*Asema mbunge akikataa mikutano mitatu atafukuzwa
Na Tumaini Makene
HOJA ya kupinga ama kukubali pendekezo la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni la kuondoa posho za vikao wanazolipwa wabunge na watumishi wa umma, imeendelea
kupamba moto huku Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda akisisitiza kuwa ni lazima kuchukua posho hizo, ikitokea mbunge hazajasaini kuzichukua kwa mikutano mitatu mfululizo anafukuzwa bungeni.
Wakati Spika Makinda akitoa kauli hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe ambaye ameshaandika barua kutaka aondolewe katika utaratibu wa kulipwa posho, amesema kuwa yuko tayari kufukuzwa aende kulima au kuvua dagaa, kuliko kuzichukua.
Kauli hiyo ya Spika Makinda inakuja siku moja baada ya wabunge wa Chama Cha
NCCR-Mageuzi, kusema kuwa leo watawasilisha nakala ya barua kwake na kwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo kuwa wanataka posho zao zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo Mkoa wa Kigoma.
Spika Makinda pia ametoa kauli hiyo siku mbili kabla ya kusomwa kwa hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambayo ina mapendekezo mengi likiwemo hilo la kuitaka serikali kuachana na utaratibu wa kuwalipa watumishi wa umma posho za vikao, kwa majukumu ambayo ni sehemu ya kazi zao, ambazo tayari wanakuwa wameshalipwa mishahara na pengine fedha za kujikimu.
Kauli ya Bi. Makinda ambayo sasa inaonekana kutaka kuwabana kisheria wabunge ambao wameshaamua kuzikataa posho hizo, kabla hata pendekezo hilo halijaingia bungeni kwa ama kuridhiwa ama kutoridhiwa, pia imekuja siku chache baada ya Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe kuweka wazi kuwa kuondoa posho kwa watumishi wote wa umma, wakiwemo wabunge, ndiyo msimamo wa kambi hiyo ili kuisaidia serikali kuondokana na mzigo wa matumizi makubwa, kuelekeza fedha hizo katika maendeleo ya wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika maeneo ya bunge, Spika Makinda alisema "Hili suala liko kisheria, mbunge asiposaini posho katika mikutano mitatu mfululizo anahesabika kuwa hayupo, hivyo anafukuzwa bungeni, kwa hiyo sisi tutawahesabia tu...lakini pia hili suala la mshahara wa mbunge linakuzwa, hizo milioni saba zinatoka wapi...mshahara wa mbunge ni milioni 2 na nusu...kabla ya kodi, kisha kila mwezi anakatwa laki tisa za mkopo wa gari, anakatwa kodi laki tano," alisema Spika Makinda kwa kifupi.
Jitihada za kumpata Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Bw. Mbowe ili azungumzie kauli hiyo ya spika, hazikufanikiwa lakini kwa upande wake, Bw. Kabwe alisema kuwa kama ni suala la kufukuzwa yeye yuko tayari.
"Kwa upande wa kambi atajibu kiongozi wa upinzani. Kwa mimi kwanza sitaki malumbano na Spika. Namheshimu. Pili, kama adhabu ya kukataa posho ni kufukuzwa ubunge nipo tayari. Nitarudi Kalinzi kulima kahawa kwa heshima. Au Mwamgongo kuvua dagaa," alisema Bw. Zitto.
Taasisi yaunga mkono
Taasisi ya Muungano wa Harakati za Kimaendeleo (ADO) imeunga mkono hoja ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe ya kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge na watumishi wengine wa umma ili zisaidie shughuli zingine za kijamii kama shule,afya, maji, miundombinu na zingine, anaripoti Gladness Mboma.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa ADO, Bw. Ntamilyango Buberwa, alisema vitendo vya baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali kutaka kuendelea kupewa posho, ikiwemo misimamo tofauti inayotolewa na viongozi wa bunge akiwemo Spika Bi. Anna Makinda vinatoa mashaka katika uzalendo wao hasa katika kusimamia maslahi ya umma.
"Viongozi hawa wanatupa wasiwasi wanapotoa misimamo kama hii, misimamo ya namna hii ni kukosa dhamira ya kweli katika uwakilishi wao kwa maendeleo ya wananchi,"alisema
Alisema katika nchi masikini kama Tanzania ambapo kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi hakizidi 160,000 kwa mwezi ni aibu kwa mbunge kukubali kulipwa fedha za walipa kodi masikini wa Tanzania.
"Wakati serikali inasema haina fedha za kutosha kulipa madai zaidi ya miaka 33 ya wazee wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, walimu na wafanyakazi wengine wa kada na idara mbalimbali kwa ujumla ni matusi makubwa kwake kutenga zaidi ya bilioni 900 kwa ajili ya kulipana posho zisizo na kichwa wala miguu,"alisema.
Bw. Buberwa alisema taasisi hiyo imeanzisha kampeni maalum ya kupokea maoni ya watu wasiopungua milioni moja nchini kote kabla ya kusomwa kwa bajeti ya Wizara ya Fedha na kuyawasilisha kwa Rais lengo likiwa ni kushinikiza posho zisizo na tija kufutwa.
AMMA SASA TUNAINGIA KARNE YA WAZEE!!MAANA SIONI LOJIKI MTU ANAKATAA POSHO ANALAZIMISHWA KUWEPO NA FOMU MBILI TOFAUTI YA KUHUDHURIA KIKAO CHA BUNGE NA FOMU YA MALIPO YA POSHO,HUWEZI KUMFUKUZA MBUNGE ETI KUKATAA POSHO HIYO NI HAKI YAKE NA KUKATAA PIA NI HAKI YAKE.KAMA MNAONA ANATAFUTA SIFA BASI HIVYO MNAVYOLIKUZA NDIO MNAZIDI KUMPA SIFA,NYIE MNAONG'ANG'ANIA HIYO POSHO CHUKUWENI MPK HAPO SHERIA ITAKAPOPITISHWA YA KUFUTA HIZO POSHO. NAWE NDUGU YANGU ZITO KAMA NIA YAKO NJEMA BASI FUNGUA AKAUNTI UWEKE HIZO PESA ZIELEKEZE ZIPITE MOJAKWAMOJA KDI.SPIKA ANAGALIA KIFUNGU CHA KUMFUKUZA MBUNGE NI VIKAO 3 AU SIKU 3? NA ITAKUWAJE UMWAMBIE HAKUHUDHURIA WAKATI ATAKUWEPO BUNGENI? UHAKIKI NI SAINI AU UWEPO WAKE?JE, MTU AKISAINI AKAONDOKA INAKUWAJE?USIKURUPUKE
ReplyDeleteMama Spika asiwe na hasira,hiyo sheria kama ipo ya posho ajue ilitungwa na imefika mwisho wake maana haina tija.walitunga watu kama yeye na muda wa hiyo sheria unatenguliwa,na bila watu kukomaa na kuzikataa hizo posho,mabadiliko hayatafanyika.mama utambue migomo mingi imeleta mapinduzi,bila mgomo chuoni mapinduzi hakuna. La msingi kubadili hizo sheria za kujazia matumbo machache na kuacha wengine wahanga.wananchi wamekutuma uwatumikie,wewe unangangania posho,jimboni kwako watoto wanakaa chini hakuna dawati,jimboni kwako wamama wanazalia njiani,hakuna zahanati wala gari, jimboni kwako hawajui maji salama ya bomba zaidi ya kisima kimoja kata nzima,leo unakaa kimya unagombea posho,dhamira ibadilike.kama wabunge wa zaman walibobea posho sasa ni kizazi kipya cha mabadiliko,sheria nyingine mgando zibadilike haraka sana,zinaumiza wananchi.hizo posho mnangangania ongezeni pensheni kwa wazee wanaostaafu hasa waalimu waweze kutunza uzee wao.mkubali mabadiliko,yatatokea maandamano.mtajifungia huko bungeni mtalala hukohuko.
ReplyDeleteHivii hawa viongozi wetu wanafikiri kwanza kabla ya kusema au kutoa tamko? Hawana aibu hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kuelewa kipi kinachoendelea. Mtaliibia taifa letu kwa style zenu hizo mpaka lini? Tafakarini kabla ya kutoa maamuzi. Siku za mwizi ni arobaini. Mimi ninapenda sana mawazo ya Zitto, nikizingatia jinsi jimbo lake lilivyoduni, anao uchungu wa pesa za kuleta maendeleo eti yeye aziweke mfukoni, ALUTA CONTINUE ZITTO, usiwasikilize hao. Zidi kuwatete wanyonge!!!! ANNA mshipa wako wa aibu pamoja na hao wafanyakazi wa bunge umepata kiharusi wewe na watu wako. WATANZANIA WANATESEKA, na nyie mnafuja pesa zao, za mkulima, mvuvi muuza maharage na unga. Tumechoka!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeletehaina maana m2 kulipwa posho kwa kazi ambayo imo ktk majukumu yake ya kila cku,hayo ni malipo mara 2 na ni ubadhirifu.Nimefurahi NCCR kuunga mkono hoja hii haina maana aclimia 75 ya bajeti ma2mizi ya kawaida ya serikali 2taendelea lini huko c ni sawa na kufanyia kazi tumbo tu unakula leo unatafuta ya kula kesho bac.hatuna umeme wa uhakika,reli nayo hakuna wakati zinahitaji pesa ndogo 2,ccm badilikeni jamani 2cje kuondoa kwa aibu hata mctamani kusema mliwahi kutawala nchi hii......
ReplyDeleteKwa kweli sasa nimeamini kuwa Tanzania haina Spika wala haina "future" inayoeleweka hata kidogo. Kwanza kabisa, niungane na Anonymous 10:22PM. Tafsiri ya mikutano ya bunge ni "Sessions" za bunge na sio vikao anavyovisema Mh. Zito (k.m. vikao vya uongozi wa bunge, kamati ya sera, masuala ya kijamii ya bunge n.k. ambavyo ndivyo analalamikia zaidi hizo posho kulipwa). Mkutano tafsiri yake ni kama kusema mkutano/ Kikao cha kumi cha bunge...
ReplyDeletePili, ni kuwa mtu kuhudhuria kikao hata kama ni vinginevyo zaidi ya vile nilivyovitaja hapo juu, tafsiri ya kuhudhuria ni kulipwa posho au ni kuwepo katika kikao na kuchangia hoja za kikao?? Hivi Mh. Zito akiwa ndio Mwenyekiti mathalani katika kikao na wakafanya maamuzi mbalimbali, hizo miniti za kikao hazitatambulika kwa kuwa hakupokea posho??
Tatu, kwanini Spika ambaye kimsingi ningeamini ni muelewa wa sheria japo yeye ni karani wa hesabu za kiuhasibu kisheria; anadhani kuwa kutishia Mbunge sheria ambayo nayo kitafsiri amekosea, atamtisha mtu?? Kwani ni lazima ukurupuke kutolea maelezo?? Huwezi kusema angalau kama alivyosema naibu spika?? Kwanini Spika aendeshe mhimili wa dola kwa hisia zaidi badala ya kuzingatia hoja?? Aibuuuuu. Hicho kiatu kinakupwaya mama, chukua hatua mapema mama, unaaibisha!! Hufai hata kidogo.
Tatu ambalo ni la msingi ni kuwa, kwanini viongozi wetu wakipata wazo zuri kama hili wasitulie na kufanya upembuzi yakinifu na wa dhati ili kupata suluhu yenye manufaa kwa taifa letu?? Mh. Zito anasema, nchi yetu ni maskini, wabunge wana mishahara tena minono tu ambayo inalipwa kwa kuwa ni wafanyakazi wa "bunge", hivyo hawastahili kulipwa posho wakati wako katika vikao wakiwa kazini. Kwa kiongozi makini, unatakiwa uchambue na upambanue hoja kwa nguvu za hoja na sio kwa hoja za nguvu. Badala yake Mkulo anaishia kusema huo ni unafiki na kuanzisha fomu nyingine za posho; Spika nae anakurupuka, ntafukuza mbunge.... That is damn Stupid!!! Yaani hamuwezi chambua vipaumbele? Jengeni hoja ni kwanini Mbunge apate allowance mara mbili au tatu kwa siku inapotokea vikao hivyo?? Mjibuni Zito, msitishie watu nyie kenge!! Mnazidisha unazi kwa chama unnecessarly kweli. Vilio vya wananchi vitasikilizwa wapi kwa mpango huu??
Nne, Hoja ya kukataa posho halafu ipelekwe KDI nayo haina mshiko; maana bado itatafsiriwa kuwa umeikataa kama mtu binafsi lakini ikienda huko maana yake bado ni yako tu; maana ipo jimboni kwako. Nilidhani basi kuwa pawepo na hoja ya kukataa posho kwa kuwa ni mzigo kwa taifa na sio utashi wa mtu anavyojisikia; japo ni hatua ya kupongeza. Hivyo basi, haifai kukataa posho na kisha ikaenda jimboni kwako. Kataa posho ili kama wote mtaikataa iwe ni fungu litakalosaidia kuleta maendeleo katika sekta fulani kitaifa.
Otherwise, naendelea kusikitishwa kwa kauli za viongozi wetu ambao wanaleta "mipasho ya taarabu" ndani ya muhimili muhimu wa dola. Shame on you Md. Speaker and the Minister for finance.
Naona ni muhimu kuitisha maandamano ya AMANI kumuunga mkono bwana ZITO ili wananchi wanufaike na matunda ya nchi yao.Kwani sasa hivi wasomi na wataalamu wa fani mbalimbali wanakimbilia SIASA kwa ajili ya hizo posho kwa sababu ya mishahara midogo.Pia viongozi waelewe kuwa wa tz wa sasa sio wale wa mmiaka ya 80 kurudi nyuma!kila mtu anaelewa ni nini kinaendelea.KABWE OYEEEEEEEEEEEEEEEE!
ReplyDeleteHivi nyie mliemchaguwa huyu mama spika ANNE mnajuwa anatupeleka wapi, maana ukweli hana busara kaanza na kufunga barabara sasa hivi kama muonavyo kitu cha busara ni kujadili na siyo kuonyesha misuli na hii ndiyo tabia ya viongozi wengi wa kiafrika kujiona miungu watu tunajua nchi yetu siyo masikini angalieni matumizi ya viongozi, na kima cha chini cha mshahara wa mtanzania sasa kiongozi kama zitto anayaona haya siyo hao wanaojali maslahi yao na kusahau hata waliowaweka hapo. Kuwa shujaa muhishimiwa zitto tuko sote ila wajue cheo ni dhamana ole wao kelele kila kukicha eti sisi masikini ili wapate fursa ya kututawala kirahisi na kama mnadhani mnatawala matahira subirini muone, maana hata vitabu vya dini vinasema siku hiyo ikifika kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe ALLUTA
ReplyDeleteNinaungana mkono mawazo mazuri ya kuipunguzia serikali gharama kubwa. Ni kweli ya kwamba Zitto anaonyesha uzalendo.Ili kusiwe na malumbano yasio na maana kwa sasa Wabunge chukueni posho zenu kisha mkazitoe majomboni kwa ajili ya maendeleo. Kisha swala hili lipitishwe Bungeni ili muweze kulijadili na kubadilisha sheria mlioitunga wenyewe kwa busara.
ReplyDeleteSina hakika na busara za Mhe. Spika zinazotumika kuendeleza malumbano ya posho ambayo ni haki ya mtu kuipokea au kutoipokea. Mbona Bunge letu tukufu limeanza kuelekea pagumu katika kuingilia kwanza uhuru wa mtu na pili kupoteza muda. Nape kasema sawa, suala hili lina nafasi ya kujadiliwa na kuona je, iko haja ya kuendelea kutoa posho hizo au la? Majibu yangepatikana tu badala ya malumbano haya yasiyo na tija. Hivi sisi wapiga kura tumewapeleka Bungeni kwa ajili ya kushinikizaa posho lazima zilipwe au ni suala la mantiki tu. Hizo posho za waheshimiwa zinazotajwa na Mheshimiwa Spika zinakatwa kodi na TRA kama sheria zinavyosema ? Je, si kweli magari yanayosemakana wanakopeshwa wanapewa Bure ? Ebu ondoeni hizo posho kama kuna mbuge atakayekopa gari na kumaliza kulipa deni kwa wakati mwafaka ? Posho hizo na kutumia nafasi ya ubunge kutekeleza azma binafsi ndicho kinawafanya wengi kukimbilia ubunge, hususan wale wenye tamaa. Mheshimiwa Spika, waache Waheshimiwa wabunge wenzako wanaotaka wachangie posho zao kwa maendeleo ya majimbo yao wafanye hivyo. Aliyenunua kura za wananchi anastahili posho hizo ambazo ni jasho la wapiga kura wako iwe ndiyo marejesho na adhabu yao.
ReplyDeleteHivi ni mantiki kweli ulipwe mara mbili kwa kazi hiyo hiyo ? Mimi ningetumia utaratibu wa Serikali wa kiongozi kutoa asante kwa kazi nzito ya mara moja kuliko kufanya kuwa ni utaratibu ? Mbona wahudumu wa ofisi na hata wenye mishahara kidogo huko katika ofisi wanapopata malipo ya ziada kwanza yanahakikiwa kwa ajili ya kukkatwa kodi na TRA na pili si jambo la kila mwezi ? Posho inakuwa kubwa kuliko mshahara na unakuwa utaratubu wa kilamwezi hadi bunge kuisha ?
Lipe fursa Serkalim iangalie utaratibu mzuri zaidi.
Si kila kinacholetwa na wapinzani ni kutaka umaarufu. It is a rational thing.
Mimi sioni sababu ya mh. Zitto kuogopa kauli ya Spika mama Makinda. Kama ni swala la kisheria basi mh. Zitto basi zito ahudhurie bungeni na achangie kama kawaida halafu apate nakala ya mikanda ya video/TV records ambazo huchukuliwa live kila siku zikionyesha tarehe na muda wa kikao. Halafu aende mahakamani ku-challenge kufukuzwa bungeni kwa vile hajasaini mara tatu. Mh. aitake mahakama itoe tafsiri ya kukosa vikao vitatu mfululizo inatafsiriwa kwa kusaini tu au uwepo halisia wa mbunge kwenye vikao vyake rasmi. Mimi naamini akienda na ushahidi huo pia na kumbukumbu za bunge (hansard) kwa siku hiyo kwa vyovyote atambwaga Makinda katika swala hilo. Makinda anatumia mbinu za enzi za nuhu/ujima. Makinda anahitaji kuonyeshwa namna ya kutumia usomi na akili kutatua complex issues.
ReplyDeleteNADHANI MAGAZETI,WATOA MAONI NA AKINA ZITO WANAPOTOSHA WATANZANIA.
ReplyDeletePALE BUNGENI KUNA UTARATIBU WA KUSAINI MAHUDHURIO KAMA ILIVYO SEHEMU NYINGINE YOYOTE YA KAZI ILI KUBAINI WALIOKUWEPO SIKU HUSIKA. POSHO NI JAMBO LINALOFUATIA KWAMBA ITALIPWA KWA KWA KUINGIZIWA KATIKA AKAUNTI ZAO BENKI KWA SIKU WALIZOHUDHURIA. 1. TARATIBU ZA KUBADILISHA SHERIA ZINAJULIKANA NA HAZIJAFUATWA NA HAZIWEZI KUBADILISHWA KWA MAANDAMANO NA NGONJERA. WAHUSIKA WAPELEKE HOJA BUNGENI.
2. MAADAM AKINA ZITO WANAJUA KWAMBA UTARATIBU WA KUBADILI SHERIA UNACHUKUWA MUDA NA WAO WANGEPENDA POSHO ZAO ZIENDE KWENYE MFUKO WA MAENDELEO JIMBONI KWAO KWANINI WASIZIPOKEE NA MWISHO WA SIKU WAKAANDIKA CHEQUE KUINGIZA FULL VALUE KWENYE AKAUNTI HUSIKA NA WAO KUPEWA RISITI.NA WAKIPENDA SIFA KAMA INAVYOONEKANA WAWAITE WAANDISHI WA HABARI NA KUTANGAZA WAKATI WAKIKABIDHI.
3. KAMA HOJA ILIKUWA KUPUNGUZA MATUMIZI YA SERIKALI BASI HOJA INGEKUWA BAJETI IPUNGUZWE KWA KIASI HICHO CHA POSHO ILI ANGALAU PESA TULIZOWEKA KAMA MKOPO WENYE RIBA KATIKA BAJETI ZIPUNGUZWE NDIPO MANTIKI ITAONEKANA.
4. PESA NI ZA WATANZANIA WOTE NA KIUTARATIBU MTUMISHI WA UMA UKACHANGIA KUOKOA ZINAPASWA KURUDI KWENYE KAPU ILI IAMULIWE WAPI ZITAHITAJIKA ZAIDI NDIKO ZIPELEKWE SIYO KUPANGA WEWE AS AN INDIVIDUAL.
MSIJADILI HOJA KWA JAZBA NA USHABIKI.
MASUALA HAYA YANAWAGUSA DIRECT WAFANYAKAZI,JE KATIKA UTEKELEZAJI WA DEMOKRASIA MMEKAA NA WAFANYAKAZI KUPITIA VYAMA VYAO NDIPO MKAJA NA HILI AU? NA MMEAINISHA POSHO MNAZOTAKA ZIONDOLEWE?
weweeee!!!!!!! serikali hii haisikii,dawa yake ndio kuonyesha vitendo kama hivyo ukijidanganya eti upeleke kwa kulijadili, nanii atakubali, hili halikuanza leo,wabunge wasisiemu ni wabinafsi,hawana uchungu na nchi hii, ndio maana wengi wamehonga ili kuingia bungeni. sasa kuondoa posho wakati ni moja ya mikakati yao watakubali wapi?
ReplyDeleteHakuna hoja inayotoka upinzani inayokubalika na huyo mama pamoja na wenzake(CCM).
ReplyDeleteTunakumbuka hoja ya posho za wabunge zilipigiwa kele kabla, CCM na hata wananchi (inasikitisha kuona jinsi tunavyodanganyika kirahisi) wakashika bango wakisema, "mnapigia kelele posho mbona hamzikatai?" Sasa leo wamezikataa, mnawwambia msiposaini siku 3 mnafukuzwa --UPUUZI MTUPU!
Mi najua sheria mama inasema hakuna kupokea mishahara miwili. Sasa iwapo majukumu muhimu ya mbunge ni kuhudhuria bunge, ule mshahara amba spika kautaja mil 2.5 ni kwa ajili gani? Unahitaji kweli kuwa mwanasheria kulijua hili? Na hiyo sheria ya kulipa posho za wabunge ni sheria ipi? Tutajiwe na vifungu vyake, ili tujue jinsi walivyojitungia sheria ya kutuibia, kama ambavyo wamei-exempt mishahara yao na kodi as if wao si watz!! Kauli yangu ni hii - Yote ni majizi, na hayataki kuacha kuiba!
Halafu suala hili ni pana zaidi - posho hazikataliwi kwa wabunge tu - ni wafanyakazi wote wa serikali.
zito msomi,ataingia bungeni,na hatasaini,na hatafukuzwa bungeni,huyo mama apotezee maana elimu yake na zito tofauti,hamwezi kesi zito atambwaga mbali,wakili hamsaidii mama huyu,apotezee.zito hataki pesa.basi.kula na ccm yako mzidi kuvimbiwa.tumewazoea
ReplyDeleteJamani hakuna midume ika-mtombe huyu mama ili afunguke akili? Mwanamke yeyote asiye na mume hafai achilia mbali kuongoza. Ndio maana yesu alikuwa na wasaidizi wanaume tu na Quran inasema 'Ole wao watakaoongozwa na wanawake'! Makinda toka la si sivyo tutakuingilia kinyume na maumbile! Wale vijana wa UDOM wangepenya saa hizi ungekuwa unajipaka salimia liniment kupoza maumivu nyama wee!
ReplyDeleteJamani tuwaache hao wavue gamba kwanza, ndio baadaye wataelewa mantiki ya kuondoa posho!! Taabu ni kwamba magamba yenyewe hawayajui, watayavuaje?
ReplyDeleteGamba kuu ninaloliona mimi ni fikra, likifuatiwa na umimi kabla ya ufisadi. So ufisadi (ambao ndio wanauona gamba na ambalo limewashinda kuvua)ni matokea ya fikra finyu kama hizi za kulazimishana posho, zikisukumwa na umimi.
Therefore, an effective way ya kujigambua ni kutafiti fikra na kuzi-straiten up, hapo dhamira ya kupambana na maouvu itakuwa thabiti!
hawatakaa wavue gamba maana gamba likitoka sumu inabaki,na linaota gamba jingine.na hilo gamba linafanana na la kwanza.haitakaa itokee wakubali mapungufu yao,wameshajua chama ni chao hakuna mwingine wa kukiweza,waliacha makamba kakiuua kabisa leo ndo kumekucha kwao.watavua gamba na waliona makamba anatoka wakamweka mtoto,hilo gamba litakaa liishe na huku wanarisishana,chama cha urithi kile,achana nao,wanalindana kuliko watoto wa tumbo moja,hakuna kuchukua posho.hawaachi ndo ccm,ndo zinawapa uhai.walafi wale,wote matumbo makubwa,kusinzia bungeni na kusaini jioni.
ReplyDeleteSielewi jamani, hivi na sisi ambao sio wanasiasa tunakubali vipi kuingia mchezo wao, kwa mfano wakati Sheria inasubiriwa ya kufuta posho,kwa nini wabunge wasichukue posho hizo, wakazipeleka katika saccos mbalimbali majimboni mwao? Kuna Ugumu gani jamani au ndo kutaka kuendelea kuwa front pages
ReplyDeleteNafikiri hapa sio suala la kuwa front page, suala hapa ni kuwa kuna matumizi mabaya ya fedha. Kiuchumi wataalamu wanaita "Double payment" ingawa hii imehalalishwa na hawa walafi kwa kisingizio kuwa wamefanya kazi ya ziada. Hoja ya Mh. Zito ni kuwa wasilipwe kwa kuwa wanapata mshahara kwa kazi hiyo. Sasa suala sio kupeleka fedha Saccos wala majimboni kwao. Tunapolijadili suala hili, tunatakiwa kuliangalia kitaifa zaidi na sio kibinafsi. Ndo maana nasema tuliangalie kama mzigo wa taifa na jinsi ya kulitatua. Kusema posho ziko kisheria ni kweli lakini sheria hizo ziliwekwa na watu (wabunge hao) na kwamba zaweza kubadilishwa kuleta tija katika taifa letu. Period!!! Hakuna siasa wala ushabiki. Nilipochangia hapo awali nilisema kuwa wanaoipinga hoja ya Zito, wahalalishe malipo hayo kwa nguvu za hoja sio kwa hoja za nguvu. Ukikurupuka kusema "wanafiki" au tutachukua sheria kuwafukuza; hapo hujatatua tatizo. Kuwa makini Anonymous 8:53AM.
ReplyDeleteNdiyo maana nimemsoma an.no.10.54 kuwa sheria ilitungwa na watu,na inabidi hao watu waibadilishe ikiwa haikidhi mahitaji ya taifa.tusingangane na sheria mgando ambazo hazina tija. posho hiyo hakuna haja aichukue mtu mojamoja apeke jimboni kwake.kuwa isitengwe kabisa,serikali bl.900 zote za posho za ajabu ajabu za nini,hilo fungu elekezeni kwenye afya,vituo vya afya vijijini havina hata umeme wala generator, watoto mashuleni hawana dawati wala kikombe cha uji, walimu huduma zao duni, mnataka mwl aende kijijini akafundishe sekondari ya kata(vodafasta)hana nyumba,wala baiskel atembee klmeta 10 kufundisha,posho ya kujikimu hakuna,mnataka elimu ipande,ipandeje? kwa miujiza,nani atakubali kwenda huko porini huduma za jamii hakuna,nyie mjikatie maposho ya ajabu hapo dodoma,mkae mtafakari,huduma za jamii kwanza;mnachopewa salary kama wabunge yatosha.basi.posho ziishie hapo.yatosha.
ReplyDeleteUPUMBAVU WA MJADALA HUU:
ReplyDelete1. HAKUNA SABABU YA KUMLAZIMISHA MBUNGE ACHUKUE POSHO.
2.WANAOKATAA WASIIAMBIE SERIKALI IPELEKE MAJIMBONI WAPELEKE WENYEWE AU VYAMA VYAO VIPELEKE. NA KAMA HAWATAKI KUPELEKA WENYEWE ZIWEKWE KWENYE AKAUNTI YOYOTE YA DHARURA.
3. NILIFIKIRI WABUNGE WANA AKILI KUMBE PUMBA TUPU HILI SI SUALA LA KUTANGAZA AU KULUMBANA MNAJIONYESHA MLIVYO DHAIFU WA AKILI NA WANAOWASHABIKIA NDIO TAAHIRA KABISA