03 June 2011

Tutadhibiti wafanyabiashara CCM-Nape

Na Juddy Ngonyani,Sumbawanga

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kimeangalia upya njia ya kuwadhibiti wafanyabiashara wanaojiunga na chama hicho na kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi ndani ya chama hicho

Akizungumuza katika mkutano wa chama hicho wenye lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu nini maana chama hicho kujivua gamba  mkoani Rukwa jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Bw. Nape Nnauye alisema kuwa uamuzi huo unatokana wafanyabishara hao kutumia uwezo walio nao kuendekeza vitendo vya rushwa ilikijipatia uongozi.

Alisema kuwa hiyo ni hatua moja wapo ya chama  kujisafisha, huku akibainisha njia zitakazotumika kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.

Bw. Nnauye alisema kuwa ilifika mahali waanachi wakapoteza imani na chama pamoja na  viongozi wake jambo lililofanya chama hicho kurekebisha mambo mengi ikiwemo kutokomeza vitendo vya rushwa ama  kwa wagombea na waachama ili kukirudisha chama katika mstari unaotakiwa.

Awali Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini Bw. Aeshy Hillary pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Rukwa  Bw. Hipolitus Matete waliipongeza hatua  iliyochukuliwa na Halmashauri Kuu Taifa  ya kuwaondoa wabadhilifu  na wale wasio na maadili mema ndani ya chama hicho.

Hata hivyo Bw. Hillary alitumia nafasi hiyo pia kutoa msaada wa baiskeli kumi  kwa  baadhi ya walemavu washio katika manispaa hiyo.

9 comments:

  1. Bw Nape, Tatizo sio wafanyabiashara bali ni mfumo nyie wenyewe mliojiwekea wa kula nao!

    Sasa mkianza kuwabagua wafanyibiashara eti wanajiunga na kutumia nguvu ya utajiri kukivuruga chama ndio mtaanguka kabisaa! nyie wekeni mfumo utakaothibiti mtu kutumia uwezo wa kifedha kupata madaraka. HAMSOMI maandiko ya NYERERE?Wewe najua ulikuwa hujazaliwa enzi hizo, lakini naamini CCM inao wazee ambao wanajua vizuri tunu alizoacha Mwalimu.Tujaribu kuwasikiliza na kuwaheshimu.Huna haja ya kuzunguka nchi nzima ukiyasema hayo.Kila kitu kipo ni kufuata tu na ku-customize kwa hali ya sasa.KIDUMU CCM!

    ReplyDelete
  2. Mhh Nape kazi unayo!! Unajua kwa kipindi hiki cha ubepari..ukiwaondoa wafanyabiashsra umeua chama kwa nini ni kwamba..asilimia 80 ya wabunge na makada wa CCM ni watu matajiri kwa vigezo vya Tanzania na pia ni wafanya biashara..unadhani wakiondoka Chama hakitakuwa na wafadhili sababu wakulima Tanzania ni maskini na wanatumiwa na hao wafanya biashara kupata uongozi..Sikufichi wewe endelea kubaadilishana mippasho na Chadema sahau mambo ya CCM na Wafanya Biashara maana ndio wenye Chama wala si wewe wala Mkama..please tafuta nafasi upate unachokusudia kisha kaa uishi maisha ya pepo..ni ushauri wa Bureeee

    ReplyDelete
  3. Mh Nape ni kama ulikua unapeleka ujumbe kwa mbunge wa sumbawanga mjini Mh Aeshy,sijui nguvu za kuzungumzia watu wasio na maadili anazitoa wapi Mh Aeshy.

    ReplyDelete
  4. Kijana Nape usitudanganye lolote. Enzi zile tulidanganyika lakini sasa hivi wananchi tumeamka. Nani anayefadhili CCM kwa kiasi kikubwa kama sio hao hao wafanyabiashara? Wewe mwenyewe hapo ulipo kila Mkoa unaokwenda kufanya hiyo mikutano ya kutudanganya unafikiri hatujui kwamba gari unalotumia linawekwa mafuta na wafanya biashara hao hao unaozungumzia? Tunazo data zote kila Mkoa uliopita na majina ya wafanya biashara wanaokukarimu kwa kulipa gharama zote. Kwa hiyo Bw. mdogo Nape chunga sana mdomo wako unajua kabisa kwamba mdomo uliponza kichwa. Hivi Bw. Nape mbona wewe ni Mkuu wa Wilaya na unalipwa mshahara na wewe wewe Nape ni Katibu wa Itikadi na Uenezi na CCM inakulipa posho pamoja na per diem huko kote unakozungukia. Hizo kofia mbili ulizo nazo huo nao si ufisadi wa aina yake Bw. Nape? Uwe makini na unayobwabwaja kwenye majukwaa kwa sababu unafuatiliwa sana Nape. Hakuna Vuvuzela CCM kama alivyokuwa Bw. Yusufu Makamba je nakuuliza Bw. Nape huyu mzee yuko wapi si ameachwa kwenye system kiaina jiulize wewe utabaki kwani wewe nani haswa?

    ReplyDelete
  5. NAPE KUITWA VUVUZELA NI HAKI KWA SABABU HAJUI ANACHOKIONGEA NA ATHARI ZAKE KWA CCM. NI MTU ASIYE NA MAONO YA MBALI NA MPUMBAVU. MTU YEYOTE MWENYE BUSARA HUWA KABLA HAJAONGEA CHOCHOTE ANAPIMA NA KUWAZUA THEN AKITOA KAULI INAKUWA NA MASHIKO.CCM IMEJAWA NA WAFANYABIASHARA NA WABUNGE WAKE WENGI NI WAFANYABIASHARA NA NYINGI NI ZA SIRI. MFANO NI ROSTAM,ABOOD,SYLVESTA KOKA,MOHAMED DEWJI NA WENGINE WENGI. SASA NAPE ANASEMA WANAKUSUDIA KUPELEKA MSWADA BUNGENI AKIWA KAMA NANI? WAFANYABIASHARA SIO TATIZO NA NI NGUZO MUHIMU SANA KATIKA SISA ENDAPO WATATUMIWA VIZURI, KWA UWAZI NA KWA MANUFAA YA NCHI BILA UPENDELEO. CCM WAMEHARIBU SASA WANASINGIZIA WAFANYABIASHARA. MWENYEWE RAISI NI MFANYABIASHA?YEYE NDIYO CHANZO CHA KUCHAFUKA CCM NA WAPAMBE WAKE NA SIO WAFANYABIASHARA. CCM TATIZO NI WAONGO NA NI MAFUNDI WA KUTUNGA JAMBO ILI MRADI WAWAAMINISHE VIPOFU NA VIZIWI WACHACHE WASIOJUA MAOVU YAO/WANAYAJUA LAKINI KWA AKILI ZA KUSAHAU WANASHAWISHIKA. NAPE NI VUVUZELA TU NA HANA CHOCHOTE ZAIDI YA MCHONGNISHI NA KILAZA ASIYEJU ALAMA ZA NYAKATI. KATIKA UJANA WAKE ASIWE MZEE KFIKIEI KIASI CHA KUTOJUA UMUHIMU WA KILA MTU KATIKA NAFASI ALIYONAYO ENDAPO ATAITUMIA KWA MANUFAA YA TAIFA.NAPE AJUE KUWA HAJISEMEE BALI ANASEMEA CHAMA NA ASIPOKUWA MWANGALIFU ATAKIANGAMIZA ZAIRI NA KUZIDISHA UADUI NA MAKUNDI KATIKA CHAMA CHKE. AJICHUNGE NA AWE NA BREAK HUYU KIJANA ALIYEFIKIA KIKOMO CHA KUFIKIRI KAMA CHAMA CHAKE. WAFANYABIASHARA NDIO UHAI WA CCM NA HATA FEDHA WANAZOZITOA NDIO ZINAMWEZESHA HUYU PAPASI NAPE KWENDA MIKOANI KUTAPIKA HOVYO BILA KUFIKIRI.

    ReplyDelete
  6. huna jipya kijana nape hao mafisadi wafanyabiashara si ndio waliomwingiza bosi wako ikulu? kwa hiyo huwawezi CCM ONDOKENI MADARAKANI HARAKA KABLA NGUVU YA UMMA HAIJAWAONDOA NA KUWASHTAKI

    ReplyDelete
  7. The Heague inanukia, kaulizeni Kenya.

    ReplyDelete
  8. Nape jitahidi ujue kwanza uhalisi wako kama ni kwa Moses Nnauye au Profesa nanihi.i.i.i. La sivyo kauli unazotoa zitakurudi muda si mrefu kijana! Watu wanakujua sana Nape, huwezi kuwaamninisha lo lote kwa sababu huna jipya wewe. Unakumbuka Katibu Mkuu alishakufungia uanachama hapa duniani hata Mbinguni ukakata rufaa? Sasa hujiulizi ni kwa nini JK anakutumia kuwatuhumu marafikizake hadharani wakati yeye mwenyewe anawakumbatia sirini? Akili yake ndogo sana Nape, utafikiri hukwenda shule au ndiyo wale wale wa DESA kwa sana?

    ReplyDelete
  9. Nape hana jipya na hajui afanyalo au anaigiza. Wafanyabiashara si tatizo maana hata nchi kama Marekani matajiri ndo mhimili wa vyama. Kumbukeni hata Hayati mwalimu Baba wa taifa alisaidiwa na wafanyabiashara kama akina Lupia kuijenga TANU. Lakini alikuwa makini na wafanyabiashara wabovu hakuwapa nafasi. CCM leo haiangalii njia bora za kufanya kazi na matajiri pia imeacha ushauri wa Mwalimu Nyerere. Kinachowasumbua CCM ni laana ya Mwalimu, hawakumbuki aliwakataa KIkwete, Lowasa,na wengine lakini wao wamewakumbatia? Hadi watakapofuata mawazo ya mwasisi wa chama ndio mambo yataende vizuri ndani ya CCM.

    ReplyDelete