02 June 2011

Wafugaji Rwanda waua Watanzania sita Ngara

*Kamati ya Ulinzi na Usalama yasaka watuhumiwa

Na Theonestina Juma, Bukoba

WATANZANIA sita ambao ni wakulima wa Kijiji cha Murbanga Kata ya Mursagamba wilayani Ngara mkoani Kagera wamevamiwa shambani na kuua kikatili na
wafugaji wanaosaidikiwa kuwa ni raia wa Rwanda.

Tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati wakulima hao wa Tanzania wakiwa wamepiga kambi katika eneo la pori lililoko katika kijiji hicho, kwa ajili ya kuandaa mashamba kwa kusubiri mvua za vuli na kulinda mazao yao yasishambuliwe na wanyama.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Bw. Vitus Mlolere zinasema kuwa waliouwa ni wanaume.

Habari hizo zinadai kuwa katika tukio hilo, wafugaji hao ambao ni raia wa Rwanda (idadi haijafahamika) walipowakukuta watu hao katika mashamba yao ambako wamejenga vibanda vya muda kwa ajili ya kupumzikia, waliwakamata na kuwafunga kamba mikono kwa nyuma na kuanza kuwashushia kipigo kwa kutumia fimbo na marugu hadi kufa.

Wakulima hao walikuwa wanane, wawili kati yao walikimbia na kunusurika katika mauaji hayo.Miongoni mwa walionusurika mmoja alikimbia hadi kwa wananchi wanaoishi jirani na kutoa taarifa.

Kwa sasa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara kwa kushirikiana na polisi kutoka Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa imepiga kambi katika pori hilo kufuatilia tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwasaka Wanyarwanda hao wanaosakidiwa kufanya mauaji hayo.

Kati ya waliouawa, watatu wametambulika kuwa ni Bw. Karabanye Daniel (70), Benedict Bashogongo (65) na Selestine Mawela (47).

Wakulima wa Kata ya Mursagamba kila mara wamekuwa wakizozana na wafugaji wa Kinyarwanda kwa kuacha mifugo yao kushambulia mzao yao kila kukicha.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Bw. Mlolere alisema kuwa atatoa taarifa za mauaji hayo leo.

5 comments:

  1. kamata hao wauaji wamezoea kuuana kwao wasituletee mabalaa yao

    ReplyDelete
  2. Hakuna kiongozi wakufuatilia mauaji haya, inasikitisha sana serikali ya Tanzania yenyewe niyawauaji sasa unadhani ndugu yangu watahangaika kufuatilia raia waliouawa na wageni? nchi haina kiongozi in waigizaji na wauaji

    ReplyDelete
  3. mwambieni dr wenu afatilie sihakuna kiongozi wa kufatilia?

    ReplyDelete
  4. Kile chama kinachopenda kutumia maiti kisiasa wahi haraka kuchukua hiyo miili. Yule mbunge wenu mTundu yuko wapi hajafika Ngara? Fanya fasta, tekeleza mikakati yenu kama mlivyokubaliana. Tafuta na wapiga picha wa kigeni, litakuwa kosa kubwa kuachia hii dili.

    ReplyDelete
  5. NDUGU YANGU WA MAONI YA 1:21
    UNAONYESHA KUWA UNA USHABIKI USIOFAA NA AMBAO HAUNA MAANA HIVYO INAWEZA IKAWA HATA KULETA MAENDELEO IKASHINDIKANA KWA WATU KAMA NINYI, KWASABABU UMEAMBIWA KABISA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAKO POLINI WAMEWEKA MTEGO WANAFUATILIA, JE WASINGEFANYA CHOCHO INGEKUWAJE. TUWE MAKINI HUKO SIO KUPENDA NA WATU KAMA NYIE PIA NI WEPESI WA KUGEUKA KWA NINI USISEME UKWELI ? AU ULITAKA KIFANYIKE NINI ?

    ReplyDelete