Na Addolph Bruno
MASHINDANO ya Kumsaka 'malikia wa Vyuo Vikuu' Miss Dar Inter Collage 2011, yanatarajia kufanyika Juni 17 mwaka huu katika Ukumbi utakaotangazwa
baadaye.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mratibu wa Mashindano hayo, Vicky Kimaro alisema maandalizi yameanza ikiwa ni pamoja na baadhi ya vyuo kufanya mashindano ya kuwapata watakaowawakilisha.
Alisema mashindano hayo yanatarajia kushishirikisha warembo 15, kutoka katika vyuo vya mbalimbali ambao wataanza mazoezi rasmi Juni 4, mwaka huu katika Ukumbi wa Brake Point uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Alivitaja baadhi ya vyuo vitakavyoshiriki mashindano hayo ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Biashara (CBE), Chuo cha Ustawi wa Jamii na Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ).
"Warembo watakaowania taji hilo wataanza mazoezi chini ya mwalimu wao, Beatrice Lukindo na tunatarajia kuwa mashindano hayo yatakuwa bora zaidi ya msimu uliopita na tutaweza kumpata mshindi atakayefanya vyema kwenye fainali ya Miss Tanzania," alisema Kimaro.
Alisema mashindano hayo yanaandaliwa na Kampuni ya Kapital Letaz Entertainment, ambapo yatadhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi Vodacom na Redds Premium Cold.
No comments:
Post a Comment