kuku! Hatutumii akili kabisa tunaendeshwa na matukio. Watu ya mbuga ya wanyama wanatakiwa kushitakiwa kwa kufanya kitendo hatarishi. Vipi askari wa usalama barabarani hawakuona hilo! Kila kitu tukipe mtazamo chanya na kwamba our action cannot cause problem to other!
ReplyDelete